Mbowe: Tabora ni kama vile wamepewa limbwata na CCM

Na Raymond Kaminyoge na Mussa Juma, Mwananchi

Igunga/Hai. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema wananchi wa Mkoa wa Tabora ni kama wamepewa limbwata na CCM na kuendelea kutoa majimbo yote 10 kwa chama hicho licha ya mkoa huo kuwa miongoni mwa mikoa maskini nchini.
NUKUU “Wana-Tabora ni kama vile mmepewa limbwata na CCM, majimbo yote 10 ya uchaguzi mmewapa CCM lakini mnaendelea kuwa maskini siku hadi siku, badilikeni” Mbowe.

Mbowe alisema hayo jana katika Kijiji cha Choma wilayani Igunga akiwa ziarani katika mikoa ya Tabora, Katavi, Kigoma, Singida, Morogoro na Dodoma.

Jana, Mbowe akitumia chopa, alifanya mikutano mitano katika maeneo ya Bukene Mjini, Mwamali katika Wilaya ya Nzega na maeneo ya Choma, Igulubi na Igunga Mjini.
“Wana-Tabora ni kama vile mmepewa limbwata na CCM, majimbo yote 10 ya uchaguzi mmewapa CCM lakini mnaendelea kuwa maskini siku hadi siku, badilikeni,” alisema Mbowe ambaye pia ni kiongozi wa Upinzani Bungeni.
Mkoa wa Tabora una majimbo ya Tabora Mjini, Igunga, Nzega, Bukene, Sikonge, Igalula, Tabora, Tabora Kaskazini, Urambo Mashariki na Urambo Magharibi ambayo yote yanaongozwa na wabunge wa CCM.
Alisema wakulima wa Tabora wanaolima mpunga bado wanakabiliwa na hali mbaya ya kiuchumi kwa sababu CCM inakumbatia matajiri kwa kuwapa vibali vya kuingiza mchele kutoka nje ya nchi.
“Mchele wa nje ukiingizwa nchini unauzwa kwa bei rahisi wakati mchele wenu unakosa soko na kusababisha hali ngumu, hiyo ndiyo CCM yenu mnayoipenda,” alisema.
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s