HAMAD, MAALIM SEIF KUMEKUCHA

Stori: Mwandishi wetu

VITA ya mahasimu wawili wa kisiasa kutoka CUF Makamu wa Rais wa kwanza wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad na Mbunge wa Wawi Hamad Rashid Mohamed, inaonekana bado mbichi baada ya mjumbe huyo wa Bunge Maalum la Katiba kumlipua bosi wake hadharani.

Makamu wa Rais wa kwanza wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad.

Jumatatu iliyopita akiwa bungeni, Hamad aliyefukuzwa uanachama wa CUF miaka michache iliyopita, alimponda Maalim Seif kwa kumuita Popo na Mfitini, akijibu mapigo ya hivi karibuni baada ya Katibu Mkuu huyo wa CUF, kusema kuwa mbunge huyo ni wakala wa CCM anayetumika kuwarubuni wabunge wa chama chake ili waingia bungeni kukamilisha akidi za Bunge Maalum.

Mbunge wa Wawi Hamad Rashid Mohamed.

Inadaiwa kuwa vita ya wawili hao imeongozeka zaidi baada ya wote kwa nyakati tofauti kutangaza kuwa watawania Urais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu ujao, wakipambana na kiongozi wa sasa, Dr Mohamed Shein.Hata hivyo haijafahamika mara moja Hamad Rashid  atasimama akigombea kwa chama kipi, kwani baada ya kufukuzwa, ameendelea kuwa mbunge kwa amri ya mahakama.Chanzo:www.globalpublishers.info

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s