MAJALIWA AWASILI KIBITI KWA ZIARA YA SIKU MOJA Wednesday, 28 September 2016


kibi1

Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum Zainab Vullu baada ya kuwasili kwenye  Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kibiti kwa ziara ya siku moja wilayani humo Septemba 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

kibi2

Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na Wabunge, Zaibab Vullu wa Viti Maalum (kulia) na  Ali Ungando wa Kibiti  baada ya kuwasili kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kibiti akiwa katika ziara ya  siku moja wilayani humo Septemba 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Dk.Kigwangalla afanya ziara Hospitali za Wilaya ya Mlele na Mpanda Mkoani Katavi


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Chifu Kayamba wa Pili wa Kabila la Wakonongo. Wakati wa kupokelewa alipowasili ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Mlele,Mkoani Katavi.

Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Bi.Rachel Kasanda akisoma taarifa kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla (katikati).

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua moja ya vifaa katika chumba cha Maabara ya hospitali ya Mlele.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla amefanya ziara ya kikazi katika Wilaya ya Mlele na kutembelea Hospitali ya Mlele ya Wilaya hiyo pamoja na Hospitali ya Mpanda iliyopo Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi huku akitoa maagizo mbalimbali ya kiutendaji.

Katika ziara yake katika Hospitali ya Mlele, Dk.Kigwangalla amewaagiza viongozi wa Serikali wa Wilaya na ule wa Hospitali hiyo kuhakikisha wanakamilisha mambo muhimu ikiwemo ujenzi wa chumba cha upasuaji, jengo la kuhifadhia mahiti na vitu vingine huku akitaka ndani ya miezi mitatu view vimekamilika.

Akiwa katika Hospitali hiyo ya Mlele, Dk.Kigwangalla ameweza kutembelea sehemu mbalimbali za hospitali pamoja na kukagua ujenzi wa majengo ya Chumba cha upasuaji, chumba cha kuhifadhia maiti na majengo mengine ambapo amemtaka Mkuu wa Wilaya kuhakikisha wanafanya juhudi wanakamilisha kwa wakati majengo hayo ili wananchi wapate huduma bora.

Kwa upande wa ziara yake hiyo katika Wilaya ya Tanganyika yaliyopo makao makuu ya Mkoa wa Katavi, Dk. Kigwangalla ameweza kutembelea Hospitali ya Mpanda ambayo kwa sasa inahudumia kama Hospitali ya Mkoa ambapo napo ameagiza kufanyiwa marekebisho mbalimbali ikiwemo kuzingatia masuala usafi.

Aidha, ametoa maagizo kuhakikisha wanafunga mfumo wa malipo wa kisasa katika vyanzo vyote vya mapato ili kukusanya pesa nyingi zaidi zitakazoweza kuendesha huduma za Afya ndani ya Hospitali hiyo. Chanzo:mjengwablog

MHE. JANUARY MAKAMBA AWATOA WASIWASI WAATHIRIKA WA TETEMEKO KAGERA


maka1

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. January Makamba (kushoto) akimpa pole waathirika wa tetemeko la ardhi waliolazwa Hospitali ya Rufaa ya Bukoba jana 22/9/2016.

maka2

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. January Makamba (kushoto) akiwapa pole waathirika wa tetemeko la ardhi waliolazwa Hospitali ya Rufaa ya Bukoba jana 22/9/2016.

maka4

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. January Makamba (kulia) akimpa pole Mwalimu Mkuu Shule ya Sekondari Ihunga Bw.Thomas Bonevanture mara alipowasili shuleni hapo kuwapa pole waathirika jana 22/9/2016.

maka5

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. January Makamba (katikati) akiwa ameongozana na Mkuu wa Wilaya ya Misenyi Luteni Kanali Denice Filangali Mwila (kushoto) pamoja na Diwani wa Kata ya Bugandika Bw. Amudi Migeyo kwenda kuangalia maeneo yaliyoathirika na tetemeko la ardhi jana 22/9/2016 Wilayani Misenyi.

maka6

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. January Makamba (wa pili kushoto) pamoja na viongozi wengine wakiwapa pole baadhi ya waathirika wa tetemeko la ardhi Wilayani Misenyi leo 22/9/2016.

Na Benedict Liwenga-WHUSM, Bukoba.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. January Makamba amewatoa wasiwasi waathirika wa tetemeko la ardhi lilitokea Wilayani Bukoba Mkoani wa Kagera.

Mhe. Makamba ameyasema hayo leo mkoani Kagera wakati wa ziara yake ya kutembelea maeneo mbalimbali yaliyokumbwa na tetemeko hilo kwa lengo la kuwapa pole waathirika na kuwap ujumbe wa Serikali kuhusu namna inavyojitahidi kuwasaidia waathirika hao.

Amesema kwamba, wananchi wasiwe na wasi wasi kuhusu suala la kupatiwa misaada ya dharura kwani Serikali imejipanga na bado inaendelea na zoezi la kufanya tathmini ya uharibifu uliotokea ingawa zoezi la kuwapatia baadhi ya huduma za msingi linaendele.

“Tumekuja kutoa msaada kwa mji kwa ujumla wakati tunapanga namna ya kusaidia katika masuala ya mazingira na tambueni kuwa Serikali inawajali ndiyo maana kuna viongozi wakubwa wako hapa na wengine wanazidi kuja”, alisema Mhe. Makamba.

Aliongeza kuwa, suala la kuwasaidia waathirika wa tetemeko hilo limepewa uzito mkubwa na Serikali na suala la kuchelewa kwa kutolewa kwa misaada kunatokana na umakini unaoendelea kufanywa sasa hivi na Serikali ili kuwatendea haki waathirika pekee.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Misenyi Luteni Kanali Denice Filangali Mwila amesema kuwa katika Wilaya yake sehemu iliyoathirika zaidi ni Kata ya Minziro ambapo jumla ya nyumba 512 haziwezi watu kuishi,pia nyumba 1,524 zenye nyufa mbalimbali zinazohitaji ukarabati, Taasisi za serikali 91 na taaisis 71 za watu binafsi ikiwemo makanisa na misikiti imeathirika na tetemeko hilo.

Ameongeza kuwa tayari amepata msaada wa Serikali katika tukio hilo kupitia Kamati ya Maafa ambapo jumla ya maturubai 520 amepewa kwa ajili ya maeneo mbalimbali, chakula, blanketi 240 ambazo pia zimegaiwa kwa waathirika hao.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Bugandika Bw. Amudi Migeyo amewataka wananchi wake kutobeza juhudi za Serikali zinazofanywa sasa na amewataka kuridhika na chochote wakipatacho katika kipindi hiki kigumu.

Hivi karibuni siku ya tarehe 10 Septemba, 2016 mkoa wa Kagera ulikumbwa na ukubwa wa nguvu za mtetemo wa ardhi wa tetemeko la 5.7 kwa kutumia skeli ya ‘Ritcher’ ambapo jumla ya watu 17 walipoteza maisha na majeruhi kadhaa ambapo wengi wao wameshapatiwa matibabu na wanaendelea vizuri.

MBUNGE WA SIMANJIRO JAMES OLE MILYA AZINDUA MADARASA MANNE YA SHULE YA MSINGI EMBOREET MARA,SIMANJIRO


Mbunge wa Simanjiro James Ole Millya akishikana mikono na  Mwanamuziki wa nchini Marekani Kristie Cooter ishara ya  uzinduzi wa  madarasa manne katika shule hiyo yaliyojengwa kwa ufadhili wa shirika lisilokua la kiserikali la Wings of Kilimanjaro.Picha na Woinde Shizza

Mbunge wa Simanjiro James Ole Milya akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Emboreet mara baada ya kuzindua madarasa manne katika shule hiyo yaliyojengwa kwa ufadhili wa shirika lisilokua la kiserikali la Wings of Kilimanjaro.

Mbunge wa Simanjiro James Ole Millya akiteta jambo na Mwanamuziki wa nchini Marekani Kristie Cooter katika uzinduzi wa  madarasa manne katika shule hiyo yaliyojengwa kwa ufadhili wa shirika lisilokua la kiserikali la Wings of Kilimanjaro.PICHA NA WOINDE SHIZZA

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA URUSI NA JAMHURI YA KOREA HAPA NCHINI IKULU JIJINI DAR


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi wa Jamhuri ya Korea hapa  nchini Song Geum-Young mara baada ya kupokea picha hiyo ya mfano wa Daraja jipya la Salenda.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kumkaribisha  Balozi wa Urusi hapa nchini Yuri Popov aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiaagana na Balozi wa Urusi hapa nchini Yuri Popov mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kumkaribisha  Balozi wa Jamhuri ya Korea hapa nchini Song Geum-Young aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea picha ya mfano wa Daraja jipya la Salenda litakojengwa kuanzia maeneo ya Hospitali ya Agha Khan na kupita baharini  hadi eneo la Coco beach jijini Dar es Salaam kutoka kwa Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Song Geum-Young aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo. Daraja hilo litakuwa na urefu wa kilomita 7 na kati ya hizo kilomita 1.4 zitapita baharini na ujenzi wake unatarajiwa kuanza mwezi Juni mwakani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Song Geum-Young mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkemia Mkuu wa Serikali Profesa Samwel Manyele Ikulu jijini Dar es Salaam.

PICHA NA IKULU.

Mkutano wa Kilele wa G20 waanza China


Mkutano wa kilele wa siku mbili wa kundi la G20 umefunguliwa nchini China Jumapiliv (04.09.2016) kwa wito kwa chombo hicho kuwa timu ya vitendo badala ya kuwa mahala pa kupiga porojo.

Akifunguwa mkutano huo katika mji wa Hangzhou Rais Xi Jinping wa China amesema anataraji huko Hangzhou wanaweza kushughulikia dalili za matatizo halikadhalika sababu kuu za matatizo ya uchumi wa dunia …..”G20 inapaswa ibadili mtizamo wake na kuweka umuhimu sawa kwa sera za muda mfupi na sera za muda mrefu.”

China ni mwenyeji wa viongozi 20 wa kundi hilo la nchi zenye maendeleo makubwa ya kiuchumi duniani na zile zenye kuinukia kiuchumi katika mji mashuhuri wa kihistoria wa Hangzhou ulioko mashariki mwa China kuanzia Jumapili (04.09.2016) hadi Jumatatu ambapo usalama umeimarishwa kwa kuwekwa kwa vikwazo barabarani.

Rasi Xi alisalimiana kwa kupeana mikono na wageni waliokuwa wakiingia mmoja baada ya mwengine katika kituo cha Maonyesho ya Kibiashara cha Kimataifa cha Hangzhou kunakofanyika mkutano huo miongoni mwao Rais Barack Obama wa Marekani, Kansela Angela Merkel wa Ujerumani, Rais Vladimir Putin wa Urusi, Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki, Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini.

Dhima ya China

Tukio hilo linaonyesha dhima ya China katika jukwaa la dunia wakati baadhi ya viongozi wakitarajiwa kuishinikiza China kutii kanuni za kimataifa za biashara na uzaslihaji wake wa kupindukia wa chuma.

Katika hotuba yake ya ufunguzi Rais Xi amesema kundi hilo la G20 halipaswi kuchukuwa hatua mpya za kuhami masoko na badala yake ichukuwe hatua madhubuti za kuchochea ukuaji wa uchumi duniani.

Obama na XI walikutana Jumamosi jioni ambapo nchi zote mbili zilitangaza kujiunga rasmi na makubaliano ya Paris ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Wakati wa mazungumzo yao yaliochukuwa muda mrefu Xi aliihimiza Marekani kutimiza dhima yenye tija katika kudumisha amani na utulivu katika eneo la Bahari ya China Kusini.China inadai kumiliki takriban eneo lote hilo ambalo pia linagombaniwa na Vietnam, Taiwan,Ufilipino,Malaysia na Brunei.

Nafasi ya vyombo vya habari yaleta tafrani

Mkutano wa Xi na Obama ulitiwa kiwingu na mzozo kuhusu suala la vyombo vya habari kuuangazia mkutano huo ambapo hapo Jumapili Rais Obama alikiri kwamba kulikuwepo na mvutano kuhusiana na sisitizo la Marekani la kujumuishwa kwa vyombo vya habari wakati wa Mkutano huo wa kilele wa kundi la mataifa 20 ambapo amesema hatoomba radhi kwa kuvitetea vyombo vya habari.

Akizungumza katika mkutano huo Obama amesema “tunafikiri ni muhimu kwamba vyombo vya habari vinapatiwa nafasi ya kuelewa kazi tunayoifanya ili wawe na uwezo wa kujibu maswali. Hatuyaachi nyuma maadili yetu wakati tunapofanya safari hizi.”

Mzozo huo ulianza mara baada ya kutuwa kwa ndege ya Air Force One katika mji wa Hangzhou hapo Jumamosi ambapo kundi la waandishi wa Kimarekani lililokuwa likiandamana na Rais Obama lilipozuiliwa wakati rais alipokuwa akiteremka kwenye ndege ambapo afisa wa China aliwapigia makelele wafanyakazi wa Ikulu ya Marekani kuwaondowa kabisa waandishi wa habari katika eneo hilo.

Wakati afisa wa Ikulu aliposema hilo lilikuwa ni suala linamhusu rais wa Marekani na kwamba hiyo ilikuwa ni ndege ya Marekani kwa hiyo waandishi hao wataendelea kubakia katika eneo hilo afisa huyo wa China alijibu kwa ukali kwamba “Hii ni nchi yetu”.

Afisa huyo pia alipapurana na Mshauri wa Usalama wa Taifa Susan Rice na Naibu Mshauri wa Usalama wa Taifa Ben Rhodes wakati walipokuwa wakijaribu kutembea karibu na Rais Obama.Kuhusiana na kisa hicho Rice alisema baadae “Wamefanya mambo ambayo hawakuyategemea.”

Mvutano huo uliendelea tena hapo Jumapili wakati sehemu ya mkururo wa vyombo vya habari uliokuwa ukimsindikiza Obama ulipozuiliwa kukaribia eneo la mapokezi la mkutano huo wa kilele wa G20.

Mbali na suala la ukuaji wa uchumi mkutano huo unatowa fursa kwa viongozi kujadili masuala mbali mbali muhimu duniani.DW