BUNGE KUJADILI HOJA YA KUMN’GOA ZUMA JUMANNE

Bunge kujadili hoja ya kumn’goa Zuma Jumanne

Bunge la Afrika kusini litajadili hoja ya kumng’oa rais Jacob Zuma madarakani siku ya Jumanne.

Spika wa bunge la Afrika Kusini ametoa taarifa hiyo baada ya shinikizo kutoka kwa vyama vya upinzani vikiongozwa na kile cha Economic Freedom Fighters (EFF) kinachoongozwa na Julius Malema.

Spika Baleka Mbete, amesema wakati umewadia wa kujadili wito wa kumfuta kazi rais Zuma kufuatia tuhuma za ufisadi ubadhirifu wa mali ya umma na matumizi mabaya ya madaraka yake.

Spika Baleka Mbete, amesema wakati umewadia wa kujadili wito wa kumfuta kazi rais Zuma

Vyama vya upinzani vilikuwa vimemtaka ajiuzulu baada ya kupatikana na hatia ya kutumia madaraka yake vibaya kwa kuidhinisha ukarabati wa makazi yake licha ya kushauriwa asifanye hivyo.

Siku ya Alhamisi, mahakama kuu ya nchi, ilisema kuwa rais amekwenda kinyume na katiba, katika kashfa ya mamilioni ya dola, yaliyotumiwa kukarabati nyumba yake ya binafsi.

Upinzani uliwasilisha kesi mahakamani baada ya bwana Zuma kupuuza uamuzi wa mwaka 2014 kuwa alinufaika kutokana na ukarabati wa nyumba yake na kwamba alistahili kulipa pesa zilizotumiwa.

Economic Freedom Fighters (EFF) kinachoongozwa na Julius Malema kimekuwa kikimshinikiza ajiuzulu

Mahakama ilisema wizara ya fedha itatambua ni kiasi gani cha pesa kilichotumiwa na kwamba Zuma atatakikana kuzirejesha.

Rais Jacob Zuma alikubali uamuzi wa mahakama ya kikatiba uliompata na hatia na akaapa kulipia ukarabati uliofanyiwa makao hayo ya Nkandla kama ilivyoamua mahakama.BBC

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s