SERIKALI ITAWACHUKULIA HATUA WATAKAOBAINIKA KUHUSIKA NA MATUKIO YA MOTO MKOANI ARUSHA

A1

Mkurugenzi wa Elimu ya Msingi katika Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Sarah Mlaki, akimkabidhi cheti cha kumaliza darasa la saba mhitimu Mercygracious Tolla wa Shule ya Msingi ya Macedonia kwenye mahafali ya tano ya shule hiyo iliyoko Tabata Segerea jijini Dar es Salaam.

A2

Hussein Makame-MAELEZO

SERIKALI imesema itawachukulia hatua stahiki wale wote watakaobainika kwa sababu moja au nyingine kuhusika na matukio ya moto yaliyotokea mkoani Arusha hivi karibuni.

Hayo yamesema na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. SimonMsanjila katika mahafali ya tano ya Shule ya Msingi ya Macedonia iliyopo Tabata Segerea jijini Dar es Salaam yaliyofanyika mwishoni mwa wiki.

Akizungumza kwa niaba ya Prof. Msanjila ambaye alialikwa kuwa mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Elimu ya Msingi wa wizara hiyo Sarah Mlaki alikuwa akijibu kilio cha Mkuu wa shule hiyo aliyelaani matukio hayo ya moto kuendelea kujitokeza huko mkoani Arusha na maeneo mengine.

Alisema mbali na kuwachukulia hatua wahusika, Serikali imechukua hatua mbalimbali kudhibiti majanga ya moto katika shule zetu za sekondari za bweni nchini.

“Serikali imechukua hatua mbalimbali kudhibiti majanga ya moto katika shule zetu za sekondari za bweni.Tutachukua hatua stahiki kwa wale ambao watabainika kwa sababu moja au nyingine wanahusika na majanga hayo”, alisema Mkurugenzi Mlaki.

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa Serikali pia imejipanga kuboresha miundombinu ya shule zake ili watoto Watanzania wapate haki yao ya msingi ya kupata elimu.

Kwa upande mwingine, Mkurugenzi Mlaki alisema soko la vitabu vya kiada vinavyotumika katika shule  za msingi nchini limevamiwa na watu mbalimbali na Serikali inafahamu kuwa kuna vitabu vingine havina ubora unaostahili kwa matumizi ya shule.

Hata hivyo, Mkurugenzi Mlaki alisema Serikali kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania (TEA) imepewa dhamana ya kuandaa vitabu vya kiada ili wanafunzi wote kutumie vitabu hivyo bila ya kuwa na tofauti katika elimu inayotolewa.

“Kwa kweli soko la vitabu limevamiwa na watu mbalimbali na tunafahamu kuna vitabu vingine havina ubora stahiki, lakini Serikali kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania (TEA) imepewa dhamana ya kuandaa vitabu vya kiada (text book) ili wanafunzi wote waweze kutumia vitabu hivi pasiwe na tofauti katika elimu inayotolewa” alisema Mkurugenzi Mlaki.

Aliongeza kuwa anaamini kwamba tatiz hilo litatatuliwa kadri siku zinavyokwenda kwa kuwa taasisi husika tayari inalishughulikia suala hilo kulingana na uzito wake.

Katika mahafali hayo jumla ya wanafunzi 53 wa shule hiyo walihitimu na wanatarajia kufanya mitihani ya taifa ya darasa la saba mwaka huu, wakiwemo wanafunzi 24 wanaume na wanawake 29.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Shukuru Mbwire alisema shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 2009, imekuwa ikifanya vizuri katika mitihani ya darasa la saba na la nne ambapo ilianza na wanafunzi 70 lakini hadi sasa ina wafanuzi 782.

Alisema katika matokeo ya mitihani ya kitaifa ya darasa la saba shule hiyo imekuwa ikifanya vizuri mwaka hadi mwaka ambapo katika mitihani ya mwaka 2015 shule hiyo ilipata wastani wa daraja A na kushika nafasi ya 3 kati ya shule 56 kiwilaya, nafasi ya 28 kati ya shule 534 kimkoa na kitaifa ilishika nafasi ya 219 kati ya shule 16,096.

“Kwa miaka yote hiyo shule ilifaulisha wanafunzi kwa asilimia 100 ambapo watoto wote walifanikiwa kujiunga na shule za Sekondari za vipaji maalum na zile za kawaida” alisema Mbwire.

Katika risala ya wanafunzi wa shule hiyo, wahitimu walitangaza kumuunga mkono kaulimbiu ya Rais John Pombe Magufuli ya Hapa Kazi Tu na kuwataka Watanzania wafanye kazi kwa bidii ili kulikomboa Taifa na umasikini.Chanzo:mjengwablog

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s