MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA MAADHIMISHO YA MIAKA 20 YA MAHAKAMA YA MAUAJI YA KIMBARI YA RWANDA ICTR JIJINI ARUSHA.


unnamedMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia kwenye Maadhimisho ya miaka 20 ya Mahakama ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR), ulioanza leo Novemba 8, 2014 kwenye Ukumbi wa AICC Jijini Arusha. Picha na OMR

unnamed1Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia kwenye Maadhimisho ya miaka 20 ya Mahakama ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR), ulioanza leo Novemba 8, 2014 kwenye Ukumbi wa AICC Jijini Arusha. Picha na OMR

unnamed2Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitazama baadhi ya picha za kumbukumbu za Mahakama ya Kimbari zilizo katika ukumbi huo wakati akiondoka baada ya kufungua rasmi Mkutano wa Maadhimisho ya miaka 20 ya Mahakama ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda ICTR, ulioanza leo Novemba 8, 2014 kwenye Ukumbi wa AICC Jijini Arusha. Picha na OMR

unnamed3Baadhi ya washiriki waliohudhuria mkutano huo wakimsikiliza makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akihutubia. Picha na OMRunnamed4Baadhi ya washiriki waliohudhuria mkutano huo wakimsikiliza makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akihutubia. Picha na OMRunnamed5Baadhi ya washiriki waliohudhuria mkutano huo wakimsikiliza makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akihutubia. Picha na OMRunnamed7Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya washiriki wa mkutano huo wa maadhimisho ya miaka 20 ya Mahakama ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR), ulioanza leo Novemba 8, 2014 kwenye Ukumbi wa AICC Jijini Arusha. Picha na OMR

Advertisements

Ikulu yaguswa kwenye ujangili


 

Ikulu yaguswa kwenye ujangili MIEZI tisa tangu mwandishi wa Uingereza, Martin Fletcher wa gazeti la The Mail on Sunday, kuchapisha makala akidai Serikali ya Tanzania inabariki ujangili wa meno ya tembo, gazeti la New York Times la Marekani, nalo limechapisha habari ikihusisha ndege ya Rais wa China, Xi Jinjing kuhusika kubeba pembe za ndovu alipokuwa Tanzania. Katika toleo la Novemba 5 mwaka huu, mwandishi wa New York Times, Dan Levin alinukuu ripoti ya Shirika la ujasusi la mazingira lenye makao yake mjini London, akisema kwamba China ilinunua maelfu ya kilo za pembe za ndovu na kuzitorosha kwa kutumia ndege ya Rais huyo wakati alipozuru Tanzania Machi 2013. Machi 2013, Rais wa China, Xi Jinping, aliwasili Tanzania katika ziara yake ya kwanza kwenye Bara la Afrika akiwa ni kiongozi wa nchi ambayo ni ya pili kiuchumi duniani. Katika ziara hiyo aliambatana na ujumbe wa maofisa wa serikali na wafanyabiashara ambao walikuwa maalum kwa ajili ya kukuza mahusiano baina ya nchi hizo mbili. Kwa mujibu wa mwandishi huyo, ripoti mpya ya shirika la ujasusi la mazingira inaonesha kuwa ujumbe wa Rais Jinping ulitumia ziara hiyo kama nafasi ya kufanya biashara haramu ya pembe za ndovu kwa kupandisha bei yake mara mbili kufikia dola 70,000 za Marekani kwa kilo, au dola 31,800 kwa kila paundi. Kwamba, wiki mbili kabla ya Rais Jinping kuwasili, wanunuzi wa Kichina walikwenda kwenye maeneo mbalimbali yanayojihusisha na biashara hiyo na kununua maelfu ya pembe hizo ambazo baadaye zilipelekwa China kwa kutumia mabegi ya wanadiplomasia kwenye ndege ya Rais. “Rais wenu alikuwa hapa,” ananukuliwa Suleiman Mochiwa, Mtanzania anayedaiwa kujihusisha na biashara hiyo haramu ya pembe za ndovu, akimaanisha Rais Jinping. “Akiwa hapa, kilo nyingi zimekwenda nje kwenye ndege pasipo ulinzi. Walinunua kutoka kwetu.” Ripoti hiyo inaitaja Tanzania kama chanzo kikuu duniani kwa uharamia wa pembe za ndovu na kwamba, China imekuwa mnunuzi mkubwa wa bidhaa hizo kimagendo. Read more »