MATOKEO YA HARAMBEE YA TAASISI YA MKAPA ILIYOFANYIKA MWANZA 23 AGOSTI 2014

Kwa niaba ya Msarifu wa Taasisi Mhe. Benjamin William Mkapa, Bodi ya Wadhamini, Menejimenti na wafanyakazi wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa tunatoa shukrani za dhati kwa kuweza kufanikisha harambee ya kuchangia. Mradi wa Mkapa Fellows, iliyofanyika jijini Mwanza siku ya Jumamosi, tarehe 23 Agosti 2014 katika ukumbi wa Hotel ya JB Belmont.

Harambee iliyohudhuriwa na wageni karibia 230 iliongozwa na Waziri Mkuu wa Tanzania,Mhe Mizengo Pinda ambae alikuwa mgeni rasmi akiambatana na Raisi mstaafu,Mhe. Benjamin W. Mkapa pamoja na Mama Anna Mkapa. 

Harambee hii iliyofanyika na Taasisi ya Benjamin W. Mkapa ni ya mara ya kwanza kutekelezwa na Taasisi nje ya Mkoa wa Dar Es Salaam. Kwa hatua za awali tuliamua kuanzia katika Kanda ya Ziwa,na kuwashirikisha washikadau waliopo katika mikoa sita (6) ya Kanda ya Ziwa. Harambee ilifanikiwa kukusanya kiasi cha Tshs 1.38billioni na hivyo kuvuka lengo lililowekwa la kukusanya kiasi cha Tsh 500 millioni katika Kanda hiyo.

Kiasi kilichokusanywa kitatumika kutekeleza mradi wa Mkapa Fellows unaoendeshwa na Taasisi ya Benjamin W. Mkapa kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania. Mradi huu wa Mkapa Fellows unatekelezwa katika mizunguko miwili; ambapo mzunguko wa kwanza ulianza Januari 2013 na utamalizika Desemba 2014 na ulifikia Halmashauri sita (6) nchini za Sumbawanga vijijini, Kalambo, Nkasi, Msalala, Kishapu na Biharamulo. Baadhi ya mafanikio ya mradi huu hadi leo, ni pamoja na tumeshaajiri na kuwapeleka katika wilaya hizo 6 wataalam wa afya 30 kati ya lengo la miaka mitano la watalaam 180, na pia ujenzi wa vyumba vya upasuaji 9 kati ya 30 umeshakamilika, na ununuzi na uwekaji wa vifaa vya kutolea huduma pia kukamilika. Fedha za utekelezaji wa mzunguko huu wa kwanza zilifanikiwa kupatikana kupitia mfadhili wa Serikali ya Ireland na wafanyabiashara zaidi ya 50, wakiwemo pia Kampuni ya African Barrick Gold.

Mzunguko wa pili wa huu mradi utaanza Januari 2015 mpaka Desemba 2017 na utafikia Halmashauri 9 za Shinyanga vijijini, Kahama,Meatu, Bariadi, Itilima, Busega, Maswa,,Chake Pemba na Mkoa wa Kati Unguja. Continue reading →

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s