Mbowe afichua ufisadi mzito bomba la gesi

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Taifa, Freeman Mbowe, amefichua tuhuma za ufisadi wa kutisha akisema kuwa gharama ya ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam imeongezwa maradufu huku kiasi kilichoongezwa kikiwa ni hongo kwa viongozi wa serikali na jamaa zao.

Katika madai hayo aliyoyatoa juzi jioni katika Uwanja wa Barafu mjini Igunga na kurejea jana Uwanja wa Parking Nzega mjini, Mbowe amesema kuwa ufisadi huo unahusisha viongozi wa Serikali ya CCM, ndugu zao wa kifamilia na maswahiba katika biashara.
Alisema kuwa, ufisadi huo umewashtua hata nchi wahisani ambao Tanzania imekuwa ikiwategemea katika bajeti za kuendesha shughuli za maendeleo, akiongeza kuwa hata utegemezi huo ni dalili ya matokeo ya ufisadi na kutowajibika.
Mbowe ambaye jana alizindua rasmi operesheni ya chama hicho inayoitwa ‘Operesheni Delete CCM’ (ODC), ikiwa inakiandaa chama hicho kuelekea kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Uandikishaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, Kura ya Maoni ya Katiba Mpya na Uchaguzi Mkuu mwakani, ameitaka Serikali kuwajibika katika hilo.
Akizungumza kwa msisitizo kuhusu tuhuma hizo, huku akirejea kashfa mbalimbali kubwa ambazo zimekuwa zikihusishwa na Serikali ya CCM, Mbowe alisema kuwa kashfa hiyo ya sh trilioni 2 ambazo ni fedha za mkopo zitakazolipwa na Watanzania maskini, imevunja rekodi.
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s