SAI alia na BABY wake

 

Ulimwengu wa muziki wa kizazi kipya nchini umeongeza memba mpya baada ya kijana Simon Robert, 22, kuipua ngoma yake iitwato ‘BABY’ inayofanya vema kwenye vituo vya runinga nchini.
Akifahamika zaidi kwa jina la Sai, msanii huyu amesema kuwa, ametengeneza wimbo wake huo katika studio za C9 Records ya jijini Dar es Salaam kwa mtayarishaji C9 na kwamba, ameamua kutoa video kwanza kabla ya audio.
“Nashukuru Mungu. Nimepiga kazi moja ya ‘Baby’ ambayo nimeanza kutoa video niliyopiga na Skillz Videos – kwa Pizzo Mtena ambayo nimeisambaza kwenye vituo vya runinga na mitandao mbalimbali ya YouTube, tovuti na blogu kadhaa,” akasema Sai.
Wimbo wake huo aliouachia Machi 8 mwaka huu, umetengezwa katika mahadhi ya Pop-Mduara na maudhui yake ni masuala ya mapenzi ambayo yanagusia mkasa wa wapenzi wanaishi kwa kuzinguana.
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s