Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo imepanga kufanya mikutano ya kusikiliza maoni ya wadau

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

BUNGE LA TANZANIA

indexTAARIFA KWA UMMA

Katika kutekeleza majukumu yake, Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo imepanga kufanya mikutano ya kusikiliza maoni ya wadau (Public Hearing) kwa mujibu wa Kanuni ya 117 (9) kuhusiana na Sheria Ndogo zilizowasilishwa na Serikali katika Mkutano wa Pili wa Bunge uliomalizika Februari 2016.

Mikutano hiyo ya kusikiliza maoni ya wadau kuhusu Sheria Ndogo inatarajiwa kufanyika Jumatatu tarehe 4 Aprili, 2016 na Jumanne tarehe 5 Aprili, 2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam. Sheria Ndogo ambazo Kamati inakaribisha wadau na umma kwa ujumla kutoa maoni yao ni pamoja na zifuatazo:-

  1. The Petroleum (Bulk Procurement) Regulations, 2015
  1. The Public Private Partnership Regulations, 2015
  1. The Copyright and Neighboring Rights (Copyrighted Works – Communication to the Public) Regulations, 2015
  1. The National Examinations Regulations, 2015
  1. The Institute of Judicial Administration Lushoto (Students’ General Welfare, Conduct and Disciplinary Matters) Regulations, 2015
  1. The Institute of Judicial Administration Lushoto (Students’ Performance Assessment) Regulations, 2015
  1. The Fire and Rescue Force (Fire Precautions in Buildings) Regulations, 2015

Sheria Ndogo zilizotajwa hapo juu pamoja na nyingine ambazo zinashughulikiwa na Kamati, zinapatikana kwa kupakua (downloadable) katika tovuti ya Bunge la Tanzania ya http://www.parliament.go.tz pamoja na tovuti ya Serikali ya http://www.tanzania.go.tz

Aidha, maoni ya wadau yanaweza kuwasilishwa kwa njia ya posta au barua pepe kwa anuani ifuatayo:-

Katibu wa Bunge, Ofisi ya Bunge,

  1. L. P. 9133, DAR ES SALAAM

Barua pepe: cna@bunge.go.tz

Imetolewa na:

Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano Ofisi ya Bunge

DAR ES SALAAM

29 Machi, 2016.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s