MISS TZ AFARIKI GHAFLA


Stori: Imelda Mtema

KWELI kifo hakina huruma jamani! Mshiriki wa Miss Tanzania 2013 akitokea Miss Ilala, Martha Gewe, mkazi wa Tabata Segerea, Dar amefariki dunia baada ya kuugua ghafla, Ijumaa Wikienda linakupa zaidi.

Martha amekutwa na mauti katika Hospitali ya Mkoa wa Ilala, Amana jijini Dar es Salaam, Ijumaa iliyopita ambako alikimbizwa baada ya kuugua na madaktari walibaini kwamba, malaria ilipanda kichwani.

Marafiki wa aliyekuwa mshiriki wa Miss Tanzania 2013 akitokea Miss Ilala, Martha Gewe wakiwa na…

Advertisements

SINEMA YA SITTI MTEMVU YA ENDELEA………


Mshindi wa Miss Tanzania 2014 Sitti Mtemvu, kwa hiari yake mwenyewe bila kulazimishwa na mtu ameamua kulivua rasmi taji hilo la urembo.

Akiongea na EATV mratibu wa shindano hilo Hashimu Lundenga amesema kuwa Sitti Mtemvu ameamua kwa maamuzi yake binafsi na sio wao kama kamati ya Miss Tanzania.

“Sababu kubwa ya Sitti kulivua taji hilo ni baada ya kuchoshwwa na maneno mengi yaliyozushwa juu yake, maana pia aliitwa na RITA kwaajili ya uchunguzi zaidi hivyo ameona mambo yanazidi kuzushwa mengi hivyo ameamua kulivua taji hilo”. Amesema Hashimu Lundenga.VICTOR SIMON/mjengwablog