Lowassa Atoa Waraka Kuhusu Kukamatwa Kwake


LowassaWAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ametoa waraka akisema kitendo cha askari wa Jeshi la Polisi kuwakamata wakati wakiwa kwenye kikao cha ndani cha Chadema jana  kimemuimarisha na kumpa nguvu zaidi ya kudai demokrasia.

Katika waraka wake kwa vyombo vya habari leo, Lowassa amesema anafurahishwa na kutiwa moyo na jinsi Watanzania walivyoipokea operesheni yao ya Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (Ukuta) iliyopangwa kuanza kesho kwa maandamano na mikutano, lakini vitendo vya polisi vinawapa wasiwasi wananchi.

Lowassa, akiwa na Freeman Mbowe, ambaye ni mwenyekiti wa Chadema, John Mnyika (naibu katibu mkuu-Bara) na viongozi wengine wa chama hicho kikuu cha upinzani walikamatwa jana wakiwa kwenye kikao cha ndani kilichofanyika Hoteli ya Girrafe na baadaye kwenda kituo kikuu cha polisi kwa mahojiano kabla ya kuachiwa na kutakiwa kwenda kituo hapo kesho.

Advertisements

Waziri Nape azindua michezo ya Umoja wa Vyama vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika


WAL1

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (wa tatu kulia) akiingia katika Uwanja wa Michezo wa Taifa tayari kwa ufunguzi wa mashindano ya michezo inayoshirikisha Vyama vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO), kushoto kwake ni Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Bw. Gratian Mukoba na kulia kwake ni Rais wa Chama cha Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) Bw. Henry Kapenda na Katibu Mkuu wa chama hicho Bw. Richard Gundane.

WAL3

Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Bw. Gratian Mukoba akisoma risala wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Vyama vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO), kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye.

WAL4

Rais wa Chama cha  Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) Bw. Henry Kapenda akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Umoja wa Vyama vya walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye, na kushoto ni Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT)Bw. Gratian Mukoba.

WAL6

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akitoa salamu kwa wanamichezo ambao ni walimu wanaowakilisha nchi za kusini mwa Afrika wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo leo jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Rais wa  Umoja wa Vyama vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) Bw. Henry Kapenda na kushoto ni Rais wa Chama cha Waalimu Tanzania (CWT) Bw. Gratian Mukoba.

WAL7

Kikosi cha Brass Bendi ya Polisi Nchini wakiongoza maandamano ya wanamichezo ambao ni walimu kutoka nchi za Kusini mwa Afrika kuingia uwanjani wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo leo Jijini Dar es Salaam.

WAL8

Wanamichezo ambao ni walimu kutoka Zambia wakiingia uwanjani wakati wa ufunguzi wa mashindano yaliyoshirikisha nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) leo JijiniDar es Salaam.

WAL9

Wanamichezo ambao ni walimu kutoka Afrika ya Kusini wakiingia uwanjani wakati wa ufunguzi wa mashindano yaliyoshirikisha nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) leo Jijini Dar es Salaam.

WAL10

Wanamichezo ambao ni walimu kutoka Tanzania wakiingia uwanjani wakati wa ufunguzi wa mashindano yaliyoshirikisha nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) leo Jijini Dar es Salaam.

WAL11

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akifyatua baruti juu kuashiria ufunguzi rasmi wa mashindano ya Vyama vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika(SATO) leo JijiniDar es Salaam.

WAL12

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimiana na wachezaji wakati wa  ufunguzi  wa mashindano ya  Vyama Vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) leo Jijini Dar es Salaam.

WAL13

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimiana na wachezaji wakati wa  ufunguzi  wa mashindano ya  Vyama Vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) leo Jijini Dar es Salaam.

Picha Na: Lorietha Laurence WHUSM

……………………………………………………………………

Lorietha Laurence – WHUSM

Michezo ni mojawapo ya nyenzo muhimu katika kuimarisha ushirikiano  na mahusiano baina ya nchi na nchi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye wakati wa ufunguzi wa michezo ya Umoja wa Vyama vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) ambayo imeanza rasmi leo Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Nnauye amesema kuwa ni fahari kubwa kwa serikali ya Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano hayo kwa kuwa inatoa fursa kwa wageni na wenyeji kujumuika kwa pamoja na kujifunza mbinu mbalimbali za kimichezo.

“Kuunganisha nchi na nchi si kazi rahisi lakini kupitia michezo imekuwa ni jambo rahisi kwa kuwa inawafanya kuwa na umoja uliothabiti na hivyo kuimarisha mahusiano baina ya nchi husika” alisema Mhe. Nnauye

Aidha Mhe. Nnauye aliwataka washiriki wasiishie kwenye michezo tu bali pia watumie  fursa ya kuwepo nchini kwa kutembelea vivutio mbalimbali vilivyopo katika Jijini la Dar es Salaam ikiwemo Makumbusho ya Taifa pamoja na Bagamoyo ambako kuna historia kubwa ya nchi.

Naye Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Bw. Gratian Mukoba ameeleza kuwa mashindano hayo ni muhimu kwa walimu kwa kuwa yanawasiadia kuimarisha afya pamoja na kushirikiana katika kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili  sekta hiyo.

“kupitia michezo hii tunaimarisha afya pamoja na kujadili changamoto  mbalimbali wanazokumbana nazo walimu ikiwemo ukosefu wa walimu wa masomo ya hesabu na sayansi na namna ya kutatua tatizo hilo “ alisema Bw. Mukoba.

Kwa upande wake Rais wa Vyama vya Walimu  wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) Bw. Henry Kapenda amesema kuwa kupitia michezo hiyo walimu hujifunza tamaduni mbalimbali baina yao ukizingatia elimu ndio msingi wa maendeleo.

Mashindano haya ya Umoja wa Vyama vya Walimu wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SATO) yanafanyika kwa mara ya sita huku Tanzania ikiwa mwenyeji wa mashindano hayo kwa mara ya kwanza ikihusisha nchi za Namibia, Lesotho, Botswana, Zimbabwe, Zambia, Malawi, Afrika ya Kusini, Swizland na Tanzania.

DKT. SHEIN AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI LEO


index

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Dkt. Ali Mohamed Shein amefanya uteuzi wa viongozi katika Taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee, ACP Sida Mohammed Himid ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ anayeshughulikia Idara maalum za SMZ.

Ndugu Hassan Khatib Hassan ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto anayeshughulikia masuala ya Wazee, vijana, wanawake na Watoto.

Dkt. Ali Salim Ali ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Mnazi mmoja katika Wizara ya Afya.

Uteuzi huo umeanza leo tarehe 30 Agosti, 2016.

Bw. Mohammed Kheir Mtumwa ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala kuanzia tarehe 28 Agosti, 2016.

MHE. AUGUSTINO MREMA AWATAKA WATANZANIA KUYAPUUZA MAANDAMANO YA CHADEMA SEPTEMBA MOSI MWAKA HUU


 

mrema
Na Ismail Ngayonga-MAELEZO
Dar es Salaam

 

WAZIRI wa zamani wa mambo ya ndani ya nchi, Augustino Mrema amewataka Watanzania kuyapuuza  maandamano ya Septemba Mosi mwaka huu yaliyoandaliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na badala waendelee na shughuli za ujenzi wa Taifa.
Mrema alisema hakuna haja ya kufanya maandamano Septemba Mosi kwani hayana faida yoyote kwa taifa badala yake wananchi wa kawaida ndio watakaoathirika.
 
Akizungumza katika mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii leo Jijini Dar es Salaam, Mhe. Mrema ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Misamaha kwa Wafungwa (Parole) alisema mikutano ya hadhara na maandamano yasiyokwisha kila kukicha yatasababisha wananchi wasifanye kazi.
Nchi yetu ni maskini hivyo tunahitaji wananchi wafanye kazi kwa bidii” alisema Mrema. Alisema iwapo CHADEMA  wataona wameonewa ni vyema  watumie njia za mazungumzo au ikibidi kwenda mahakamani badala ya kufanya maandamano ambayo yanaweza kusababisha vurugu na kuharibu amani na utulivu wa nchi.
 
Aliwataka Watanzania kukumbuka maandamano ya mwaka 2001 yaliyoitishwa na Chama cha Wananchi (CUF) huko Zanzibar ambapo watu kadhaa waliuwawa na mamia kukimbilia uhamishoni nchini Kenya na Somalia.
 
Akizungumzia kuhusu utendaji kazi wa Serikali ya Awamu, Mhe. Mrema alimpogeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa hatua yake ya kurejesha maadili na miiko ya utumishi kwa watumishi wa umma nchini hali iliyosaidia kurejesha uwajibikaji wa Serikali kwa wananchi.
Mrema alisema tangu kuingia madarakani kwa Serikali ya Awamu Tano, kumekuwepo na mabadiliko kwa watendaji wa umma katika ngazi mbalimbali za kimamlaka ukitofautisha na miaka ya nyuma ambapo baadhi ya watendaji walikuwa wakifanya kazi kwa mazoea.
“Viongozi wengi wa umma walikuwa wakifanya kazi kwa mazoea bila kujali wajibu wao na wala hakukuwa na uwajibikaji cha kusikitisha mamlaka husika zilikuwa haziwachukulii hatua za kinidhamu, hivyo viongozi wa umma badala ya kuwatumikia wananchi wakawa wanatumikia matumbo yao” alisema Mrema.
Mrema alisema Rais Magufuli ameanza kutekeleza kwa vitendo ahadi yake aliyoitoa kwa wananchi ya kuwaondoa madarakani viongozi wazembe na wasiowajibika na wasiokuwa na uwezo wa kufanya kazi katika kuwatumia wananchi.
Aliongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inastahili pongezi kwa hatua inazochukua katika mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa na ufisadi ikiwemo uanzishwaji wa Mahakama ya Mafisadi nchini, kwani hakuna maendeleo yatakayoweza kupatikana katika nchi pasipo na kupiga vita rushwa.
Mrema alisema ni wajibu wa kila mwananchi kuichukia rushwa kwa vitendo ikiwemo kuwafichua hadharani kikundi cha watu kinachojihusisha na rushwa kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia Tanzania kupiga hatua kubwa za maendeleo.
“Kama mnavyokumbuka mimi nilifukuzwa kazi serikalini kwa sababu ya kupinga ufisadi ambao kwa wakati ule ulikuwa umekithiri serikali, ivyo nilichokuwa nikikipigania mimi ndicho anachifanya Rais Magufuli” alisema Rais Magufuli.
 
Akizungumzia kuhusu hatua ya Serikali ya Awamu ya Tano kuhamishia shughuli zake Mjini Dodoma, Mrema alipongeza uamuzi huo kwani kiulinzi na kiusalama Dodoma ni pazuri zaidi kuliko Dar es Saalam kwani ni katikati ya nchi.
“Dodoma panafaa sana kiulinzi na usalama kwa kuwa ni vigumu kwa adui watoke baharini wafike hadi Dodoma kabla hawajathibitiwa” alisema Mrema.
 
“Kuhusu ubora wa miundombinu ya Mkoa wa Dodoma Mrema alisema Mkoa huo unafikika kirahisi zaidi kwa wananchi waishio mikoa ya pembezoni na mipakani kufika Dodoma kuliko ilivyo Dar es salaam ambayo iko Mashariki kabisa ya nchi”  alisema Mrema.Chanzo:www.fullshangweblog

RAIS DKT. MAGUFULI ALIPOHUTUBIA MKUTANO GEITA MJINI !


1

2

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wakazi wa Geita mjini mara baada ya kuwasili kutoka Kahama.

3

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka katika viwanja vya mikutano vya Geita mjini mara baada ya kuhutubia.

4

Wananchi wa Geita wakionesha furaha yao wakati Rais Dkt. Magufuli alipokuwa akihutubia mkutano viwanjani hapo.

PICHA NA IKULU (P.T)