Makonda akazia ufungwaji wa kumbi za burudani


Makonda (11)

 

 

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, leo alizungumza na wamiliki wa kumbi za starehe, bendi na wadau wa burudani ambapo mada kubwa iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu ni utekelezaji wa amri ya kufunga kumbi za starehe saa sita usiku.

Akiichambua hoja hiyo kwenye mkutano uliofanyika Ukumbi wa Vijana Kinondoni, Makonda alisema hawezi kubadilisha agizo hilo kwa kuwa yeye anatimiza wajibu wake kwa kusimamia sheria na atakayekiuka atakiona.

“Siwezi kutengua sheria hiyo mpaka itakapofanyiwa marekebisho bungeni, kwani kufanya hivyo naweza kuonekana natumia vibaya madaraka yangu au pengine nimepewa kitu fulani ili kunishawishi kuwaruhusu kuvunja sheria.
Kumbi zinazotakiwa kutumika muda wowote ni zile zenye vibali maalum vya Night Club” alisema Makonda.

Makonda alisema hayo na hakutaka kupokea swali lolote katika kikao hicho lakini aliwasisitiza wajumbe wa kikao hicho kujadiliana mapendekezo yao na kumpelekea ili nae ayapeleke kwa wahusika ili yakionekana kufaa yakajadiliwe bungeni na kubadili sheria hiyo.

PICHA NA RICHARD BUKOS / GPL

Advertisements

BUNGENI: Serikali imeagiza sukari kutoka nje sababu ya uhaba


  1. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema bungeni leo wakati akifanya majumuisho ya bajeti yake kuwa, Serikali imeagiza sukari nje ya nchi kuukabili uhaba wa bidhaa hiyo.

    Amewaagiza maofisa biashara wa wilaya, mikoa na Taifa kukagua maghala yote ya wafanyabiashara walioficha sukari na kuwachukulia hatua.

    Waziri Majaliwa alisema hayo leo asubuhi wakati akihitimisha mjadala wa hotuba ya mapato na matumizi ya ofisi yake na kuliomba Bunge likubali kupitisha.

    Waziri Mkuu alisema ni kweli kwamba kuna upungufu wa sukari nchini, ingawa pia upo udanganyifu kwa baadhi ya wafanyabiashara.

MARIA NYERERE ATEMBELEA DARAJA LA KIGAMBONI


Mama Nyerere (1)

Mama Maria Nyerere, Mjane wa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, akiwa na mwanae Mhe. Makongoro Nyerere na msaidizi wake akifurahia mandhari wakati walipotembelea Daraja la Nyerere Kigamboni jijini Dar es salaam jana.

Mama Nyerere (2)

 

Mama Maria, ambae hakujali mvua kubwa iliyokuwa inanyesha, alionekana mwenye furaha kufika darajani hapo kwani ndoto ya miaka mingi iliyoanzishwa na hayati mumewe imetimia. Pia alimshukuru sana Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwa kuagiza daraja lipewe jina la Mwalimu na siyo yeye, jambo ambalo amesema limemfariji sana kwani vizazi vya sasa na vijavyo vitamkumbuka mwasisi wa Taifa.Chanzo:Mjengwablog

Mama Nyerere (3)

 

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA NCHINI AFUNGA RASMI MAFUNZO YA MAAFISA WATEULE DARAJA LA KWANZA , MKOANI MOROGORO


1Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja akikagua Gadi Maalum iliyoandaliwa na Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza yalifanyika Aprili 27, 2016 katika Viwanja vya chuo cha Jeshi la Magereza, KPF Mkoani Morogoro.

2Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja katika jukwaa akipokea salaam ya heshima kutoka Gadi Maalum iliyoandaliwa na Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza(hawapo pichani).

3Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza wakipita mbele ya Mgeni rasmi katika sherehe za kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika Viwanja vya chuo cha Jeshi la Magereza, KPF Mkoani Morogoro.

4Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja(kushoto) akimvisha cheo cha RSM mmoja wa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza ambaye amefanya vizuri zaidi katika Mafunzo hayo yaliyofanyika kwa muda wa miezi miwili.

5Baadhi ya Maofisa wa Kike wa Jeshi la Magereza ambao ni miongoni mwa wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza kama wanavyoonekana katika picha.

6Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja akitoa hotuba fupi kwa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza(hawapo pichani).

7Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni kama wanavyoonekana katika picha.

8Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja akifanya mahojiano na baadhi ya Wawakilishi wa Vyombo vya Habari, Mkoani Morogoro.

9Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza waliosimama mstari wa nyuma.

(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

MHE.NAPE APANIA KUIBORESHA TASNIA YA HABARI


indexWaziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akikabidhi Ipad tano kwa mkuu wa wilaya ya Bukoba Bw.Jackson Msome kwa ajili ya matumizi ya maafisa habari wa mkoa wa Kagera. Bwana Msome alikuwa akimwakilisha Mkuu wa mkoa wa Kagera, Meja Jenerali mstaafu Salum Mustafa kijuu.……………………………………………………………………………………………………

Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
 
Sekta ya habari ni kiungo muhimu cha mawasiliano kati ya wananchi na serikali yao. Ndiyo maana wanazuoni hupenda kusema kuwa habari ni muhimili wa nne wa dola. Kwa kuzingatia umuhimu huo, katika kuchekecha huku na huko, Mhe. Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akamteua mtu mahiri kuongoza sekta hii, Mhe. Nape Moses Nnauye.
 
Kwa uteuzi huu ninadiriki kusema hatimaye Wizara imepata mtu sahihi na mchapakazi anayeweza kwenda na kasi ya Mheshimiwa Rais Magufuli na ni dhahiri kabisa kuwa kumpa Mhe. Nape ni kuthibitisha usemi wa wahenga usemao upele umepata mkunaji.
 
Kwa jinsi hii tuna kila sababu ya kumshukuru Mwenyezi Mungu, Muumba wa Mbingu na Nchi kwa kutujalia kupata kiongozi wa nchi ambaye ni mchapakazi na aliyejaliwa kipawa cha kuona mbali kwa kuwaweka viongozi wa chini yake katika nafasi za uongozi wanazostahili.
 
Sekta ya habari ni sekta nyeti na muhimu sana katika dunia hii kwa kua bila kupashana habari na kujua kinachoendelea daima hakutakua na maendeleo kwa hiyo, ni sekta inayohitaji kuangaliwa kwa jicho la tatu ili kuhakikisha kwamba inachukuliwa uzito na inapewa kipaumbele kwa kupewa vifaa na elimu ya kutosha ili kuepusha upotoshaji na kukosekana kwa habari muhimu hasa za Serikali zinazotakiwa kuwafikia wananchi kwa muda husika.
 
Tukiangalia katika sekta ya habari, Mhe.Rais hakukosea kabisa kumuweka Waziri Mhe. Nape kwa kuwa ameanza kuitumikia Wizara kwa kasi nzuri na ameonyesha nia ya kuiboresha Wizara hasa kwa tasnia ya habari kwa kuanzia kwenye wizara yake hadi katika ofisi za umma zilizoko mikoani ili kuhakikisha wanahabari wote nchini wanatambua thamani ya kazi yao.
 
Kwa maneno yake aliyoyatoa Jijini Mbeya alipokua akigawa vitendea kazi vya kisasa kwa ajili ya mawasiliano yaani ipad kwa maafisa mawasiliano wa mkoa huo alikaririwa akisema,”Nataka Wizara ihamie mikoani” hii haimaanishi kuwa Wizara ihamie mikoani kama alivyosema bali alimaanisha kiutendaji zaidi kuwa yale yote anayoyafanya katika Wizara yake atahakikisha na maafisa wa mikoani pia wanafanyiwa hivyo ikiwemo kugawiwa vitendea kazi pamoja na mambo mengine.
 
Katika kuhakikisha hilo, kwa upande wa sekta ya habari, Waziri Nape ameanza kwa kugawa ipad  kwa maafisa mawasiliano walioko mikoa ya pembezoni ambao wana upungufu mkubwa wa vitendea kazi na kwa muda mrefu wameshindwa kuifanya kazi yao kwa ufanisi kwa sababu ya uhaba wa vifaa vya kufanyia kazi hiyo.

Continue reading →

SPIKA WABUNGE ALIPOKUTANA NA BALOZI WA KOREA NA BALOZI WA KENYA


U2Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akisalimiana na Balozi wa Korea Kusini nchini Song Geum aliyemtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma.

U3Balozi wa Korea Kusini nchini Song Geum akimuonesha jambo Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai wakati alipomtembelea  Ofisini kwake Mjini Dodoma.

U4Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akisikiliza kwa makini Balozi wa Korea Kusini nchini Song Geum aliyemtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma. Kulia ni Mke wa Balozi huyo.

U5Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akisalimiana na Balozi wa Kenya nchini  Chirau Ali aliyemtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma.

U6Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akimsikiliza kwa makini Balozi wa Kenya nchini  Chirau Ali aliyemtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma.

U1Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (mwenye tai nyekundu katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi wa shule ya msingi Feza iliyopo Dar es Salaaam. Wanafunzi hao walikuja kutembelea Bunge.

(Picha na Ofisi ya Bunge)

WAZIRI MKUU: TATIZO LA AJIRA KWA VIJANA LAPUNGUA


G2Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasilisha  bungeni   Mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi  ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka 2016/2017.

G3Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenhye Ulemavu, Jenista Mhagama (kushoto) na Naibu wake, Dktt.  Abdallah Posi wakiteta bungeni mjini Dodoma Aprili 22, 2016.

G1Watendaji wakuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zake wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowasilisha bungeni  Mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi  ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka 2016/2017.

G4Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Kilimo na Maendeleo ya Mifugo, Mwigulu Nchemba, Bungeni Mjini Dodoma Aprili 20, 2016.

G5 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Fedha  ambao Aprili 22, 2016  walikwenda Bungeni mjini Dodoma kwa ziara ya mafunzo.

G6Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na Afisa Habari wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Hamis Dambaya (katikati) na  Mhadhiri Msaidizi  wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam , Egbert Mkoko kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Aprili 22, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

……………………………………………………………………………….

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kiwango cha ukosefu wa ajira kwa vijana nchini kimepungua kwa asilimia 2.5 na kwamba Serikali itaendeleza juhudi za kuvutia uwekezaji ili kupunguza zaidi kiwango hicho.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Ijumaa, Aprili 22, 2016) wakati akiwasilisha mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma.

“Utafiti wa hali ya ajira nchini wa mwaka 2014 umeonesha kuwa kiwango cha ukosefu wa ajira kimepungua kutoka asilimia 11.7 mwaka 2006 hadi asilimia 10.3 mwaka 2014. Aidha, ukosefu wa ajira  kwa vijana umepungua kutoka asilimia 14.2 mwaka 2006 hadi asilimia 11.7 mwaka 2014,” amesema. 

Waziri Mkuu amesema moja ya changamoto zinazosababisha ukosefu wa ajira ni vijana kutojengewa maarifa na ujuzi wa kuajiriwa na kuajirika. Hivyo, Serikali itaendelea kutekeleza Programu ya Miaka Mitano ya Kukuza Ujuzi Nchini (2015/2016 – 2019/2020).

“Programu hiyo inalenga kuongeza idadi ya watu wenye kiwango cha juu cha ujuzi kutoka asilimia tatu ya sasa hadi asilimia 12 inayotakiwa kuendesha uchumi wa viwanda. Vilevile, kupunguza idadi ya watu wenye kiwango cha ujuzi wa chini kutoka asilimia 75 ya sasa hadi asilimia 54,” amesema.

Amewaagiza watendaji wakuu wa wizara, idara zinazojitegemea, wakala za serikali, taasisi za umma, mikoa na mamlaka za serikali za mitaa kuhakikisha kuwa ukuzaji wa ajira  unakuwa ni agenda ya msingi ya kudumu katika utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo.

Akizungumzia kuhusu vitendo vya ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu hususan watu wenye ualbino, Waziri Mkuu amesema Serikali inafanya jitihada kubwa kukomesha vitendo hivyo ikiwa ni pamoja na kuwakamata wote wanaojihusisha na vitendo hivyo na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.

“Ukatili huo umesababisha watu wenye ualbino kupoteza maisha na wengine kupata ulemavu wa kudumu. Hali hiyo haikubaliki na haivumiliki katika jamii ya Watanzania. Napenda kusisitiza watu wenye ulemavu wana haki ya kuthaminiwa utu wao na kulindwa dhidi ya ukatili na aina yoyote ya ubaguzi,” amesema.

Waziri Mkuu amesema katika mwaka ujao wa fedha, Serikali itaviboresha Vyuo vya Ufundi na Marekebisho (Vocational and Rehabilitation Training Centres) vya watu wenye ulemavu nchini ili kutoa ujuzi unaoendana na mahitaji yao katika soko la ajira ikiwa ni pamoja na kuandaa walimu wa elimu maalum na kutoa vifaa saidizi kwa walimu na wanafunzi wenye ulemavu mashuleni.

Akitoa maelezo kuhusu juhudi za Serikali kuwawezesha wananchi kiuchumi, Waziri Mkuu amesema Serikali imesaidia uanzishwaji wa taasisi mwavuli ya kusimamia VICOBA inayoitwa VICOBA FETA ambayo imeanza kuonyesha matunda mazuri.

“Takwimu zilizotolewa mwezi Februari 2016 na taasisi hiyo zinaonesha kuwa kuna vikundi 100,000 vya VICOBA vyenye wanachama milioni 2.2 na mtaji wa shilingi trilioni 1.2. Ni jambo la kujivunia kwamba asilimia 79 ya wanachama wa VICOBA ni wanawake,” amesema.

Amezitaka Halmashauri zote nchini ziweke orodha sahihi ya vyama vya ushirika wa kuweka na kukopa vilivyosajiliwa kwa kila kijiji na kuchukua hatua za kuwezesha uanzishaji na usajili wa SACCOs zinazokidhi vigezo kulingana na shughuli za uzalishaji katika Halmashauri husika.

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

  1. L. P. 980,

DODOMA.

IJUMAA, APRILI 22, 2016.