SANKARA ALIKUWA KIONGOZI WA VITENDO

sankara_9bc73.jpg
Alitinga Ikulu kudai Rais atoe fedha kununulia pampu ya maji..!

Kwenye kitabu ‘ Sankara, Nguvu Mpya Ya Afrika’, Captain Thomas Sankara anasimulia kisa cha kutinga Ikulu ya Rais kudai pampu ya maji. Wakati huo Sankara alikuwa mkuu wa kikosi cha makomandoo kwenye mji wa Po. Kambini kulikuwa na shida ya maji, lakini, Sankara aliona uchungu pia kuwaona wananchi waliozunguka kambi wakiwa kwenye shida hiyo kubwa ya maji. Alizunguka kwenye taasisi mbali mbali zikiwamo za dini kuwaomba msaada wa pampu ya maji. Hakupata.
Asubuhi moja Sankara, akiwa na cheo cha Luteni, alivaa mavazi ya kijeshi na akabeba silaha yake pia. Akamuamuru dereva wake waendeshe gari hadi Ouagadogou. Alipofika mjini akamuamuru mwenye duka amuuzie pampu na aandike maombi ya kulipwa fedha zake kwa anwani ya Ikulu.
Kisha Sankara akafika mpaka Ikulu. Akapata muda wa kuonana na Rais Lamizana.
Rais alishangaa kwanza kumwona Luteni ameingia ofisini wakati Rais ni Jenerali. Sankara alisema: Wewe ni Jenerali na mimi ni Luteni, lakini wote sisi ni maofisa wa jeshi. Huko kwenye field watu hawana maji. Naomba fedha ya kununua pampu ya maji.
Jenerali Lamizana haraka sana akamwandikia Luteni Thomas Sankara cheki ya kwenda nayo kumlipa mwenye duka alikonunua pampu ya maji…!(VICTOR SIMON)

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s