Balozi Sefue afunguka Katiba Mpya

Na Elias Msuya, Mwananchi

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue amesema hakuna uwezekano wa kubadili muundo wa muungano kutoka Serikali mbili kwenda Serikali tatu katika mchakato wa Katiba.

Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue.

Kauli ya Balozi Sefue imekuja ikiwa ni siku chache tangu Rais Jakaya Kikwete kukutana na viongozi wa Kituo cha Demokrasia (TCD) na kutoa uamuzi wa kuahirisha mchakato wa Katiba hadi baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Suala la muundo wa muungano lilichukua mjadala mkali ndani ya Bunge Maalumu la Katiba huku wajumbe wanaounda kundi la Ukawa wakiunga mkono mapendekezo ya Rasimu ya Katiba ya muundo wa Serikali tatu na wajumbe wa CCM wakisisitiza muundo wa Serikali mbili.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili, Balozi Sefue alisema mchakato wa Katiba unahitaji maridhiano, lakini suala la muundo wa muungano halina maridhiano katika jamii hivyo litachelewesha upatikanaji wa Katiba:
“Katika historia ya nchi yoyote, wakati unafika wananchi wakawa na maridhiano fulani, wakaamua kuyaingiza ndani ya Katiba. Tatizo linajitokeza pale watu au makundi fulani yanapong’ang’ania kuingiza ndani ya Katiba mambo ambayo ni dhahiri hayana maridhiano ndani ya jamii. Mfano ni suala la muundo wa Muungano,” alisema na kuongeza:
“Uzoefu wa Bunge Maalumu hadi sasa ni kuwa hakuna uwezekano wa kupata maridhiano ya kubadili muundo wa Muungano kutoka Serikali mbili kwenda tatu. Hutapata maridhiano hayo ndani ya Bunge Maalumu na hutapata maridhiano ukienda kwa wananchi,” alisema.
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s