Taarifa ya UTEUZI Kutoka IKULU:Rais Jakaya Kikwete Amteua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dkt. Hamisi Hassan Mwinyimvua (pichani) kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, anayesimamia Menejimenti ya Fedha za Umma (Public Finance Management). Kabla ya uteuzi wake, Dkt. Mwinyimvua alikuwa Msaidizi wa Rais wa muda mrefu wa masuala ya uchumi. Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Yohana Sefue leo, Jumatatu, Februari 2, 2015, imesema kuwa uteuzi wa Dkt. Mwinyimvua ulianza Jumamosi, Januari 24, 2015. Dkt. Hamisi Hassan Mwinyimvua ni mwanataaluma mwenye ujuzi na uzoefu mkubwa katika uchumi. Anayo shahada ya kwanza ya B.A. (Econ) ya Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1986), Shahada ya Uzamili ya M.A. (Econ) ya Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1988) na Shahada ya Uzamivu ya PhD ya uchumi kutoka vyuo vikuu vya Dar es Salaam na Lund cha Sweden. Dkt. Mwinyimvua amekuwa mhadhiri wa miaka mingi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako amepanda daraja kutoka Tutorial Assistant, mwaka 1986-1988, Mhadhiri Msaidizi, mwaka 1988-1996, Mhadhiri, mwaka 1996-2005, Mhadhiri Mwandamizi, mwaka 2005-2006 na Mkuu wa Idara ya Uchumi ya chuo hicho mwaka 2006. Dkt. Mwinyimvua aliteuliwa kuwa Msaidizi wa Rais, Uchumi, mwaka 2006, nafasi ambayo ameishikilia hadi mwaka huu, 2015. Imetolewa na: Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, DAR ES SALAAM.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dkt. Hamisi Hassan Mwinyimvua(pichani) kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, anayesimamia Menejimenti ya Fedha za Umma (Public Finance Management).

Kabla ya uteuzi wake, Dkt. Mwinyimvua alikuwa Msaidizi wa Rais wa muda mrefu wa masuala ya uchumi.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Yohana Sefue leo, Jumatatu, Februari 2, 2015, imesema kuwa uteuzi wa Dkt. Mwinyimvua ulianza Jumamosi, Januari 24, 2015.

Dkt. Hamisi Hassan Mwinyimvua ni mwanataaluma mwenye ujuzi na uzoefu mkubwa katika uchumi.

Anayo shahada ya kwanza ya B.A. (Econ) ya Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1986), Shahada ya Uzamili ya M.A. (Econ) ya Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1988) na Shahada ya Uzamivu ya PhD ya uchumi kutoka vyuo vikuu vya Dar es Salaam na Lund cha Sweden.

Dkt. Mwinyimvua amekuwa mhadhiri wa miaka mingi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako amepanda daraja kutoka Tutorial Assistant, mwaka 1986-1988, Mhadhiri Msaidizi, mwaka 1988-1996, Mhadhiri, mwaka 1996-2005, Mhadhiri Mwandamizi, mwaka 2005-2006 na Mkuu wa Idara ya Uchumi ya chuo hicho mwaka 2006.

Dkt. Mwinyimvua aliteuliwa kuwa Msaidizi wa Rais, Uchumi, mwaka 2006, nafasi ambayo ameishikilia hadi mwaka huu, 2015.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s