JENGA TANZANIA FOUNDATION YAWALETEA KIPIMO CHA MALERIA PAPO HAPO

Mwanadiaspora Mtanzania na Mkurugenzi wa JENGA TANZANIA FOUNDATION Bw. Nasoro Ally akitambulisha rasmi Home Malaria Kit katika mkutano wa Africa Diaspora Market Place (ADMP III) uliofanyika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani tarehe 10/27/2014.
Akizungumza katika mkutano huo, Bw.. Nasoro Ally alieleza kuwa bado Malaria ni tishio kubwa la uhai kwa Sub-Sahara Africa na ni chanzo cha vifo vya watoto wadogo hasa chini ya umri wa miaka 5 .
Kipimo hicho chenye uwezo wa kugundua vijidudu vya Malaria mwilini kati ya dakika 5 hadi 10 kimekubalika na shirika la World Health Organization (WHO) kama kipimo sahihi na cha haraka kwa upimaji wa Malaria nyumbani. Bw. Nassoro aliongeza kusema, kipimo hicho kitatolewa bure nchini Tanzania kwa familia zisizojiweza na kuhakikisha kinafika sehemu mbali mbali za ndani hasa mikoani na vijijini ili kurahisisha upatikanaji wa huduma sahihi za afya na kufupisha safari ndefu na zenye milolongo.
Mkurugenzi wa JENGA TANZANIA foundation Bw. Nasoro Ally na Mwanasayansi msaidizi wa JENGA TANZANIA, Da. Asha Nyanganyi wakitambulisha rasmi kipimio cha nyumbani cha Malaria kwa Mhe. Balozi Liberatous Mumulala na wawakilishi wa USAID waliohudhuria mkutano huo.
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s