Dk.BILAL KUWEKA JIWE LA MSINGI CHUO KIKUU CHA BAGAMOYO

MAKAMU wa Rais, Dk.Mohammed Gharib Bilal (pichani) Desemba 2 anatarajiwa Kuwa mgeni rasmi katika sherehe za uwekwaji wa jiwe la Msingi la Chuo Kikuu Cha Bagamoyo(UB), zitakazofanyika Kijijini Kiromo,Bagamoyo Mkoani Pwani. Akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake Mikocheni Dar es Salaam Ofisa Habari wa (UB), Happiness Katabazi alisema sherehe hizo zitafanyika Kijijini Kilomo Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani na kwamba uwekwaji wa jiwe hilo ni ufunguzi rasmi wa ujenzi wa Chuo Kikuu Cha Bagamoyo Katika Kijiji hicho ambao utaanza mapema Januari Mwaka 2015. Katabazi alisema Dk. Bilal ndiye atakuwa mgeni rasmi katika sherehe hiyo ya kihistoria katika Wilaya ya Bagamoyo kwasababu Somo la Historia linatufundisha kuwa mji wa Bagamoyo ilikuwa ukikaliwa na watumwa. ” Sasa sisi UB tunaitambua hiyo historia na ndiyo maana tukaamua kuanzisha Chuo Kikuu ambacho tumekipa jina la Bagamoyo.Na kwakuwa kupitia Mji wa Bagamoyo tulikuwa watumwa, basi sasa kupitia UB ambayo inajenga makazi yake ya kudumu katika mji huo, binadamu wote watakuwa huru kwasababu tutapata elimu” alisema Katabazi. Alisema UB ambayo ilianzishwa rasmi mwaka 2011 ambayo ina makazi yake yake ya muda ,Mikocheni ,Dar es Salaam na kwamba ujenzi wa Makazi ya kudumu ya UB kijijini Kilomo , utasaidia kukuza shughuli za uchumi, wananchi wa eneo hilo kupata huduma ya elimu ya ngazi ya Chuo Kikuu kwa ukaribu. Aidha aliwaomba wananchi Wilaya Bagamoyo na Mkoa wa Pwani kwa ujumla kujitokeza kwa Wingi Katika sherehe hiyo. UB ilianzishwa rasmi Mwaka 2011. Chanzo: Gazeti la Tanzania Diama, Jumatatu, Desemba Mosi Mwaka 2014

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s