Ripoti IPTL yavuja

RIPOTI ya uchunguzi wa kashfa ya kuchota fedha zaidi ya sh bilioni 200, zilizohifadhiwa kwenye Akaunti Maalum ya Escrow katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), inadaiwa kuvuja, Tanzania Daima Jumapili, limedokezwa.
Ripoti hiyo iliyotokana na uchunguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), tayari imetua mikononi mwa Spika wa Bunge na jana ilikabidhiwa kwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC). inayoongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA).
Zitto ambaye aliwasili jana mjini hapa na kuingia moja kwa moja kwenye kikao cha Kamati ya Uongozi, alisema baada ya kikao hicho atajua Kamati yake itakutana lini na uongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ili waweze kufanya kazi yao vizuri.
Mbunge huyo (Zitto) naye anadaiwa kugawiwa fedha za IPTL sh milioni sita kwa ajili ya matibabu ya marehemu mama yake Shida Salum, aliyetakiwa kupelekwa nchini India
Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili, Zitto alisema watu wanaowashambulia katika kusimamia sakata la upotevu wa fedha za Tegeta Escrow wamepewa pipi kwa nia ya kuwaondoa watanzania katika mstari, huku waliowapa pipi hizo wakiwa wanafaidi mabilioni ya watanzania.
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s