MUHAMMAD ALI KUZIKWA IJUMAA YA WIKI HII

Picha iliyokuzwa ilichukuliwa mwaka 1974 wakati Muhammad Ali alipokuwa akijindaa na pambano lake na George Foreman lililopigwa Kinshasa, DRC

Picha iliyokuzwa ilichukuliwa mwaka 1974 wakati Muhammad Ali alipokuwa akijindaa na pambano lake na George Foreman lililopigwa Kinshasa, DRC

Na Emmanuel Richard Makundi-RFI

Dunia imealikwa kuhudhuria msiba wa Muhammad Ali, kwenye mji alikozaliwa siku ya Ijumaa ambako maisha ya nguli huyu wa masumbwi yatasherehekewa huku uma ukipewa nafasi ya kushiriki mazishi na ibada ya kumbukumbu, amesema msemaji wa familia ya Ali.

Muhammad Ali, bingwa mara tatu wa uzito wa juu duniani na mwanaharakati wa haki za binadamu ambaye alikuwa nembo muhimu katika karne ya 20, alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 74 kutokana na matatizo ya kiafya yaliyochangiwa kwa muda mrefu na mapambano yake dhidi ya ukongwa wa kutetemeka “Parkinson.

Taarifa rasmi kuhusu sababu za kifo cha Muhammad Ali, imeeleza kuwa alifariki kutokana na kupata mstuko, kitaalamu inafahamika kama “Septic Shock” ambapo hata hivyo kilichosababisha mshtuko huo hakijabainishwa kitaalamu.

Mohamed Ali akiwa na mkufunzi wake Angelo Dundee

Mwanamasumbwi huyo aliyekuwa na mbwembwe na uwezo mkubwa uliongoni, na ambaye matamshi yake yalikuwa yanawagusa wengi, yalikuwa hatari kama ngumi alizokuwa akizirusha uliongoni, ambapo alikimbizwa kwenye hospitali ya Arizona mwanzoni mwa wiki iliyopita.

Wanasiasa maarufu, wanamichezo, watu maarufu na mashabiki duniani kotea walisimama kwa dakika moja kumkumba “Bingwa” ambaye maisha yake yameduni kwa miongo mitatu.

Siku ya Jumapili familia ya Ali na ndugu wa karibu, waliusinidika mwili wake kutoka Arizona kwenda Louisville alikozaliwa kusini mwa jimbo la Kentucky.(P.T)

Read more…

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s