MAKAMU WA RAIS DKT BILALI ABARIKI KANISA LA KIASKOFU JIMBO LA KONDOA MKOA WA DODOMA


kiiiiiiiiiiiiiii2

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilai akizungumza na waumini wa Dini ya kikiristo wakati washerehe za kutabaruku Kuweka wakfu, kanisa la Kiaskofu la Roho mtakatifu jimbo la kondoa  jana 4/12/2014 iliofanyika Wilaya ya Kondoa Mkoa wa Dodoma.

kiiiiiiiiiiiiiiiiii4

Makamu wa Rais wa jamhuri ya Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal akiwa katika picha ya pamoja na Maaskofu na mashekh wa Wilaya ya kondoa mkoa wa Dodoma Mara baada ya kuzungumza na waumini wa Dini ya kikiristo jana tarehe 4/12/2014.

kiiiiiiiiiiiiiiiiiii5

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal akiagana na Askofu mkuu wa Kanisa katoliki Tanzania Kardinali Polcarp Pengo wakati wa Sherehe za Kutabaruku kuweka wakfu ,kubariki kanisa lakiaskofu la roho Mtakatifu la jimbo la kondoa iliofanyika wilayani kondoa mkoa wa Dodoma juzi tarehe 4/12/2014                                                                                     

kiiiiiiiiiiiiiiiiii3

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt Mohammed Gharib Bilal akipongezwa na Askofu wa kanisa katoliki Jimbo la kondoa Baba  Bernadin Mfumbusa mara baada ya kuzungumza na waumini wa kanisa la kiaskofu la Roho mtakatifu jimbo la Kondoa juzi 4/12/2014 iliofanyika walaya ya kondoa mkoa wa Dodoma.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA MAADHIMISHO YA MIAKA 20 YA MAHAKAMA YA MAUAJI YA KIMBARI YA RWANDA ICTR JIJINI ARUSHA.


unnamedMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia kwenye Maadhimisho ya miaka 20 ya Mahakama ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR), ulioanza leo Novemba 8, 2014 kwenye Ukumbi wa AICC Jijini Arusha. Picha na OMR

unnamed1Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia kwenye Maadhimisho ya miaka 20 ya Mahakama ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR), ulioanza leo Novemba 8, 2014 kwenye Ukumbi wa AICC Jijini Arusha. Picha na OMR

unnamed2Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitazama baadhi ya picha za kumbukumbu za Mahakama ya Kimbari zilizo katika ukumbi huo wakati akiondoka baada ya kufungua rasmi Mkutano wa Maadhimisho ya miaka 20 ya Mahakama ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda ICTR, ulioanza leo Novemba 8, 2014 kwenye Ukumbi wa AICC Jijini Arusha. Picha na OMR

unnamed3Baadhi ya washiriki waliohudhuria mkutano huo wakimsikiliza makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akihutubia. Picha na OMRunnamed4Baadhi ya washiriki waliohudhuria mkutano huo wakimsikiliza makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akihutubia. Picha na OMRunnamed5Baadhi ya washiriki waliohudhuria mkutano huo wakimsikiliza makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akihutubia. Picha na OMRunnamed7Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya washiriki wa mkutano huo wa maadhimisho ya miaka 20 ya Mahakama ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR), ulioanza leo Novemba 8, 2014 kwenye Ukumbi wa AICC Jijini Arusha. Picha na OMR

Ikulu yaguswa kwenye ujangili


 

Ikulu yaguswa kwenye ujangili MIEZI tisa tangu mwandishi wa Uingereza, Martin Fletcher wa gazeti la The Mail on Sunday, kuchapisha makala akidai Serikali ya Tanzania inabariki ujangili wa meno ya tembo, gazeti la New York Times la Marekani, nalo limechapisha habari ikihusisha ndege ya Rais wa China, Xi Jinjing kuhusika kubeba pembe za ndovu alipokuwa Tanzania. Katika toleo la Novemba 5 mwaka huu, mwandishi wa New York Times, Dan Levin alinukuu ripoti ya Shirika la ujasusi la mazingira lenye makao yake mjini London, akisema kwamba China ilinunua maelfu ya kilo za pembe za ndovu na kuzitorosha kwa kutumia ndege ya Rais huyo wakati alipozuru Tanzania Machi 2013. Machi 2013, Rais wa China, Xi Jinping, aliwasili Tanzania katika ziara yake ya kwanza kwenye Bara la Afrika akiwa ni kiongozi wa nchi ambayo ni ya pili kiuchumi duniani. Katika ziara hiyo aliambatana na ujumbe wa maofisa wa serikali na wafanyabiashara ambao walikuwa maalum kwa ajili ya kukuza mahusiano baina ya nchi hizo mbili. Kwa mujibu wa mwandishi huyo, ripoti mpya ya shirika la ujasusi la mazingira inaonesha kuwa ujumbe wa Rais Jinping ulitumia ziara hiyo kama nafasi ya kufanya biashara haramu ya pembe za ndovu kwa kupandisha bei yake mara mbili kufikia dola 70,000 za Marekani kwa kilo, au dola 31,800 kwa kila paundi. Kwamba, wiki mbili kabla ya Rais Jinping kuwasili, wanunuzi wa Kichina walikwenda kwenye maeneo mbalimbali yanayojihusisha na biashara hiyo na kununua maelfu ya pembe hizo ambazo baadaye zilipelekwa China kwa kutumia mabegi ya wanadiplomasia kwenye ndege ya Rais. “Rais wenu alikuwa hapa,” ananukuliwa Suleiman Mochiwa, Mtanzania anayedaiwa kujihusisha na biashara hiyo haramu ya pembe za ndovu, akimaanisha Rais Jinping. “Akiwa hapa, kilo nyingi zimekwenda nje kwenye ndege pasipo ulinzi. Walinunua kutoka kwetu.” Ripoti hiyo inaitaja Tanzania kama chanzo kikuu duniani kwa uharamia wa pembe za ndovu na kwamba, China imekuwa mnunuzi mkubwa wa bidhaa hizo kimagendo. Read more »

RAIS PROFESA JAKAYA KIKWETE ATEUA WAKUU WA MIKOA WAPYA NA KUWAHAMISHA VITUO VYA KAZI WENGINE


 

D92A7608

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amefanya uteuzi wa wakuu wapya wanne wa Mikoa, amewahamisha wengine sita na ameamua kuwa wengine watatu watapangiwa kazi nyingine.

Taarifa iliyotolewa mjini Dodoma jioni ya leo, Jumatano, Novemba 5, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue inasema kuwa, Wakuu wapya wa Mikoa ni Bi. Halima Omari Dendego ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Dkt. Ibrahim Hamisi Msengi ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Bi. Amina Juma Masenza ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa na Bwana John Mongella Vianney ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera.

Taarifa inasema kuwa kabla ya uteuzi wake Bi. Dendego alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Dkt. Msengi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Bi. Masenza alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilemela na Bwana Mongella alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha.

Taarifa hiyo inasema kuwa Wakuu hao wapya wa Mikoa wataapishwa kesho, Alhamisi, Novemba 6, 2014 saa saba mchana, Ikulu, Dar es Salaam.

Aidha, taarifa hiyo imesema kuwa Wakuu wa Mikoa ambao watapangiwa kazi nyingine ni Kanali (Mst) Fabian Massawe wa Kagera, Dkt. Christine Ishengoma wa Iringa na Kanali Joseph Simbakalia wa Mtwara.

Wakuu wa Mikoa ambao wamehamishwa vituo vya kazi ni Bwana Magesa S. Mulongo ambaye anakwenda Mkoa wa Mwanza kutoka Arusha, Dkt. Rehema Nchimbi ambaye anakwenda Mkoa wa Njombe kutoka Dodoma, Bwana Ludovick John Mwananzila anakwenda Tabora kutoka Lindi, Kepteni (Mst) Anseri Msangi anayekwenda Mkoa wa Mara kutoka Njombe na Mhandisi Everist Ndikilo ambaye anakwenda Arusha kutoka Mwanza.

Wengine waliohamishwa ni Luteni (Mst) Chiku A.S. Galawa ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kutoka Tanga, Dkt. Rajab Rutengwe ambaye anakwenda Mkoa wa Tanga kutoka Katavi, Bi Fatma Mwasa ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita kutoka Tabora na Bwana Magalula S. Magalula ambaye anahamishiwa Lindi kutoka Geita.

Taarifa hiyo imesema kuwa Wakuu wa Mikoa ya Dar es Salaam, Kigoma, Kilimanjaro, Manyara, Mbeya,Morogoro, Pwani, Rukwa, Shinyanga, Ruvuma, Singida na Simiyu watabakia kwenye vituo vyao vya sasa.

Aidha, Rais Kikwete amefanya uteuzi wa Wakuu wapya wa Wilaya, kuhamisha baadhi yao na kutengua uteuzi wa baadhi.

Taarifa kamili itatolewa na Waziri Mkuu baada ya kuwa wamepangiwa vituo vya kazi.

Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
05 Novemba,2014