PICHA NA TAARIFA RASMI KUTOKA OFISI YA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS IKULU: MHESHIMIWA MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AMUWAKILISHA RAIS JAKAYA KIKWETE KWENYE MKUTANO WA MAZINGIRA (COP20) JIJINI LIMA, PERU DESEMBA 10,

  Katibu Mkuu, Ban Ki-Moon, akizungumza katika mkutano huo……..
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia katika Mkutano wa 20 wa Kimataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, unaoendelea Jijini Lima nchini Peru. Makamu wa Rais alizungumza kwa niaba ya nchi za Afrika kuhusu utekelezaji wa maazimio mbalimbali ya mabadiliko ya tabianchi. Pamoja na mambo mengine Dkt. Bilal alizungumzia namna nchi za Afrika zilivyojizatiti katika maazimio mbalimbali yanayolenga kunusuru majanga yatokanayo na Tabianchi.
 Ujumbe wa Tanzania, katika mkutano huo…..
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipiga picha ya kumbukumbu na Mkuu wa Ujumbe wa China, katika mkutano wa Mkutano wa 20 wa Kimataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, Xie Zhenhua, wakati walipokutana kwa mazungumzo baada ya kuhudhuria na kuhutubia katika mkutano huo unaoendelea Jijini Lima nchini Peru, ambapo  alizungumza kwa niaba ya nchi za Afrika kuhusu utekelezaji wa maazimio mbalimbali ya mabadiliko ya tabianchi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mjumbe maalum wa Marekani katika masuala ya Mabadiliko ya Tabianchi, Todd Stern, baada ya kuhudhuria katika Mkutano wa 20 wa Kimataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, unaoendelea Jijini Lima nchini Peru, ambapo  alizungumza kwa niaba ya nchi za Afrika kuhusu utekelezaji wa maazimio mbalimbali ya mabadiliko ya tabianchi.
  Makamu wa Rais na ujumbe wake …….
 Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya Mawaziri wakati wakitoka katika chumba cha mkutano huo
 Taswira ya kumbi za mikutano hiyo.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
—-
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA MAKAMU WA RAIS
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal jana Desemba 09, 2014 amemuwakilisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ni Mwenyekiti Kamati ya Wakuu wa Nchi na Serikali Barani Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi, kwenye mkutano wa Kimataifa wa Mazingira Duniani (Cop20) unaofanyika jijini Lima, Peru.
read more

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s