UN YARIDHIA HATUA ZA KUKABILIANA NA UDHALILISHAJI WA KINGONO

Zentralafrikanische Republik Blauhelmsoldat

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limedhinisha azimio lake la kwanza kabisaa siku ya Ijumaa, kukabaliana na tatizo linaloongezeka na udhalilishaji wa kingono na wanajeshi wa kulinda amani katika maeneo ya migogoro.

Umoja wa Mataifa umemulikwa kwa miezi kadhaa kuhusiana na madai ya kuwabaka watoto na na ukiukaji mwingine wa kingono unaofanywa na wanajeshi wake w akulinda amani, hasa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati na DRC. Umoja wa Mataifa unasema kulikuwa na madai 69 ya udhalilishaji wa kingono na dhuluma nyingine dhidi ya walinda amani mwaka 2015, na visa vingine 25 zaidi kwa mwaka huu wa 2016.

Azimio hilo liliidhinishwa kwa kura 14 kwa 0, huku Misri ikijizuwia baada ya kushindwa kwa marekebisho ya dakika za mwisho iliyoyapendekeza, ambayo yangedhoofisha maandishi ya muswada wake. Muswada huo ulioandaliwa na Marekani unaidhinisha mpango wa mageuzi wa Katibu Mkuu Ban Ki-Moon, ikiwemo uamuzi wa kuvirejesha vikosi vya kijeshi au polisi, “pale inapobainika kuna ushahidi wa ukiukaji mkubwa na udhalilishaji wa kingono.”

Pia linamtaka Katibu Mkuu Ban kubadili vikosi pale ambapo madai hayajachunguzwa vizuri, wakosaji hawajawajibishwa ipasavyo, au iwapo katibu mkuu hajafahamishwa kuhusu maendeleo ya uchunguzi. Marekebisho yaliokuwa yamependekezwa na Misri, yangetaka masharti yote matatu yatimizwe kabla ya kikosi cha jeshi au polisi kurejeshwa nyumbani, na siyo moja wapo kama inavyotakiwa sasa.

Ujumbe mzito kwa mataifa husika

Marekani, ambayo ndiyo mchangiaji mkubwa zaidi wa kifedha kwa operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa, ilisema ilitaka chombo hicho chenye nguvu zaidi cha Umoja wa Mataifa kutuma ujumbe mzito kwamba hakitavumilia tatizo hilo linalozidi kukuwa.

“Kwa waathirika wa dhuluma za kingono na ukiukaji unaofanywa na walinda amani, tunaahidi kwamba tutafanya zaidi,” alisema Samantha Power, balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa. “Tutafanya kazi nzuri zaidi kuhakikisha kwamba wanajeshi wa kulinda amani tunaowatuma kama walinzi wenu hawageuki kuwa wahalifu.”(P.T)

Read more…

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s