Jaji Warioba: Namshangaa Sitta

Na Elias Msuya, Mwananchi

Dar es Salaam. Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, amesema anashangazwa na Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta kung’ang’ania kuendelea na Bunge hilo licha ya Rais Jakaya Kikwete kuridhia lifikie kikomo Oktoba 4 mwaka huu.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, Jaji Joseph Warioba akizungumza na mhariri wa gazeti hili Julius Magodi (Kulia) na mwandishi wa habari Elias Msuya jijini Dar es Salaam. Picha na Said Khamis

Hivi karibuni, Rais Kikwete alikutana na viongozi wa vyama vya siasa vilivyo chini ya Kituo cha Demokrasia (TCD) na kukubaliana kusitisha mchakato wa Katiba hadi baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Akizungumza katika mahojiano maalumu wiki hii jijini Dar es Salaam, Jaji Warioba alisema ameshangazwa na uongozi wa Bunge Maalumu la Katiba kuendelea na vikao wakati uwezekano wa kukamilisha mchakato haupo.
“Hivi kuna haraka gani ya kuwa na rasimu katika Bunge hili? Mimi nilivyoelewa makubaliano ya Rais na TCD ni kama walikuwa wanasema kwa ustaarabu hebu twende polepole. Nimeambiwa kuwa Rais alitoa muda mpaka Oktoba 4, lakini uongozi wa Bunge ukapanga mpaka mwisho wa Oktoba,” alisema Jaji Warioba na kuongeza:
“Mimi nafikiri makubaliano kati ya Rais na viongozi wa vyama ni kukataa kuongeza muda. Hiyo kwangu ni lugha ya kistaarabu kwa Bunge kwamba hamwezi kumaliza kazi hii kwa kipindi hiki,” alisema Jaji Warioba.
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s