ATCL YATOA OFA YA MWEZI MMOJA KWA SAFARI ZA MWANZA


image

Na Daudi Manongi-MAELEZO

Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) imetoa ofa ya mwezi mmoja kwa abira wanaosafiri kutoka Dar es salaam kwenda Mwanza kulipa nauli ya shilingi 160,000/- kwa safari moja.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na na Kaimu Afisa Mawasiliano wa Kampuni Bi.Lily Fungamtama wakati akiongea na Idara ya Habari.

Amesema Ndege za Kampuni zimeanza kutoa huduma kuanzia Jumamosi ya wiki iliyopita ya tarehe 15 ya mwezi huu kama ilivyobainisha kupitia vyombo vya Habari.

Safari hizo zilianza kwa kutoa huduma ya kusafirisha abiria kuelekea nchini Comoro na hapa nchini itoa safari katika mikoa ya Mwanza, Arusha na Kigoma.

Bi.Fungamtama amesema kwa kuanzia walianza na mazoezi ya vitendo kwa marubani na wafanyakazi wa ndani ya Ndege ambapo hatimaye walianza safari za biashara ya kusafirisha abiria mnamo tarehe 15 Oktoba kama ilivyopangwa.

Ameongeza kuwa ATCL imeboresha huduma zake kwa kiasi kikubwa kwa kuwapatia wateja wake ofa ya kubeba kilo 20 za mizigo na kilo 7 za mzigo wa mkononi bure   pamoja na kutoa vinywaji na ubadilishaji wa tiketi ni bure ndani ya mwezi.

Aidha, Kaimu Afisa Mawasiliano wa Kampuni Bi.Lily amekanusha taarifa potofu kuwa zimekwama kuanza safari zilizopangwa.

Amesema kuwa habari hizo sio za kweli kwani hivi sasa wameshaanza huduma katika mikoa hiyo mitatu.

Kampuni ya Ndege ya ATCL kwa sasa ina ndege tatu,zikiwemo mbili aina ya Dash8-Q400 zenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja na Dash8-Q300 moja yenye uwezo wa kubeba  abiria 50.Chanzo:mjengwablog

Makamu Wa Rais Azindua Mradi Wa Ujenzi Wodi Za Wazazi


samia-6Makamu wa Rais, Samia Suluhu akizindua jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo la wazazi katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala Dar.samia-5Baadhi ya wananchi mbalimbali waliofika kushuhudia hafla hiyo.  samia-7Makamu wa Rais (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi waliofika katika hafla hiyo.

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, leo amezindua mradi wa ujenzi wa majengo matatu ya wodi za wazazi wenye thamani ya shilingi bilioni 4.5 kwa Halmashauri tatu za jiji la Dar es Salaam.

Mradi huo wa ujenzi ulizinduliwa katika Hospitali za Rufaa za Mwananyamala (Kinondoni) , Amana (Ilala) na ile ya Temeke .

Akizungumza katika hafla hiyo, Samia Suluhu alimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa juhudi zake katika kutafuta wadau  mbalimbali na kufanikisha kujitolea kujenga majengo hayo ambayo yatakuwa muhimu kwa wazazi mkoani Dar. Pia alimshukuru Mkurugenzi wa Amsons Group, Abdallah Naheer kwa kukubali kujenga majengo hayo yatakayopunguza vifo vya akina mama na watoto.

Kwa habari kamili tembelea Global TV Online kuona hotuba kamili ya hafla hiyo.

Na Denis Mtima/Gpl.Chanzo:globalpublishers.info

MFUMUKO WA BEI WA TAIFA KWA MWEZI SEPTEMBA 2016 UMEPUNGUA KWA ASILIMIA


Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Ephraim Kwesigabo (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar eas Salaam leo, kuhusu mfumuko wa bei ya taifa kwa mwezi Septemba 2016.

Mkutano na wanahabari ukiendelea.

waandishi wa habari wakichukua taarifa hiyo.

Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo

Na Dotto Mwaibale

MFUMUKO wa Bei wa Taifa kwa mwezi Septemba, 2016 umepungua hadi asilimia 4.5 kutoka asilimia 4.9 ilivyokuwa mwezi Agosti 2016.

Hayo yabebainishwa na Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Ephraim Kwesigabo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar eas Salaam leo.

” Hii inamanisha kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Septemba, 2016 imepungua ikilinganishwa na kasi ya upandaji ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti 2016 ” alisema Kwesigabo.

Alisema  Fahirisi za bei zimeongezeka hadi 103.05 mwezi Septemba 2016 kutoka 98.64 mwezi Septemba 2015.Kwesigabo aliongeza kuwa mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi mwezi Septemba 2016 umepungua hadi asilimia 6.0 kutoka asilimia 7.0 ilivyokuwa mwezi Agosti 2016.

Alisema  kupungua kwa mfumuko wa bei wa mwezi Septemba 2016 kumechangiwa na kupungua kwa kasi ya bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi Septemba 2016 zikilinganishwa na bei za mwezi Septemba 2015.

Alisema mwenendo wa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula zilizoonesha kupungua ni pamoja na bei za dagaa kwa asilimia 11.6 na viazi vitamu kwa asilimia 3.2.

“Kwa upande mwingine mwenendo wa bei za baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilionesha kupungua ni pamoja na bei za gesi kwa asilimia 10.4, dizeli kwa asilimia 2.9 na petrol kwa asilimia 2.8.

Akizungumzia mabadiliko ya bei kati ya mwezi Agosti na Septemba 2016 fahirisi za bei zimepungua hadi 103.o5 mwezi Septemba 2016 kutoka 103.28 mwezi Agosti 2016.

Alisema kupungua kwa fahirisi za bei kumechangiwa na kupungua kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula.

Alitaja baadhi ya bidhaa zilizochangia kupungua kwa fahirisi ni pamoja na mchele kwa asilimia 2.6, unga wa mahindi kwa asilimia 1.0, dagaa kwa asilimia 3.0 na mbogamboga kwa asilimia 4.3.

Alisema kwa upande mwingine baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kupungua kwa mfumuko wa bei ni pamoja na dizeli kwa asilimia 2.9, petroli kwa asilimia 2.8 na mafuta ya taa kwa asilimia 2.9

Akizungumzia thamani ya shilingi ya Tanzania kwa mwezi Septemba 2016 kutoka mwezi Desemba 2015 alisema uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia sh.97 na senti 04 mwezi Septemba 2016 kutoka mwezi Desemba 2015 ikilinganishwa na shilingi 96 na senti 83 ilivyokuwa mwezi Agosti 2016.

Kwesigabo akizungumzia mfumuko wa bei kwa bidhaa ya nchi za Afrika Mashariki nchini Kenya mfumuko wa bei wa mwezi Septemba 2016 umeongezeka kidogo hadi asilimia 6.34 kutoka asilimia 6.26 mwezi Agosti 2016.

Alisema nchini Uganda mfumuko wa bei wa mwezi Septemba 2016 umepungua hadi asilimia 4.2 kutoka asilimia 4.8 mwezi Agosti 2016.

(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

MAKAMU WA RAIS AZINDUA KAMPENI ENDELEVU YA FAHARI YA TANZANIA NA TUZO KWA BIDHAA 50 ZA KITANZANIA


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye hafla ya uzinduzi wa kampeni endelevu ya Fahari Tanzania, iliyoambatana na utoaji wa Tuzo kwa Bidhaa 50 bora za Kitanzania zilizofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Viwanda,Bisahara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akihutubia kwenye uzinduzi wa kampeni endelevu ya Fahari Tanzania, iliyoambatana na utoaji wa Tuzo kwa Bidhaa 50 bora za Kitanzania.

Meneja wa kampeni ya Fahari ya Tanzania Bw. Emmanuel Nnko akizungumza kwenye uzinduzi wa Kampeni hizo ambapo alifafanua umuhimu wa kununua bidhaa za Tanzania.

Picha ya Tuzo 50

Vijana wa Kimaasai wakionyesha umahiri wao wa kuimba na kucheza kwa kuruka wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Fahari ya Tanzania kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

NAIBU MAWAZIRI WA OFISI YA WAZIRI MKUU WATEMBELEA BANDA LA MAONESHO LA ELIMU YA MPIGA KURA


na1

Afisa Habari wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Margareth Chambiri (kulia) akiwakaribisha kwenye banda la Maonesho la NEC, Naibu Mawaziri Mhe. Anthony Mavunde Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Ajira na Vijana na Mhe. Abdallah Possi (Mwenye Kofia) Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi,Vijana, Ajira na Walemavu wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Vijana na Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Wilayani Bariadi –Simiyu. Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inaendelea na program endelevu za kutoa elimu ya mpiga kura kote nchini.

na2

Naibu Mawaziri Mhe. Anthony Mavunde Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Ajira na Vijana na Mhe. Abdallah Possi (Mwenye Kofia) Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi,Vijana, Ajira na Walemavu wakipata ufafanuzi kutoka kwa Maafisa wa NEC kuhusu utendaji wa Mashine za BVR katika uchukuaji na uhifadhi wa taarifa za Wapiga Kura leo kwenye maadhimisho ya Wiki ya Vijana na Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Wilayani Bariadi –Simiyu.

na3

Afisa TEHAMA wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Sanif Khalifan akitoa ufafanuzi kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bariadi kuhusu taratibu za uchaguzi na hatua za uandikishaji wa wapiga kura kupitia TEHAMA leo mjini Baridi wakati wa Tume hiyo ilipokuwa ikitoa Elimu kwa Mpiga Kura kuhusu masuala mbalimbali.

na4

Baadhi ya Askari wa JKT wakipata ufafanuzi kuhusu masula mbalimbali walipotembelea Banda la Maonesho ya Elimu ya Mpiga Kura wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Vijana wilayani Bariadi, mkoani Simiyu.

na5

Baadhi ya Askari wa JKT wakipata ufafanuzi kuhusu masula mbalimbali walipotembelea Banda la Maonesho ya Elimu ya Mpiga Kura wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Vijana wilayani Bariadi, mkoani Simiyu.

na6

Naibu Mawaziri Mhe. Anthony Mavunde Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Ajira na Vijana na Mhe. Abdallah Possi (Mwenye Kofia) Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi,Vijana, Ajira na Walemavu wakifurahia jambo mara baada ya kupata ufafanuzi kutoka kwa Maafisa wa NEC kuhusu utendaji wa Mashine za BVR katika uchukuaji na uhifadhi wa taarifa za Wapiga Kura leo kwenye maadhimisho ya Wiki ya Vijana na Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Wilayani Bariadi –Simiyu.

na7

Mkazi wa Bariadi akipata ufafanuzi kuhusu karatasi zenye majina ya wagombea zinazotumika kupigia kura alipotembelea banda la maonesho na Elimu ya mpiga kura la NEC leo wilayani Bariadi mkoani Simiyu.

Picha na Aron Msigwa – NEC. (P.T)

WAZIRI WA FEDHA DK. PHILIP MPANGO NA UJUMBE WAKE WAENDELEA NA VIKAO VYAO NA WAKUU WA BENKI YA DUNIA


jem1

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia kanda ya Afrika Louis Rene Peter Larose (hayupo Pichani), makao Makuu ya Benki hiyo Jijini Washington DC, Marekani, kulia kwake ni Katibu Mkuu w Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James.

(Picha zote na Wizara ya Fedha na Mipango)

jem2

Ujumbe wa wataalamu wa Fedha, Sera na Uchumi kutoka Tanzania wakifuatilia kwa makini Mazungumzo ya Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika, Louis Rene Peter Larose (hawapo Pichani), Makao Makuu ya Benki hiyo Jijini Washington DC, Marekani, ambapo unafanyika Mkutano wa Mwaka wa Benki hiyo ambayo Tanzania ni Mwanachama, wa kwanza kushoto ni Kamishna wa Sera Augustine Ollal, Kamishna wa Bajeti John Cheyo na Kaimu Kamishna wa Fedha za Nje Mamelta Mutagwaba.

jem3

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika, Louis Rene Peter Larose walipokutana ofisini kwake Jijini Washington DC, Marekani, ambapo wamezungumzia masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya Tanzania na namna Benki hiyo ilivyojipanga kuhakikisha kuwa inaiwezesha Tanzania kufikia ndoto yake ya kuwa nchi yenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025

jem4

Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, wakishikana mikono kuonesha umoja na mshikamano mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo kati ya ujumbe huo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika, Louis Rene Peter Larose, Jijini Washington DC nchini Marekani, ambako ujumbe huo unahudhuria Mkutano wa Mwaka wa Benki hiyo.

jem5

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Katikati, Akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia kanda ya Afrika mara baada ya viongozi hao kumaliza mazungumzo yaliyogusia Nyanja mbalimbali za kijamii na kiuchumi, Jijini Washington DC, nchini Marekani, ambapo Tanzania inashiriki Mkutano wa Mwaka wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani-IMF.

jem6

Baadhi ya wajumbe wa Tanzania wanaoshiriki Mkutano wa Mwaka wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani-IMF, baada ya kumalizika kwa kikao kati ya ujumbe huo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika, Louis Rene Peter Larose, wakiwa nje ya Majengo ya Benki hiyo Jijini Washington DC nchini Marekani. Wa kwanza kushoto ni Kaimu Kamishna wa Fedha za nje, Wizara ya Fedha na Mipango, Mamelta Mutagwaba, Kamishna wa Bajeti, John Cheyo, Kamisha wa Madini James Andilile na Kamishna wa Sera Augustine Ollal.

jem7

Wajumbe kutoka takribani nchi 180 duniani kote, wanachama wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani-IMF, wakiwa katika Siku ya kwanza ya Mkutano wa Mwaka wa Taasisi hizo Jijini Washington DC nchini Marekani, Tanzania inawakilishwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt, Philip Mpango ambaye ameongoza ujumbe wa wataalamu wa Fedha na Uchumi katika mkutano huo.

jem8

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James (wa kwanza kushoto), Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (wa pili), Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania BOT, Prof Benno Ndulu (wa tatu kutoka Kushoto), Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania BoT Dkt. Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, Kamisha Msaidizi wa Nishati, Wizara ya Nishati na Madini, James Andilile, wakiangalia ripoti iliyotolewa na timu ya wataalamu wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani-IMF, kuhusu miradi mbalimbali inayotekelezwa nchini Tanzania kwa ufadhili na mkopo kutoka Taasisi hizo.

jem9

Ujumbe wa Tanzania na badhi ya  viongozi wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani-IMF wakikatisha Mitaa ya Jiji la Washington DC nchini Marekani kuwahi vikao mbalimbali vinavyoendeshwa na Taasisi hizo kabla ya kufikiwa kwa kilele cha Mkutano wa Mwaka wa Taasisi hizo Oktoba 9 mwaka huu. Chanzo:mjengwablog

MAADHIMISHO YA SIKU YA MAKAZI DUNIANI YAENDELEA JIJINI DAR ES SALAAM


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akisikiliza maelezo kutoka kwa mwakilishi wa Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) wakati wa maadhimisho ya siku ya makazi duniani jana Jijini Dar es Salaam.

kuv1

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu siku ya makazi duniani jana Jijini Dar es Salaam.

kuv2

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akakiangalia bango la Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) wakati wa maadhimisho ya siku ya makazi duniani jana Jijini Dar es Salaam.

Picha na: Jonas Kamaleki, MAELEZO