Lipumba agonganisha mihimili yote ya nchi


Na Boniface Meena, Mwananchi

Dodoma. Mjadala kuhusu sakata la polisi kumpiga na kumtia mbaroni Profesa Ibrahim Lipumba jana ulikuwa mkali, lakini uliweka bayana kugongana kwa mihimili mitatu ya nchi baada ya Bunge kujadili suala hilo wakati likiwa limeshafika mahakamani.

Mbunge wa kuteuliwa, James Mbatia akizungumza wakati wa kuhitimisha hoja yake kuhusu vurugu zilizotokea juzi jijini Dar es Salaam wakati viongozi na wafuasi wa CUF walipopigwa na kukamatwa na polisi. Picha na Edwin Mjwahuzi

Mgongano huo umetokea katika kipindi kisichozidi miezi miwili baada ya Bunge kugoma kupokea zuio la Mahakama la kujadili kashfa ya uchotwaji fedha kwenye Akaunti ya Tegeta Escow na kuendelea na mjadala ambao ulifikia maazimio ya kuwawajibisha wahusika.
Tukio lililojadiliwa jana lilitokana na Profesa Lipumba kukamatwa Jumanne wiki hii wakati akielekea Zakhem, Mbagala ambako alidai alikuwa akienda kutawanya wafuasi wa chama hicho baada ya Jeshi la Polisi kuzuia maandamano na mkutano wa hadhara wa chama hicho ulioandaliwa kwa ajili ya kukumbuka wafuasi 22 waliouawa mwaka 2001 wakati wakiandamana kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2000.
Wakati mbunge wa kuteuliwa, James Mbatia aliwasilisha hoja juzi majira ya saa 5.00 asubuhi kutaka Bunge lisitishe shughuli zake na kujadili suala hilo aliloliita “la dharura, kwa maslahi mapana ya Taifa”, Jeshi la Polisi lilimfikisha Profesa Lipumba mahakamani siku hiyohiyo lakini alasiri.
Jana, baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe kutoa taarifa ya Serikali kuhusu tukio hilo na kuomba radhi kwa yaliyotokea huku akiahidi uchunguzi kwa waliohusika kutumia nguvu kupita kiasi, Spika Anne Makinda alimsimamisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju kuzungumza.
Masaju alijaribu kuzima mjadala huo kwa maelezo kuwa tayari Profesa Lipumba ameshafunguliwa mashtaka mahakamani, hivyo haingekuwa busara kwa Bunge kujadili suala hilo.
Advertisements

Sherehe za Ufunguaji wa Majengo ya Ubalozi wa Tanzania Nchini Ufaransa


  Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe Mhe Begum Taj akikaribisha wageni baada ya  Rais Jakaya Mrisho Kikwete kufungua rasmi majengo ya ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa yaliyoko jijini Paris Jumatano jioni Januari 28, 2015.
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe akikaribisha wageni baada ya  Rais Jakaya Mrisho Kikwete kufungua rasmi majengo ya ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa yaliyoko jijini Paris Jumatano jioni Januari 28, 2015.
 Rais Jakaya Kikwete akizungumza na wageni baada ya   kufungua rasmi majengo ya ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa yaliyoko jijini Paris Jumatano jioni Januari 28, 2015.
  Rais Jakaya Kikwete akisalimia na wageni baada ya   kufungua rasmi majengo ya ubalozi wa Tanzania nchini Ufaransa yaliyoko jijini Paris Jumatano jioni Januari 28, 2015.

Jaji Warioba: Rais ajaye anafahamika


Na Florence Majani, Mwananchi

Dar es Salaam. Wakati Taifa zima likiwa katika kitendawili cha kumjua kiongozi wa nchi atakayepatikana baada ya Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu, Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema Rais ajaye anafahamika.
Jaji Warioba

Akizungumza katika mahojiano maalumu jana, Jaji Warioba alisema si kazi ngumu kwa Watanzania kumfahamu rais ajaye kwa kuwa katika miaka 50 tangu tupate uhuru, Watanzania wanazijua sifa za kiongozi bora.

Jaji Warioba alisema; “Tatizo la kumjua rais afaaye tunalikwepa lakini linafahamika. Wanaotumia fedha na lugha chafu katika kampeni na hao ndiyo wasiotakiwa.”
“Katika miaka 50 tunazijua sifa za kiongozi bora. Hapa tunakwepa tatizo tu. Tatizo ni matumizi ya fedha na lugha chafu katika kampeni,” alisema Jaji Warioba ambaye pia ni waziri mkuu mstaafu.
Hadi sasa wanasiasa zaidi ya 20 wakiwamo wa CCM na upinzani wamekuwa ama wanatajwa au wameonyesha nia ya kugombea nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu ujao.
Ukiacha wale wanaotajwa, wanasiasa waliotangaza nia hiyo kutoka CCM ni Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, Mbunge wa Nzega, Hamis Kigwangala na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, huku Mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed akitangaza nia kupitia ADC.
Akifafanua zaidi, Jaji Warioba alisema kila mtu anaweweseka kuhusu kiongozi anayefaa ingawa ni kazi rahisi kumjua kutokana na ujuzi tulionao wa miaka zaidi ya 50 ya uhuru.
Kadhalika, Jaji Warioba alisema viongozi wa Serikali hawana budi kuangalia taswira ya uchaguzi mkuu ujao kupitia uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao umeonekana kuwa na kasoro zilizosababisha vurugu.

WAMPINGA KABILA KUWANIA URAIS NCHINI DRC


Rais wa Drc Congo Joseph Kabila

Polisi nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wamewafyatulia risasi waandamanaji kwenye mji mkuu Kinshasa walio na hasira katika kile kinachoonekana kama jitihada za kutaka kuongoza uongozi wa rais Joseph Kabila.

Watu kadha walitolewa eneo la kati kati mwa mji wakiwa na majeraha ya risasi ambapo pia kulitoka makabiliano kwenye chuo kikuu cha mji huo.

Milio ya risasi iliripotiwa katika maandamano mengine katika mji ulio mashariki wa Goma.

Read more…

24/1/2015 ndani ya leaderz club. kutakuwa na bonge la show. …TigoMusictz


wasanii 18 stage moja.
instagram @tigomusictz

Diamond
ali kiba
linah
vannesa mdee
shaa
shilole
khadija kopa
isha mashauzi
joh makini
niki wa pili
gnako
fid q
mwana fa
Ay
prof jay

On 1 Dec 2014 15:39, “Wakazi” <wakaziwavina@gmail.com> wrote:

Youtube Link: http://youtu.be/ua9orsQHvoI

Hii ndio video mpya ya Lady Jaydee aliyomshirikisha Dabo inayoitwa “Forever”.

Video ya wimbo huo imefanywa na muongozaji mkongwe Adam Juma wa Next Level, na imeshootiwa on location  ndani ya jiji la Johannesburg, South Africa. Wimbo umetayarishwa na producer mahiri Man Water wa Combination Sounds.

 
for more information please follow

Instagram: @jidejaydee @dabomtanzania
Twitter: @jidejaydee @dabomtanzania
Facebook: @ladyjaydee

Notice from Tanzania Bureau of Standards (TBS) to all motor vehicle importersThe Tanzania Bureau of Standards (TBS) started to inspect used motor vehicles in 2002, since then international tenders are advertised to look for qualified agents/companies to inspect vehicles on behalf of TBS. The former tender expired in 2014 hence TBS re-advertised international tender for inspection of used motor vehicles from Japan and United Arab Emirates. Companies which won international tender and their inspection fee charges are as follow:
With effect from 1st January 2015 the mentioned above companies will be inspecting used vehicles on behalf of Tanzania Bureau of Standards. Please note that the above mentioned inspection fee are fixed.

Therefore we remind all importers of used motor vehicles from Japan and United Arab Emirates that, it is a MUST to inspect all used motor vehicles before they are shipped to Tanzania.

Legal action will be taken against whoever contravene with this notice. This will include 30% penalty of CIF value plus inspection fee at destination point of USD 140 and USD 125 for used vehicles from Japan and United Arab Emirates respectively.

For further information contact:

 

Director General

Tanzania Bureau of Standards

P. O. BOX 9524

Dar es Salaam

 

Tel: +255-22-2450206

Hotline: +0800110827

Email: info@tbs.go.tz

Website: www.tbs.go.tz 

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano Wa Kimataifa John Haule Akutana na Mabalozi wa Tanzania Nchi za Nje Waliopanda Mlima Kilimanjaro


 Katibu mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Mataifa Bw. John Haule (Wa tatu kulia) akizungumza na baadhi ya waheshimiwa Mabalozi waliopanda mlima Kilimanjaro mwezi uliopita.
Baadhi ya waheshimiwa Mabalozi waliopanda mlima Kilimanjaro wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Haule.Picha na Reuben Mchome.