Dkt. Ghalib Bilal: matumizi bora ya teknolojia ya habari yatawawezesha wanafunzi kupata elimu bora

unnamed5V

Na Maryam Kidiko/Kijakazi Abdalla Maelezo Zanzibar 

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohd Gharib Bilali amesema kuwa matumizi bora ya teknolojia ya habari yatawawezesha wanafunzi kupata elimu bora kwa urahisi.

Hayo ameyasema leo  katika skuli ya Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi Unguja wakati  wa uzinduzi wa darasa la kompyuta  ikiwa ni  miongoni mwa shamrashamra za kutimiza miaka 51 ya Mapinduzi  ya Zanzibar.

Alisema kuwa matumizi bora ya kompyuta yatawafanya wanafunzi kuimarika vizuri kielimu wakati dunia  hivi sasa imo katika mfumo  wa matumizi ya teknolojia ya mawasiliano ya habari.

Alisema kuwa teknolojia ya habari imekuwa kwa kiwango kikubwa jambo ambalo limekuwa likichangia ukuaji wa uchumi katika  Taifa

Amewashauri wanafunzi kutumia maendeleo ya teknolojia hiyo  kwa mambo yanayoweza kuwasaidia katika maendeleo ya masomo yao na maisha ya baadae.

“Vijana itumieni  teknolojia hii  katika njia zilizosahihi   ili iweze kuwaletea  faida” alisema Dkt. Bilali.  .

Amewataka wanafunzi  waongeze bidii  zaidi ili  waweza kumudu masomo hayo na kuleta maendeleo  katika jamii na nchi kwa ujumla .

Alisema kuwa matumizi ya komputa yanarahisisha kufundisha wanafunzi kwa njia rahisi na kuweza kujifunza mambo mbalimbali kupitia teknolojia hiyo na kupelekea kutanuka  kiakili.

Aidha Dkt. Bilali ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya watu wa china kupitia kampuni ya ZTE kwa msaada wa kompyuta 50  na kuhakikisha kuwa teknolojia hiyo inaenea kwa kiasi kikubwa.  

Dkt. Bilali amesema msaada huo utaweza kuleta changamoto zaidi kwa wanafunzi na  kuwa  na wataalamu wengi waliobora kwa  maendeleo ya taifa

Amesema  kuwa Serikali inathamini sana michango inayotolewa na marafiki wa maendeleo na Serikali itahakikisha michango hiyo inakuwa na faida kubwa kwa Taifa.

Katika risala  yao walimu wa skuli ya Kiembesamaki  wameiomba Serikali kuwawekea Uzio katika Eneo la skuli pamoja na usafiri kwa walimu na Wanafunzi.

Skuli  ya Kiembesamaki  Sekondari inajumla ya Wanafunzi 1,800 kwa sasa na katika sherehe za uzinduzi huo Dkt. Bilal amechangia shilingi milioni 10 kwa ajili ya maendeleo ya skuli hiyo.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s