RAIS WA ZANZIBAR AWASILI VISIWA VYA COMORO.


da1Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Gavana wa Comoro Bw.Hassan Hamadi wakati alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Comoro jana akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli,katika sherehe za kuapishwa Rais mteule wa Muungano wa Comoro Kanali Azali  Assoumani,akiwa  na ujumbe aliofuatana nao akiwemo Mama Mwanamwema Shein,[Picha na Ikulu].25/05/2016.]

da2Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Comoro Mhe,Chabaka Chilumanga Fereji wakati alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Comoro jana akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli,katika  sherehe za kuapishwa Rais mteule wa Muungano wa Comoro Kanali Azali  Assoumani, akiwa  na ujumbe aliofuatana nao akiwemo Mama Mwanamwema  Shein,[Picha na Ikulu].25/05/2016.]

da3Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein (katikatki) akifuatana na Gavana wa Comoro Bw.Hassan Hamadi (kulia) wakati alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Comoro jana akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli,katika  sherehe za kuapishwa Rais mteule wa Muungano wa Comoro Kanali Azali  Assoumani,  akiwa na ujumbe aliofuatana nao akiwemo Mama Mwanamwema Shein,(kushoto) Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Visiwa vya Comoro Dr.Ahamada El Badaoui Mohamed [Picha na Ikulu].25/05/2016.]

da4Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi mbali mbali wa Muungano wa Comoro wakati  alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Comoro jana akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli,katika sherehe za kuapishwa Rais mteule wa Muungano wa Comoro Kanali Azali  Assoumani, akiwa na ujumbe aliofuatana nao akiwemo Mama Mwanamwema Shein,[Picha na Ikulu].25/05/2016.]

Advertisements

MAJALIWA:VITA DHIDI YA RUSHWA SI NGUVU YA SODA


an1 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema vita inayoendeshwa na Serikali ya awamu ya tano dhidi ya wala rushwa na wale wanaofanya ufisadi siyo nguvu ya soda kama wengi wanavyofikiri.

“Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kupambana na wala rushwa na mafisadi. Wala hatutanii. Hawa tutacheza nao na wala wasidhani vita hii ni nguvu ya soda. Tutaendelea kuwasaka hadi tufike mwisho,” alisema Waziri Mkuu wakati akizungumza na Watanzania waishio Zambia katika mkutano uliofanyika kwenye Ubalozi wa Tanzania jijini Lusaka, Zambia juzi jioni (Jumanne, Mei 24, 2016).

“Hatutaki tabia iliyokuwepo ya mwananchi anakuja ofisini kutaka huduma lakini hasikilizwi hadi atoe chochote, sisi hiyo tabia hatutaki kuisikia kabisa. Tumedhamiria kurudisha heshima kwenye utumishi wa umma na nimeanza kupata faraja kwani sasa hivi (nimeambiwa) katika baadhi ya taasisi unasikia mtu akiulizwa una shida gani, nenda pale, jambo ambalo zamani halikuwepo,” alisema.

Alisema Serikali imeamua kupigia debe dhana ya utumishi wenye uadilifu kwa sababu huo ni utamaduni mpya. “Ni kipindi kigumu kidogo cha mabadiliko lakini tumesimamia mabadiliko haya na ndiyo maana watumishi wote tumewasisitizia kuwa suala la uaminifu, uadilifu na uwajibikaji ni muhimu,” alisema na kuongeza:

“Hatutamvumilia mtumishi yeyote ambaye hatakuwa tayari kuwatumikia Watanzania au atakayeendekeza uzembe lakini pia hatutamuonea mtu yeyote. Hapa tunasisitiza usawa na hatutaki kutengeneza gap kati ya mwananchi mtumishi na wa mwananchi wa kawaida, tunataka kila mwananchi aione Tanzania ni nchi yake na kila kinachozalishwa ni sehemu yake. Tukifika hapo, tunaamini kila mmoja ataweza kuisemea nchi yake.”

Akizungumzia kuhusu ubadhirifu wa fedha za umma, Waziri Mkuu alionya kwamba Serikali imelipa kipaumbele suala la uaminifu na uadilifu kwenye fedha za Serikali na kwamba haitakuwa tayari kuona fedha hizo zikifujwa.

“Hivi sasa Serikali imetenga fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya maendeleo na fedha hizo zitaenda vijijini. Tunataka zikafanye kazi iliyokusudiwa, na wale wadokozi wajue kuwa wamekalia kaa la moto,” alisema huku akishangiliwa.

Alisema watumishi wa umma wana wajibu wa kusimamia kazi zilizopangwa na kuhakikisha miradi iliyolengwa inakamilika. “Kama fedha zimeletwa kujenga zahanati simamia zahanati ijengwe na ni lazima zahanati hiyo ionekane,” alisema.

Alisema bajeti ya mwaka huu imeongezeka kutoka sh. trilioni 21 hadi trilioni 29 lengo kuu likiwa ni kuleta maendeleo kwa wananchi. “Ndiyo maana tumepandisha bajeti ya maendeleo kutoka asilimia 27 hadi asilimia 40. Ole wake atakayepokea fedha hizi halafu zisifanye kazi yake, ukiipoteza wewe utafute njia ya kwenda,” alisema huku akishangiliwa.

Akifafanua zaidi, Waziri Mkuu alisema vita inayoendeshwa imelenga kuifanya Tanzania ibadilike na itoke kwenye uchumi wa chini na kuingia uchumi wa kati. “Swali la msingi ni je tunafikaje hapo? Jibu ni kupitia uzalishaji wa bidhaa viwandani,” alisema.

“Nyote ni  mashahidi wa jinsi ambavyo shilingi yetu imekuwa ikishuka thamani kulinganisha na dola ya Marekani. Tulitoka sh. 1,600/-, tukapanda hadi sh. 1,900/- na sasa tumefikia sh. 2,180/-. Hii ni kwa sababu tunaagiza zaidi bidhaa kutoka nje ya nchi badala ya kuzalisha, hatuwezi kuendelea hivi na ndiyo maana tumeamua kuwa nchi ya viwanda. Leteni mitaji nyumbani muwekeze,” alisisitiza.

Akijibu swali kuhusu Serikali kutafuta njia ya kutoa mikopo kwa Watanzania waishio nje ya nchi, Waziri Mkuu alisema mkopo ni mkataba kati ya taasisi ya kifedha na mkopaji kwa hiyo Serikali haiwezi kubeba dhamana hiyo. “Benki wanataka ijue taarifa zako mkopaji, wanataka wajua dhamana zako ni zipi, wajiridhishe na shughuli unazofanya. Je panakopesheka hapo?,” alihoji.

Hata hivyo, aliwaeleza kwamba wakitaka kuwekeza nyumbani wanaweza kupata mikopo kutoka benki ya maendeleo ya kilimo (TADB), Benki ya Rasilmali (TIB Corporate na TIB Development). “Hizi benki ni za wakulima na wajasiriamali, na zina masharti yake, kwa hiyo ni lazima wakakague eneo lako au mahali unapofanyia biashara au wakague leseni yako na ukweli wa maombi uliyopelekea. Sasa ukiwa Zambia watawezaje kukukopesha? Kwa hiyo ukitaka fedha uwe nyumbani,” alisema.

Akijibu swali ni vipi Serikali itawasaidia wanadiaspora kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wakiwa nje ya nchi, Waziri Mkuu alisema Serikali haijawahi kujaribu jambo hilo licha ya kuwa ilikwishapokea mapendekezo kadhaa kutoka nchi mbalimbali lakini kwa vile wameliuliza, yeye analibeba na kwenda kulifanyia kazi.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZINDUA KITUO CHA KISASA CHA HUDUMA ZA MAGARI – ARUSHA


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro Mhe. Said Meck Saddik  alipowasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu
Mkoani Arusha, baada ya kukamilisha zira yake ya kikazi katika Mikoa ya Mwanza na Geita. Katikati Mkuu wa Mkoa Arusha Mhe. Daud Felix Ntibenda.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Viongozi na Makamanda wa Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa ya Kilimanjaro na Arusha alipowasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu Mkoani Arusha, baada ya kukamilisha zira yake ya kikazi katika Mikoa ya Mwanza na Geita.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia Vikundi vya Ngoma za aina mbalimbali
alipowasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu Mkoani Arusha, baada ya kukamilisha zira yake ya kikazi katika Mikoa ya Mwanza na Geita.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia Matairi ya Magari aina ya BF Goodrich KO2  yanayosambazwa na kampuni ya Superdoll baada kuwasili katika kituo cha kisasa cha huduma za magari na Matairi cha Superdoll mjini
Arusha kwa ajili ya kuzindua rasmi kituo hicho. Kusshoto Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Superdoll Seif Ali Seif.  
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akibonyeza kitufe na kupata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Superdoll Seif Ali Seif alipokua akizindua rasmi kituo cha kisasa cha huduma za magari pamoja na Matairi cha Superdoll mjini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Superdoll Seif Ali Seif baada ya kuzindua rasmi kituo cha kisasa cha huduma za magari pamoja na Matairi cha Superdoll mjini Arusha.
(Picha na OMR)

WAZIRI MKUU WA NORWAY ATETA NA MAJALIWA


 

8188Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Augustine Mahiga (kulia) wakizungumza na Waziri  Mkuu  wa Norway, Erna  Solberg katika  Mkutano kuhusu mikakati ya kupambana na rushwa uliofanyika London Uingereza, May 12, 2016.

(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

……………………………………………………………………………

WAZIRI MKUU wa Norway, Bibi Erna Solberg amesema nchi yake iko tayari kuisaidia Tanzania katika suala la kuendeleza elimu kwa mtoto wa kike.

Bibi Solberg ametoa kauli hiyo jana (Alhamisi, Mei 12, 2016) alipokutana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kufanya naye mazungumzo ya ana kwa ana kwenye mkutano wa siku moja wa Wakuu wa Nchi ulioitishwa kujadili suala la kupambana na rushwa duniani.

Akizungumza na Waziri Mkuu kwenye ukumbi wa Lancaster House, jijini London, Uingereza, Bibi Solberg alisema: “Malengo yetu kwa Tanzania ni kuendeleza elimu kwa mtoto wa kike,” na kuongeza kuwa mbali ya kuwa ni mdau wa maendeleo kwa miaka mingi, asilimia kubwa ya fedha za bajeti zinazotolewa na nchi hiyo kwa ajili ya misaada ya maendeleo zinaelekezwa Tanzania.

“Sasa hivi kuna Serikali mpya iliyoingia madarakani. Tengenezeni ajenda zenu na mzilete ili tuone ni jinsi gani tunaweza kuwasaidia,” alisema.

Akizungumzia kuhusu mkutano wa kupambana na rushwa, Bibi Solberg alisema ameufurahia mkutano huo sababu umetoa fursa kwa watu kulizungumzia kwa uwazi tatizo la rushwa. “Watu waliouwa hawalizungumzii suala hilo, hivi sasa wameanza kulijadili na kupanga mbinu ya kukabiliana na janga hilo kubwa,” alisema.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu Majaliwa aliishukuru Serikali ya Norway kwa misaada ambayo imekuwa ikiipatia Tanzania kwa kipindi kirefu.

Waziri Mkuu Majaliwa alimhakikishia Waziri Mkuu wa Norway kwamba fedha zote za misaada zinazotolewa kwa Serikali ya Tanzania ziko salama na zitatumika kwa uwazi na kwa malengo yaliyopangwa.

“Malengo ya Serikali ya sasa ni kuleta maendeleo ya kiuchumi lakini pia nchini mwetu kuna amani na usalama kwa sababu kama hakuna amani ina maana hakuna usalama,” alisema Waziri Mkuu.

Alimhakikishia Bibi Solberg kuwa Tanzania ni salama na wala hawana haja ya kutilia shaka juu ya uwepo wa amani. Pia alimtaka awahimize wawekezaji kutoka kwao waje kuwekeza kwenye uchakataji wa gesi ya kimiminika (LNG) kwa sababu ni muhimu kwa maendeleo ya nchi.

Katika mkutano huu, Waziri Mkuu amefuatana na Jaji Mkuu wa Tanzania, Othman Chande, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dk. Augustine Mahiga, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Valentino Mlowola, wataalamu wa sekta ya rushwa na wanasheria.

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU

IJUMAA, MEI 13, 2016.

MAJALIWA AMWAKILISHA RAIS JOHN MAGUFULI KWENYE MKUTANO WA KUPAMBANA NA RUSHWA LONDON


J3

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozwa kuingia kwenye ukumbi wa Lancaster House, London nchini Uingereza kuhudhuria mkutano  wa Wakuu wa Nchi kuhusu mapambano dhidi ya rushwa, May 12, 2016.  Majaliwa alimwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano huo.

J1

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akishiriki katika mazungumzo rasmi ya Wakuu wa Nchi katika Mkutano unaojadili mapambano dhidi ya rushwa kwenye ukumbi wa Lancaster House, London, nchini Uingereza May 12, 2016. Wa tatu kushoto ni Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron. Majaliwa alimwakilisha Rais John Magufuli katika mkutano huo.

(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)(P.T)

MAKATIBU WAKUU WA VYAMA VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA WAKUTANA NCHINI ZIMBABWE


 

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akitoa mada kwenye Kongamano la siku Nne la Makatibu Wakuu wa vilivyokuwa Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika. Kongamano hilo linafanyika Victoria Falls Zimbambwe lilianza tarehe 4 – 8 Mei, 2016. Vyama hivyo ni ANC ya Afrika Kusini, FRELIMO ya Msumbiji, MPLA ya Angola, SWAPO Party ya Namibia na CCM ya Tanzania.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akimpongeza Katibu Mtendaji Mkuu wa ZANU-PF Ndugu Ignatius Morgen Chombo kwa kufanikisha Kongamano  la Makatibu Wakuu wa vilivyokuwa Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika na anaeshuhudia katikati ni Katibu Mkuu wa FRELIMO Ndugu Eliseu Machava. Kongamano hilo linafanyika Victoria Falls, Zimbabwe tarehe 4 – 8 Mei 2016

 Picha ya pamoja ya Makatibu Wakuu wa vilivyokuwa Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika(FLM) wanaoshiriki Kongamano la siku Nne la kutafakari uimarishaji na uendelezaji wa ushirikiano wao na namna ya kukabiliana na changamoto walizonazo. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa ANC ya Afrika Kusini Ndugu Ndugu Gwede Mantashe, Katibu Mkuu wa FRELIMO ya Msumbiji Ndugu Eliseu Machava, Katibu Mkuu wa CCM ya Tanzania Ndugu Abdulrahaman Kinana, Makamu Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa wa Chama cha Kikomnisti cha China (CPC) Ndugu Guo Yezhou, Katibu Mtendaji Mkuu wa ZANU-PF ya Zimbabwe Ndugu Ignatius Morgen Chombo, Katibu Mkuu wa MPLA ya Angola Ndugu Juliao Mateus Paulo na Katibu Mkuu wa SWAPO Party ya Namibia Ndugu Nangolo Mbumba. Kongamano hilo linafanyika Victoria Falls, Zimbabwe tarehe 4 – 8 Mei 2016.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akibadilishana mawazo na Katibu Mkuu wa ANC ya Afrika Kusini, Ndugu Gwede Mantashe kwenye Kongamano la Makatibu Wakuu wa vilivyokuwa Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika(FLM) linalofanyika Victoria Falls, Zimbabwe tarehe 4 – 8 Mei 2016
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI