Kutoka Gazeti la Mwananchi LEO:Wakati vyama vya upinzani vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), vikitafakari jina la mgombea urais, Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila tayari anaye mtu anayefaa; anamtaka Dk Willbrod Slaa.


Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbrod Slaa
—–
Wakati vyama vya upinzani vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), vikitafakari jina la mgombea urais, Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila tayari anaye mtu anayefaa; anamtaka Dk Willbrod Slaa.
Kwa maoni yake, si kwamba viongozi au wanachama wa vyama vingine vinavyounda Ukawa hawana sifa za kuwania nafasi hiyo ya juu katika siasa nchini, bali Dk Slaa ana sifa ya ziada; ana mvuto.
Katika mahojiano maalumu na gazeti hili, Kafulila, ambaye alikuwa mwanachama wa Chadema kabla ya kuondoka na kujiunga na NCCR-Mageuzi mwaka 2010, alisema Dk Slaa ana nafasi kubwa kuliko viongozi wa vyama vingine vya siasa vinavyounda umoja huo ambavyo ni Chadema, NCCR, NLD na CUF kwa sababu katibu huyo mkuu wa Chadema anakubalika zaidi katika jamii kulinganisha na wengine.
read more

Urais CCM kazi pevu


Dar es Salaam. Wakati joto la urais ndani ya CCM likiendelea kupamba moto, watu watakaoingia kundi la tano bora ambalo litapitishwa na Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC), wamefahamika.
Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa.PICHA|MAKTABA

Uchambuzi uliofanywa na makada mbalimbali wa chama hicho unaonyesha kuwa makundi hayo ambayo yatatoa wagombea mmoja, ni kundi la wagombea vijana, kundi la kifo, kundi la waziri mkuu aliyepo madarakani, wagombea wanawake na kundi la wagombea kutoka Zanzibar.

Kila kundi katika hayo litatoa mgombea mmoja ambaye jina lake litapelekwa kupitishwa kwenye mkutano wa NEC kupitishwa kabla ya kupigiwa kura kwenye Mkutano Mkuu wa CCM (CC).
Kundi la Vijana
Uchambuzi unaonyesha kwa vyovyote vile CCM lazima iteue jina la mgombea kijana hata kama watakuwa hawamtaki ili kuonyesha kuwa chama hicho kimekomaa na kinawapa moyo vijana kuwania nafasi za uongozi.
Wanasiasa vijana wa CCM ambao tayari wametangaza nia ya kuwania nafasi ya urais ni Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, January Makamba na Mbunge wa Nzega, Dk Hamis Kigwangalla.
Wengine ambao wamekuwa wakitajwa katika kundi hilo ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, Mbunge wa Songea Mjini, Dk Emmanuel Nchimbi, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja.

NIHF KUFANYA KAMPENI YA SIKU 60 KUHAMASISHA WANANCHI KUJIUNGA NA MFUKO HUO WA BIMA YA AFYA


1

Kaimu Mkurugenzi mkuu na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Beatus Chijumba akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye makao makuu ya shirika hilo wakati alipotangaza kampeni ya siku 60 kwa ajili ya kuhamasisha wananchi kujiuga na Mfuko wa Bima ya Afya katika Halmashauri zipatazo 54 nchini Katikati ni Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti na mwisho ni Ali Othman Mkuu wa kitengo cha Mifumo ya Mawasiliano.

2   …

1

Kaimu Mkurugenzi mkuu na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Beatus Chijumba akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye makao makuu ya shirika hilo wakati alipotangaza kampeni ya siku 60 kwa ajili ya kuhamasisha wananchi kujiuga na Mfuko wa Bima ya Afya katika Halmashauri zipatazo 54 nchini Katikati ni Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti na mwisho ni Ali Othman Mkuu wa kitengo cha Mifumo ya Mawasiliano.

2  

Kaimu Mkurugenzi mkuu na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Beatus Chijumba akizungumza na waandishi wa habari leo katika makao makuu ya NHIF Bendera Tatu jijini Dar es salaam kuhusu kampeni ya kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko huo, Kutoka kulia ni Ali Othman Mkuu wa kitengo cha Mifumo ya Mawasiliano, Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti na kutoka mkushoto ni Dr Frank Lekei (Mkurugenzi wa Tiba na masuala ya kiufundi NHIF).

3

Athman Rehani Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) akifafanua jambo wakati wa mkutano huo , kutoka kulia ni Ali Othman Mkuu wa kitengo cha Mifumo ya Mawasiliano, Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti na Kaimu Mkurugenzi mkuu na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Beatus Chijumba.

4

Kutoka kulia ni Meneja wa CHF Bw. Costantine Makala, Ali Othman Mkuu wa kitengo cha Mifumo ya Mawasiliano,Mkurugenzi wa Uendeshaji (NHIF),Eugen Mikongoti, Kaimu Mkurugenzi mkuu na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Beatus Chijumba, Athman Rehani Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), Mkurugenzi wa masoko na Utafiti NHIF,Raphael Mwamoto na Dr Frank Lekei (Mkurugenzi wa Tiba na masuala ya kiufundi NHIF).Chanzo:www.globalpublishers.info