Kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya jamii yatembelea mradi wa upanuzi wa masafa ya usikivu ya TBC-Kisarawe.


 

tib1

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akisalimiana na mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya huduma na maendeleo ya jamii Bw.Peter Serukamba katika viwanja vya urushaji wa matangazo ya shirika la utangazaji Tanzania (TBC) Kisarawe

tib2

Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma na maendeleo ya Jamii Bw.Peter Serukamba akieleza jambo wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kuangalia mradi wa upanuzi wa masafa ya usikivu ya shirika la utangazaji Tanzania iliyopo kisarawe Pwani.

tib3

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye (wa pili kulia) akiwasilisha jambo kwa wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma na Maendeleo ya jamii walipotembelea mradi wa upanuzi wa masafa ya usikivu ya shirika la utangazaji Tanzania iliyopo kisarawe Pwani.

tib4

Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma na maendeleo ya Jamii Bw.Peter Serukamba akieleza jambo wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kuangalia mradi wa upanuzi wa masafa ya usikivu ya shirika la utangazaji Tanzania iliyopo kisarawe Pwani.

tib5

Mkurugenzi wa shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw.Ayoub Ryoba akiwasilisha  taarifa ya shirika hilo  kwa wajumbe wa wa kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma na Maendeleo ya jamii kuhusiana na upanuzi wa masafa ya usikivu kisarawe Pwani.Wengine pichani ni Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye,Naibu Waziri wa wizara hiyo Bi.Anastazia Wambura na mwenyekiti wa kamati hiyo Bw.Peter Serukamba

Picha na Daudi Manongi-Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.Chanzo:fullshangweblog

Advertisements

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKUTANA NA NAIBU WAZIRI WA SHERIA NA KATIBA LEO


 

mpanjuMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Sheria na Katiba Ndugu Amon Mpanju wakati Naibu Mpanjo alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo March 31, 2016.(Picha na OMR)

Prof. Mbarawa afanya ziara kushtukiza KOJ Kurasini.


 

1Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiongea na baadhi ya wafanyakazi wa TPA eneo la kupakulia mafuta yanayoingia nchini (KOJ) Kurasini jana jiji Dar es salaam. Wa kwanza kulia Mhandisi anayefanya kazi eneo la KOJ Jabiri Muyones.

2Kapteni Abdulla Mwingamno (kulia) akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kushoto) baadhi ya vifaa vya kituo cha kupakulia mafuta yanayoingia nchini (KOJ) Kurasini jana jiji Dar es salaam.

3Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiongozana na Mhandisi anayefanya kazi eneo la KOJ Jabiri Muyones alipotembelea TPA eneo la kupakulia mafuta yanayoingia nchini (KOJ) Kurasini jana jiji Dar es salaam.

4Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akikagua baadhi vipuri eneo la kupakulia mafuta yanayoingia nchini (KOJ) Kurasini jana jiji Dar es salaam.

5Eneo la kupakulia mafuta yanayoingia nchini (KOJ) Kurasini jiji Dar es salaam.

(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)

…………………………………………………………………………….

Na Eleuteri Mangi-MAELEZO

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amemuagiza Kaimu Meneja Msaidizi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Nelson Mlali kufanya uhakiki wa kampuni zinazotoa huduma mbalimbali bandarini ili kuboresha utendaji kazi na kuepuka mgongano wa maslahi binafsi minongoni wa watumishi wa bandari.

Profesa Mbarawa alitoa kauli hiyo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza jana jioni(29/03/2016) kwenye ofisi za Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) eneo la kupakulia mafuta yanayoingia nchini (KOJ) Kurasini.

“Mtafanyaje kazi na mtu ambaye ni mfanyakazi na huku kampuni yake inatoa huduma bandarini, hamuoni kutakuwa na mgongano wa kimaslahi binafsi,” alihoji Profesa Mbarawa.

Aidha, Prof. Mbarawa amemtaka Kaimu Meneja Msaidizi Mlali azingatie umiliki wa makampuni kulingana na taarifa za Wakala wa Usajili wa Biashara na Kampuni nchini (BRELA) katika zoezi la kuhakiki kampuni hizo.

Akiwa eneo la (KOJ) Kurasini, Prof. Mbarawa amewataka wafanyakazi wa TPA  wabadilike na kufanya kazi kwa juhudi na maarifa badala ya kufanya kazi kwa mazoea ili kuboresha kuongeza ufanisi na kuliongezea taifa mapato kwa manufaa ya wananchi  

Prof. Mbarawa amewaagiza pia Mamlaka ya Bandari wanaponunua vipuri na vifaa mbalimbali vinavyohitajika bandarini hapo wazingatie vipimo sahihi kulingana na vifaa vinavyohitajika kuendeshea mitambo mbalimbali ili kulipunguzia taifa gharama zisizohitajika.

Mamlaka ya Bandari nchini ina bandari mbalimbali zilizopo katika ukanda wa bahari ya Hindi na maziwa yaliyopo nchini.

Ukanda wa Bahari ya Hindi una bandari ya kuu za Dar es salaam, Tanga na Mtwara pamoja na Bandari ndogo zilizopo Lindi, Kilwa Masoko, Mafia, Bagamoyo, Pangani na Kwale.

Bandari nyingine ziliozo katika maziwa mbalimbali nchini ni pamoja na Ziwa Victoria lenye bandari ya Mwanza, Bukoba, Kemondo, Musoma na Nansio, Ziwa Tanganyika likihusisha bandari ya Kigoma na Kasanga wakati Ziwa Nyasa kuna bandari ya  Itungi, Manda, Liuli na Mbaba Bay.Chanzo:fullshangweblog

Changamkia nafasi hizi za kazi


kazi

 

 
kazi
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINISTRY OF HEALTH, COMMUNITY DEVELOPMENT, GENDER, ELDERLY AND CHILDREN
PRIVATE HEALTH LABORATORIES BOARD
EMPLOYMENT OPPORTUNITIES
Private Health Laboratories Board (PHLB), is the Government Institution under the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children which registers and manages all Private Health Laboratories in Tanzania (Mainland), Vacancies exist at the Board`s Head Office in Dar es Salaam and applications from suitably qualified and competent persons are invited to fill the following posts:-
1. Laboratory Quality Assurance Officer (1 post)
Duties and Responsibilities
• To implement activities involved in Laboratory Quality Assurance Framework, Laboratory Standard Guidelines, training curriculum and modules so that they meet International standards requirements.
• To monitor quality of health Laboratory Services in supporting the provison of essential intervention health packages in the private laboratories.
• To work towards Accrediting health laboratory through intenetionally recognized accrediting board.
• To document all laboratory quality activities including submission of reports to relevant authority.
• To liaise with national laboratory quakutt ststens coordinator on all matters conceming private health laboratories quality systems.
• To monitor all EQA results and provide feedback on the effectiveness and performance of private health laboratories nationwide.
• To perform competence assessment to laboratory staff.
• To perform any other relevant duties as may be assigned from time to time by Registrar.
Qualifications and Experience
• Medical laboratory technologist or medical laboratory scientist from recognised institutions and registered by health laboratory practitioners council.
• Working experience of three years implementing quality management system (QMS) the quality assurance officer will report direct to the Registar-Private Health Laboratory Board.
===========
2. Medical Health Laboratory Authorized Inspector (1 post)
Responsibilities
• To monitor all private health laboratories in Tanzania Mainland.
• To inspect health laboratories, health Laboratory products and supplies countrywide.
• To prosecute offenders by taking in implementing the Act 10 of 1997 and laboratory regulations at national.
• To coordinato preparation of samples for quality assessment, analyze results and disseminate the report.
• To perform any other duties assigned by the registrar from time to time.
Qualifications and Experience
• Medical Laboratory Technologist or Medical Laboratory scientist registered by health laboratory practitioners council
• Working experience of three years.
As a medical laboratory authorized inspector she/he will report to the Registrar – Private Health Laboratories Board.
How to Apply
Interested and qualified individuals should submit their applications enclosing detailed CV`s two passport-size photographs, photocopies of academic and professional certificates. Names and addresses of three referees to the address under mentioned not later than 8th April, 2016. For all posts mentioned above, the employment condition is for two years contract subject to be renewable.
Private Health Laboratories Board is an equal opportunity employer.
Registrar
Private Health Laboratories Board
P.O.BOX 9073
DAR ES SALAAM – TANZANIA
Source: 29th March, 2016

KAMATI YA BUNGE YAIOMBA SERIKALI KUTOA VIBALI VYA UINGIZAJI SUKARI KUTOKA NJE YA NCHI


 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Maji, Dk. Mary Nagu (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu Serikali kutoa mapema vibali vya uingizwaji wa sukari kutoka nje ya nchi ili kuweza kuziba upungufu ya bidhaa hiyo nchini. Kulia ni Mjumbe wa Kamati hiyo, Mahmoud Mgimwa.
 Mjumbe wa Kamati hiyo, Mahmoud Mgimwa akizungumza katika mkutano huo.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Maji, Dk. Mary Nagu (katikati), akiwa na wajumbe wa kamati hiyo.
 Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Mwanahabari kutoka TBC, Angela Msangi (kulia), akiuliza suala katika mkutano huo.
……………………………………………………………………………………………….
Na Dotto Mwaibale
 
KAMATI ya Bunge ya Kudumu ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Maji, imeitaka Serikali kutoa mapema vibali vya uingizwaji wa sukari kutoka nje ya nchi ili kuweza kuziba upungufu ya bidhaa hiyo nchini.
 
Pia imeitaka Serikali kudhibiti bandari bubu na njia za panya ambazo huingiza sukari kinyume cha sheria na kuua viwanda vilivyopo na kuifanya Tanzania kununua sukari kutoka nje ya nchi na kuua uchumi.
 
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dk.Mary Nagu alisema kwa sasa upatikanaji wa sukari ni mdogo ukilinganisha na mahitaji ambapo kunamapungufu wa tani 80,000 hadi 100,000.
 
Alisema mapungufu hayo yanatokana na viwanda vinavyozalisha sukari nchini kuzalisha tani 302,0000 huku mahitaji ya sukari kwa nchi nzima ni tani 402,0000.
 
Alisema kwa sasa kuna viwanda vitano tu ambavyo huzalisha sukari ambayo haitoshi kwa matumizi ya wananchi nchini hapa na kusababisha mapungufu hayo.
 
Hata hivyo alisema pamoja na viwanda hivyo kuzalisha chini ya kiwango kinacho hitajika katika kipindi hiki cha mwezi Machi hadi Juni viwanda hivyo hufungwa kwaajili ya kupisha ukarabati hivyo kwa kipindi hicho sukari inayotumika ni ile ambayo ilizalishwa katika kipindi kilicho pita.
 
Alisema kutokana na hali hiyo ni vema Serikali ikahakikisha inaagiza sukari hiyo mapema ili kuweza kuziba pengo la mapungufu ya sukari katika kipindi muafaka ili isiweze kugongana na sukari iliyopo na kusababisha kuua uzalishaji nchini.
 
“Hivyo kutokana na mapungufu hayo ili kufidia mapungufu hayo kati ya utumiaji na uzalishaji sukari inaagizwa kutoka nje, hivyo ikiagizwa tani 80,000 hadi 100,000 kuna kuwa hakuna mapungufu.
 
“Baada ya kupata taarifa ya mapungufu hayo kutoka katika bodi ya sukari tukaona humuhimu wa kumuomba Rais, kutoruhusu mapungufu ya sukari yatokee katika kipindi hichi ambacho viwanda vya sukari vinafungwa na kusimamisha uzalishaji kuanzia mwezi Machi hadi Juni kwa kuagiza mapema,” alisema.
 
Hata hivyo alisema kuwa pamoja na mapungufu hayo lakini pia kumekuwa na wafanyabiashara wabinafsi wamekuwa wakitumia vibaya mapungufu hayo kwa kuingiza sukari zaidi ya kiwango kinacho hitajika bila kujali uchumi wa nchi unavyodidimia.
 
“Katika wafanyabiashara hao wapo ambao wanaingiza sukari kwaajili ya kupeleka katika nchi nyingine lakini sukari hiyo inabaki humuhumu bila kuuza na baadae kuuza kwa bei kubwa hivyo kuua uchumi wa nchi,” alisema.
 
Alisema ni vema Serikali kuhakikisha hairuhusu mapungufu ya sukari kwani mapungufu hayo kwa kuingiza sukari hiyo kwa wakati kwani usheleweshwaji unaweza kusababisha kuuzwa kwa bei ya juu na hivyo kuua uchumi, pamoja na kuifanya nchi ya kununua sukari kutoka nje.
 
Aidha Kamati hiyo iliitaka Serikali kufunga bandari bubu na kudhibiti njia za panya za uingizaji wa sukari, kutobakiza sukari zinazotakiwa kuuzwa nje ya nchi kubaki nchini na kuwekwa mahali ambapo hapajulikani na baadae kuuzwa kwa bei ya juu kunapokuwa na mapungufu ya sukari.
 
“Sisi kama kamati tunaendelea kumshukuru rais na tutaendelea kuisaidia Serikali kusisitiza uzalishaji wa sukari ya kutosha na ziada ya kupata sukari kutoka nje uwezekano upo.
 
“Hivyo tumeapa katika kumsaidia rais katika kuhakikisha sukari inazalishwa ya kutosha na inakuwa na tija, viwanda vinafanya kazi, na nahakika siku moja Tanzania itakuwa nchi ya kuuza sukari nje na badala ya kununua,” alisema.
 
Pamoja na hilo lakini pia ni vema ikahakikisha Tanzania isiwe eneo la kuuza sukari za nchi nyingine na kuua uchumi uliopo na kukuza wa nchi hizo.
 
Alisema pia Serikali inawajibu wa kufuatilia utaratibu za uingizaji wa sukari kwani kamati hiyo imegundua tatizo hilo lisipotatuliwa bei ya sukari haiwezi kudhibitiwa kutokana na hali ya kisoko.
 
Alisisitiza kuwa pia ni vema wazalishaji kutumia muda mwingi wa kuweka mikakati ya kuongeza uzalishaji na kununua miwa kutoka kwa wakulima.
 
Hivyo alisema kama kamati imeona umuhimu wa kuwawezesha wakulima kulima ili viwanda vinapopanua uzalishaji kupata malighafi za kutosha.
 

Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo imepanga kufanya mikutano ya kusikiliza maoni ya wadau


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

BUNGE LA TANZANIA

indexTAARIFA KWA UMMA

Katika kutekeleza majukumu yake, Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo imepanga kufanya mikutano ya kusikiliza maoni ya wadau (Public Hearing) kwa mujibu wa Kanuni ya 117 (9) kuhusiana na Sheria Ndogo zilizowasilishwa na Serikali katika Mkutano wa Pili wa Bunge uliomalizika Februari 2016.

Mikutano hiyo ya kusikiliza maoni ya wadau kuhusu Sheria Ndogo inatarajiwa kufanyika Jumatatu tarehe 4 Aprili, 2016 na Jumanne tarehe 5 Aprili, 2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam. Sheria Ndogo ambazo Kamati inakaribisha wadau na umma kwa ujumla kutoa maoni yao ni pamoja na zifuatazo:-

  1. The Petroleum (Bulk Procurement) Regulations, 2015
  1. The Public Private Partnership Regulations, 2015
  1. The Copyright and Neighboring Rights (Copyrighted Works – Communication to the Public) Regulations, 2015
  1. The National Examinations Regulations, 2015
  1. The Institute of Judicial Administration Lushoto (Students’ General Welfare, Conduct and Disciplinary Matters) Regulations, 2015
  1. The Institute of Judicial Administration Lushoto (Students’ Performance Assessment) Regulations, 2015
  1. The Fire and Rescue Force (Fire Precautions in Buildings) Regulations, 2015

Sheria Ndogo zilizotajwa hapo juu pamoja na nyingine ambazo zinashughulikiwa na Kamati, zinapatikana kwa kupakua (downloadable) katika tovuti ya Bunge la Tanzania ya http://www.parliament.go.tz pamoja na tovuti ya Serikali ya http://www.tanzania.go.tz

Aidha, maoni ya wadau yanaweza kuwasilishwa kwa njia ya posta au barua pepe kwa anuani ifuatayo:-

Katibu wa Bunge, Ofisi ya Bunge,

  1. L. P. 9133, DAR ES SALAAM

Barua pepe: cna@bunge.go.tz

Imetolewa na:

Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano Ofisi ya Bunge

DAR ES SALAAM

29 Machi, 2016.

RAIS MAGUFULI APATA CHAKULA CHA MCHANA MGAHAWANI UWANJA WA NDEGE WA MWANZA AKIWA NJIANI KUELEKEA CHATO


 

MWZ1

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Joseph Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na viongozi wa mkoa wa Mwanza wakijipatia chakula cha mchana katika mgahawa wa Victoria uliopo nye ya Uwanja wa Ndege wa Mwanza alipopumzika kwa muda kabla ya kuelekea nyumbani kwake Chato mkoani Geita kwa mapumziko mafupi. Pamoja nao mezani hapo ni Meya wa Ilemela Mstahiki Renatus Mulunga, Meya wa jiji la Mwanza Mstahiki James Bwire, Mkuu wa Mkoa wa MWanza  Mhe John Mongella na Mwenyekiti wa CCM Mkoa huo Ndg Anthony Diallo.PICHA NA IKULU

MWZ2

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Joseph Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na viongozi wa mkoa wa Mwanza wakijipatia chakula cha mchana katika mgahawa wa Victoria uliopo nye ya Uwanja wa Ndege wa Mwanza alipopumzika kwa muda kabla ya kuelekea nyumbani kwake Chato mkoani Geita kwa mapumziko mafupi. Pamoja nao mezani hapo ni Meya wa Ilemela Mstahiki Renatus Mulunga, Meya wa jiji la Mwanza Mstahiki James Bwire, Mkuu wa Mkoa wa MWanza  Mhe John Mongella na Mwenyekiti wa CCM Mkoa huo Ndg Anthony Diallo.

MWZ3 MWZ4

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Joseph Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na viongozi wa mkoa wa Mwanza wakiondoka baada ya kupata  chakula cha mchana katika mgahawa wa Victoria uliopo nye ya Uwanja wa Ndege wa Mwanza alipopumzika kwa muda kabla ya kuelekea nyumbani kwake Chato mkoani Geita kwa mapumziko mafupi.