Posts by kifltd-kif Enterprises

Blogger/Managing Director of King Kif Productions

zanzibariyetu, Zanzibar Yetu just now


Waahidiwa kiwanja cha kimataifa

Dk. Ali Mohamed Shein, amewaahidi wananchi wa Kitogani kuwa uwanja wao utatengenezwa kwa kiwango ha Kimataifa kitakachoshirikisha michezo ya aina mbali mbali.

Dk. Shein aliwaeleza wananchi hao wa kijiji cha Kitogani kuwa kijiji chao kitakuwa eneo la michezo kwani watafika watu kutoka ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kuutumia uwanja wao mpya unaoendelea kujengwa ambao tayari kwa awamu ya kwanza umekamilika.

Hivyo, amewataka wakaazi wa Kitogani kujiandaa kuwapokea wageni wakiwemo wanamichezo huku akieleza jinsi Serikali ilovyojiandaa kukijenga kiwanja hicho kuwa cha kisasa na kuweza kuchezwa michezo kadhaa mbali na mpira wa miguu.

KISHAPU YAZINDUA KAMPENI YA KUHAMASISHA WANANCHI KATIKA SHUGHULI ZA KILIMO NA ELIMU


 

3

Katibu Tawala wa Wilaya, Shadrack Kengese akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha shughuli za kilimo na elimu kwa wananchi. Ofisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika katika halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Godwin Everygist akifafanua jambo kwa wananchi wakati wa uhamasishaji wa shughuli za kilimo. Ofisa Elimu Sekondari …

Read More »

WAZIRI WA ELIMU PROF. NDALICHAKO AZINDUA BODI MPYA YA MAMLAKA YA ELIMU TANZANIA (TEA)


1

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako (kulia) akielekea kwenye ukumbi kwaajili ya kuzindua Bodi mpya ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) leo jijini Dar es Salaam (kushoto) Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA ) Graceana Shirima .

2

Wajumbe wa Bodi ya Elimu Tanzania (TEA) wakiwa wamejipanga kumpokea mgeni rasmi Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako wakati wa uzinduzi wa Bodi mpya ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) leo jijini Dar es Salaam.

HEBU CHEKI….WANANCHI WAPONGEZA UKAMILISHAJI WA BARABARA MKOANI RUVUMA


1

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akisikiliza maoni kutoka kwa Bw. Mohammed Ally mkazi wa Nakapanya, Wilayani Tunduru, Mkoani Ruvuma kuhusu furaha yao juu ya kukamilika kwa ujenzi wa Barabara ya Nakapanya-Tunduru KM 66.5.

2

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akionesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani), picha ya barabara ya Nakapanya-Tunduru KM 66.5 iliyokamilika kwa kiwango cha lami wakati alipokuwa akikagua barabara hiyo, mkoani Ruvuma. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Bw. Juma Homera.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na wadau wa sekta ya filamu…


NAP1

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kushoto) akizungumza na wadau wa sekta ya filamu (hawapo pichani) wakati wa kikao cha wadau kuzungumzia sera ya filamu leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura na Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi. Nuru Millao