Siku za Bunge la Katiba sasa zinahesabika

 

 
        Bunge Maalumu la Katiba huenda likaahirishwa kati ya sasa na Oktoba 4, mwaka huu bila kufikia kwenye hatua ya kuipigia kura Katiba inayopendekezwa. Kuahirishwa kwa Bunge hilo kunalenga kupisha mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu na Uchaguzi Mkuu wa 2015 wa rais, wabunge na madiwani. Habari kutoka ndani ya kikao baina ya Rais Jakaya Kikwete na viongozi wa vya siasa vinavyounda Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), zinasema wajumbe waliafikiana kuitishwa Bunge la Muungano ili kuzifanyia marekebisho baadhi ya sheria zinazosimamia uchaguzi. Mwenyekiti wa TCD, John Cheyo alipoulizwa na wanahabari nje ya Ikulu ndogo, Dodoma jana, alisema mazungumzo yalikwenda vizuri na kwamba mambo waliyamaliza kindugu.
 
Hata hivyo, Cheyo alikataa kueleza nini kilichojiri katika mkutano huo na kusema leo atakutana na wanahabari kuelezea walichokubaliana katika kikao hicho kilichodumu kwa takriban saa tatu. “Tumefikia makubaliano, hatuna tofauti. Hoja ambazo tulikuwa tumekwenda nazo tumekubaliana… Waambieni wananchi kikao kimekaa, kimekwenda vizuri na viongozi wa vyama wameondoka na msimamo mmoja,” alisema Cheyo. Alipoulizwa kuhusu kuahirishwa kwa Bunge la Katiba, Cheyo alisema: “Kwa nini mnanitengenezea maneno nitakayozungumza na wanahabari kesho (leo)?, Hebu niacheni tukutane kesho. Unajua nazungumza juu ya watu wengi, si ndiyo? Ni draft (niandike) vizuri niwapelekee na wenzangu wakubali, ndipo nitakuja kuwasomea hiyo taarifa ambayo mimi sitaki kutoa mambo mengine ambayo watakuja kusema umetoa mambo ambayo hayaridhishi.” Alisema hoja katika kikao hicho zilikuwa ni kuhusu Uchaguzi Mkuu wa mwakani na mchakato wa Katiba unaoendelea.
 
Alipoulizwa kuhusu kurejea bungeni kwa wajumbe wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Cheyo aling’aka: “Sasa unaona wewe ndiyo ajenda yako, niache niende, asante sana.” Cheyo alitoa taarifa hiyo akiwa ndani ya gari baada ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali kumsimamisha ili awape muhtasari wa kile kilichojiri kwenye kikao hicho ambacho ni mwendelezo ya kile kilichofanyika Agosti 31, mjini hapa. Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa waligoma kuzungumza chochote wakimrushia mpira Cheyo. Hata Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia alipotafutwa alisema wamekubaliana kuwa Cheyo ndiye atakayezungumza na wanahabari kwa niaba yao kama ilivyokuwa pia kwa Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema.
 

Viongozi wengine waliohudhuria kikao hicho ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula na Katibu Mkuu wake, Abdulrahman Kinana.
 
Kusitishwa kwa Bunge
 
 
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s