Mwanasheria Mkuu aahidi kuanza na mikataba tata

Na Fidelis Butahe, Mwananchi Dar es Salaam. Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju amesema ataanza kuipitia mikataba yote inayodaiwa kuwa na utata ili aweze kutoa ufafanuzi wa kina lakini akawataka Watanzania wampe muda. Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi vitendea kazi Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju baada ya kumwapisha katika hafla iliyofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam jana. Picha na Salim Shao Hata hivyo, alisema hadhani kama watu wanaosema kuwa baadhi ya mikataba iliyoingiwa na Serikali ina utata wako sahihi na kuwataka Watanzania kuwa na imani na Serikali iliyopo madarakani. “Watu wanasema hivyo ila kuna jambo moja ambalo wanatakiwa kujua kuwa kuna baadhi ya mikataba ambayo ni siri,” alisema. Masaju aliteuliwa na Rais Jakaya Kikwete mwishoni mwa wiki kuchukua nafasi ya Jaji Frederick Werema ambaye alijiuzulu kutokana na sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow. Jaji Werema aliomba kujiuzulu kwa sababu ushauri wake kuhusu suala hilo haukueleweka na badala yake kuchafua hali ya hewa. Kabla ya uteuzi huo, Masaju alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Kuhusu uteuzi wake, alisema; “Nina furaha kwa sababu ninalitumikia Taifa na kuteuliwa kwangu kunaonyesha kuwa Serikali ina imani na mimi.” Licha ya kubanwa na wanahabari kuwa kwa nafasi aliyokuwa nayo awali anafahamu maeneo yenye matatizo, ikiwamo na mikataba yenye utata, alisisitiza kuwa apewe muda zaidi. Read more »

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s