JAMII

Nafurahishwa tena na juhudi zako za makusudi za  kusimamia uelewa mpana wa dhana nzima ya kutungwa kwa katiba mpya  itakayokuwa na maslahi kwa Tanzania na watanzania wote bila kujali dini,  rangi, mahusiano ya kisiasa n.k
Katika hoja hii ya leo, nimesoma  katika mistari na kuelewa kuwa, katika muswada wa sheria uliopitishwa na  bunge hivi karibuni wa kuanzishwa rasmi mchakato wa mabadiliko ya  katiba, kuna vipengele ambavyo vimewekwa kwa makusudi kwa maslahi ya  watu fulani au kundi fulani na wala si kwa Tanzania na watanzania kwa  ujumla.
Ninaamini wewe ni muandishi kwa taaluma, hivyo itakuwa vizuri  kama utafanya kazi ya ziada ya kupitia muswada huo mzima na kuweza  kutumia taaluma yako ya uandishi na kuainisha maeneo ambayo ki msingi  yanautata ili watu(wasomaji) wa makala utakazokuwa unatuma waweze kutoa  maoni yao.
Vile vile, kwa kuwa inajulikana kuwa tayari kuna vipengele  muhimu katika mchakato huo ulopitishwa na bunge vinautata, basi ndio  nafasi nzuri kwa wanasiasa hasa wapinzani kupanda majukwaani na kuanza  kuwaelimisha wananchi juu ya athari za vipengele hivyo muhimu katika  future ya nchi na wananchi wake.
Hayo ni maoni yangu binafsi, unaweza  kuyakubali au vinginevyo. Kama utakubaliana nayo, unaweza vilevile kuwa  wakala wangu kufikisha mtazamo wangu kwa wanasiasa ambao unadhani  watakuwa wasikivu na wanaozingatia hoja za wadau kama mimi.Mwilima
NYC.

7 Comments

  1. wakinamama! Juuuuuuuuuuuuuuuuu ,Basi ningependa kuwapongeza kwa kazi nzuri sana na ningeomba kwa wakinamama wengine kuiga mfano huo,asanteni sana kwakujituma nawapa pongezi kwadhati.

    Like

    Reply

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s