MILLEN MAGESE AMSAPRAIZ JOKATE


Mwanamitindo maarufu Bongo, ambaye anafanya kazi zake nje ya nchi Happyness Magesse ‘Millen’.

Stori: Imelda Mtema

Mwanamitindo maarufu Bongo, ambaye anafanya kazi zake nje ya nchi Happyness Magesse ‘Millen’ ambaye pia alishawahi kunyakua taji la Miss Tanzania 2001, ‘amemsapraiz’ mwanamitindo na mbunifu Jokate Mwegelo, kwa kumpatia keki yenye sura ya mdomo wake.

Read more…

TAARIFA YA UFAFANUZI WIZARA YA NISHATI NA MADINI


Katika gazeti la NIPASHE la Jumatatu tarehe 08 Desemba, 2014 ziliandikwa habari kuhusu Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (Mb) chini ya kichwa cha habari “Wanaomtetea Muhongo Wajibu haya”. Hoja zilizotolewa katika gazeti hilo zililenga kupotosha ukweli. Wizara inapenda kutoa maelezo kuhusu hoja zilizotolewa kama ifuatavyo:

Utendaji wa Wizara chini ya Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (Mb)

Read more…

Wenger amwinda beki wa Real Madrid


Sergio Ramos wa Real Madrid.Kocha wa Arsenal adaiwa kummezea mateMeneja wa Arsenal Arsene Wenger amewasiliana na ajenti wa beki wa Real Madrid Sergio Ramos kuhusu uwezekano wa mchezaji huyo kujiunga na kilabu hiyo ya uwanja wa Emirates.

Ramos mwenye umri wa miaka 28 amekuwa na kilabu hiyo ya Los Blancos kwa takriban muongo mmoja baada ya kuwasili kutoka sevilla kwa kitita cha pauni millioni 20 mwaka 2005.

Read more…

Ufisadi ni zao la Kutokuwa na hofu ya Mungu


Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Alex Malasusa akihubiri katika ibada ya Krisimasi ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Yesu Kristo katika Kanisa la Azania Front jijini Dar es Salaam

Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Alex Malasusa amesema watanzania wengi hivi sasa wamekosa kitu muhimu na cha thamani katika maisha yao, ambacho ni kutokuwa na hofu ya Mungu.CHANZO:MWANANCHI

Read more…

Taarifa Maalum Kwa Umma Kutoka IKULU:Rais Jakaya Kikwete Atazungumza na Wazee wa Mkoa wa Dar Es Salaam Leo Mchana wa Jumatatu, Desemba 22, 2014.


Rais Jakaya Kikwete

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete atazungumza na Wazee wa Mkoa wa Dar Es Salaam, mchana wa Jumatatu, Desemba 22, 2014.

Wakati wa mazungumzo yake na Wazee hao, Rais Kikwete atazungumzia masuala mbali mbali ya kitaifa, yakiwemo yale ambayo yamekuwa yanasubiri maamuzi yake tokea alipokuwa anajiuguza kufuatia upasuaji aliofanyiwa mwezi uliopita, Novemba 2014.Undani zaidi kuhusu mkutano huo kama vile mahali utakapofanyika, saa utakapofanyika na nani wataalikwa utatolewa na mamlaka zinazohusika na maandalizi ya mkutano huo.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
19 Desemba, 2014

Escrow:Je Kikwete atategua kitendawili?


Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete leo atalihutubia taifa la nchi hiyo ambapo anatarajiwa kuyatolea ufafanuzi masuala nyeti yanayoligusa taifa hilo.

Wadadisi wa masuala ya kisiasa na kijamii wanatabiri huenda hatua atakazozichukua dhidi mawaziri na maafisa wa serikali waliohusika na ufisadi wa mamilioni ya fedha katika akaunti ya Escrow itakuwa ni moja kati ya agenda muhimu atakayoitolea ufafanuzi.

Hotuba hiyo inakuja wakati kukiwa na shinikizo kutoka kwa baadhi ya raia na wapinzani wakitaka hatua zaidi zichukuliwe kutekeleza azimio la bunge ambalo linatataka mawaziri na maafisa wa serikali waliohusika na sakata hilo la ufisadi wawajibishwe ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kazi.

Read more…