Shibuda Awataka Wanasiasa Kuepukana Na Mdudu Shetani Wa Kujinufaisha Wenyewe


 

 
 
Mo Blog: Shibuda umekuwa mwasiasa kwa siku nyingi nini rai yako kwa viongozi wenzio wa kiasiasa.?
Shibuda: Napenda kutoa rai kwa vyama na viongozi wa kisiasa ambavyo viko karibu 21 hapa Tanzania, la kwanza kila chama kijifanyie tathmini, kinawajibika vipi kutekeleza mipango ya kuendeleza amani na utulivu katika hii nchi.
Vinatekeleza mipango gani? Na kila chama kifanye tathmini kijiuze mambo gani ambayo ni makosa kwa ustawi na maendeleo ya nchi yetu inaoongozwa na kulindwa na tabia, mila na desturi za mtanzania.
Vyama vya siasa viwe na wito unaoitwa ‘kwa maslahi ya umma’ na viongozi pia watekeleze wito unaoitwa kwa maslahi ya umma.
Mo Blog: Kwani una shaka na baadhi ya vyama?
Shibuda:Vyama ambavyo vina mdudu shetani anayeitwa ibilisi wa kujenga tafrani, migongano, misuguano au vyama vinavyoitwa ‘chama kampuni’ kwa maslahi binafsi, havistahiki kuwa sehemu moja wapo ya mbegu ya kuzalisha amani.
Hivyo watanzania tutafakari, tusemezane, tutazame viwango vya kila chama, katika vyama 21 kwamba je? Tija ya kila chama ni kwa kujenga ustawi na maendeleokwa jamii? Ili mwaka kesho tusherehekee tena siku ya amani duniani.

Short Course Announcement


Reactions:   
 
 

                        UNIVERSITY OF DODOMA

DEPARTMENT OF STATISTICS SHORT COURSE ANNOUNCEMENT ON DATA PROCESSING AND ANALYSIS  (To be conducted in Dar es Salaam)

The Department of Statistics, School of Mathematical Sciences is announcing a short course on “DATA PROCESSING AND ANALYSIS” that will be conducted on September 27 and 28 from 14: 00 – 18:00; September 29 – 30 from 09:30 – 17:00.

The training will cover: overview of data; data management using SPSS; data cleaning (missing values, outliers and normality); descriptive data analysis and interpretation. Participants are required to come with their laptops.

Objective of the training

The objective of the training is to improve skills of researchers into different statistical techniques applied during data processing and analysis and hence practical interpretation of the result.
Target Group: Any interested person.
Participation Fee: Tshs 250, 000/= (The amount paid will cover tuition fee, training materials, and certificate of attendance only).
Mode of payment: All payments should be done through; Account Name: College of Natural and Mathematical Sciences; Account no: 0150221567000 – CRDB
Venue: National Institute of Transport (NIT) Payment deadline: September 21, 2012.

Mode of Registration: Send an email indicating your name after making payment using contact below. Come with bank deposit slip.
Contact person:
Josephat Peter
Training Coordinator
Mobiles: 0787288998 or 0718453773
E-mail: statistics.data.udom@gmail.com

Pinda Akutana Na Rais Wa TBEA …


 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Rais wa Masuala ya Biashara za Kimataifa wa Kampuni ya TBEA ya China,Bw. Wang Pinshan kabla ya mazungumzo yao, Ofisini kwake jijini Dar es salaam September 4, 2012. Kulia ni Makamu wa Rais wa Kampuni hiyo wa Masuala ya Biashara, Bw. Shi Qiwen na wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo, Bw. Andy.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Rais wa Masuala ya Biashara za Kimataifa wa Kampuni ya TBEA ya China, Bw. Wang Pinshan kabla ya mazungumzo yao, Ofisini kwake jijini Dar es salaam September 4, 2012. Kulia ni  Makamu wa Rais wa Kampuni hiyo wa Masuala ya Biashara, Bw. Shi Qiwen na wapili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo, Bw. Andy.
                  
                          Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

TAARIFA YA JUKWAA LA WAHARIRI (TEF) KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU KUUAWA KWA MWANDISHI DAUDI MWANGOSI


Marehemu Daudi Mwangosi.

UTANGULIZI:

1. Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), limepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, mkoani Iringa, Daudi Mwangosi.
2. Mwangosi ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Iringa (IPC), aliuawa akiwa kazini jana, Septemba 2, 2012, wakati polisi walipokuwa wakiwadhibiti wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
3. Tukio hili linaiingiza Tanzania katika historia mbaya ya ukiukwaji na ukandamizwaji wa uhuru wa habari, kwani ni kwa mara ya kwanza tunashuhudia mwandishi wa habari AKIUAWA WAKATI AKITEKELEZA MAJUKUMU YAKE YA KIHABARI.
4. Taarifa za awali zinaonyesha kuwa Mwangosi kabla ya kufikwa na mauti saa 9.30 alasiri katika kijiji cha Nyololo, Mufindi, alizingirwa na kushambuliwa na polisi waliokuwa katika eneo la tukio. Na hata alipopiga kelele za kuomba msaada, hakusikilizwa na matokeo yake aliuawa na kitu kinachodhaniwa kuwa ni bomu.
5. Kwa kushirikiana na Baraza la Habari Tanzania, TEF tumechukua hatua za haraka za kuunda timu ya uchunguzi wa suala hilo, ambayo itakwenda mkoani Iringa mapema kadri itakavyowezekana, ili kubaini ukweli wa tukio hilo. Lengo la uchunguzi huo ni kuweka kumbukumbu sahihi (documentation) ya tukio hilo la aina yake katika historia ya nchi yetu.
6. Matokeo ya uchunguzi huo pamoja na mwingine unaofanywa na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), ndiyo yatakayotoa mwelekeo wa hatua ambazo TEF itachukua dhidi ya Jeshi la Polisi katika siku chache zijazo.
MTIZAMO NA MSIMAMO WA TEF
Kwa kuzingatia taarifa kutoka Iringa na zile za vyombo vya habari vya jana (Jumapili, Septemba 02, 2012) na leo (Jumatatu, Septemba 03, 2012), TEF ina mtizamo na msimamo kama ifuatavyo:
1. Kwanza tunalaani vikali tukio la kupigwa, kisha kuuwawa kwa mwandishi Daudi Mwangosi ambalo limeigusa tasnia ya habari kwamba sasa pengine waandishi wa habari ni malengo “target ya polisi” wanapokuwa kwenye kazi zao.

2. Ieleweke wazi kwamba matukio haya siyo yanaondoa imani ya waandishi wa habari kwa jeshi la polisi tu, bali yanaweza kuwa chanzo cha uhasama na ufa mkubwa ambao utawanyima wananchi nafasi ya kutumikiwa na pande mbili ambazo zinategemeana.

3. Kwa matukio ya aina hii, tunadhani wakati mwafaka kwa uongozi wa Jeshi la Polisi nchini kuwajibika, kuazia kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa na uongozi wa Makao Mkuu, akiwamo Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Saidi Mwema.

4. Tunasema hivi kwani kuna kila dalili kwamba polisi wanahusika kwa namna moja au nyingine na tukio au/na matukio yaliyosababisha kifo cha Mwangosi, kwani kitendo cha kumzingira tu na kumshambulia kinathibitisha kwamba hawakuwa na nia njema hata kidogo dhidi ya mwandishi huyu.

5. Taarifa ambazo TEF tunazo, pia zinadai kwamba kulikuwa na mpango wa polisi wa “kuwashughulikia waandishi wa habari watatu” (Mwangosi) akiwa mmojawapo na hilo lilionekana likitekelezwa kwa polisi kumshambulia mwandishi huyo, baadaye alipoteza maisha katika mazingira ya kutatanisha.

6. Hili linatiliwa nguvu na tukio jingine la polisi kumpiga na kumjeruhi mwandishi mwingine, Godfrey Mushi ambaye ni mwakilishi wa gazeti la Nipashe mkoani Iringa. Mwandishi wa tatu ambaye hadi tunapoandika taarifa hiyo yumo katika mpango wa ‘kushughulikiwa na polisi’ ni Francis Godwin ambaye ni mwandishi wa habari wa kujitegemea.

7. Vitendo vya aina hii havivumiliki na havipaswi kuachwa kuendelea kwani ni hatari kwa ustawi wa demokrasia na uhuru wa habari nchini. Hatuwezi kuendelea katika mazingira ambayo polisi wanageuka kuwa chombo cha mauaji ya raia badala ya kuwa walinzi wa raia.

8. Kwa maana hiyo, mbali na uchunguzi ambao utafanywa na polisi, tunatoa wito kwa Serikali kuunda chombo huru, ambacho kitabaini ukweli, na matokeo yake yatangazwe kwa umma, huku wahusika wa aibu hiyo wakichukuliwa hatua za kisheria. Tunasema hivyo, tukifahamu kwamba tayari kuna jitihada za kuficha ukweli na kueneza propaganda za uongo kuhusu tukio zima.

9. Mwenendo wa aina hii wa chombo cha dola kuamua kutumia silaha kuua na baadaye kupanga mbinu chafu za kuficha ukweli ni hatari kwa Taifa, na unaiweka demokraisia ya nchi yetu njia panda, huku tukielekea katika hatari ya Taifa kutumbukia katika uovu.
IMETOLEWA NA:
NEVILLE MEENA,
KATIBU MKUU – JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA (TEF)
SEPTEMBA 3, 2012

 

Mhe.Sitta Ajibu Kombora La Dkt.Slaa


 

 
Nimesikitishwa na kauli za jazba na mwangwi wa kiwewe za Mhe Dr. W Slaa alipokuwa Iringa juzi hadi kuniita mnafiki, mwongo, mtu wa hatari n.k Hali hii inatia mashaka juu ya uwezo wa kiongozi huyo wa kisiasa kuhimili kukosolewa ambayo ni sifa muhimu ya maisha ya mwanasiasa yeyote hususani anapojinadi  kuwa anaweza kuchukua madaraka ya kuiongoza nchi.
Kauli zisizo na staha alizozitoa Dr Slaa dhidi yangu kama vile sifai hata uongozi wa kata zinadhihirisha mambo mawili:
-Dr Slaa ni dicteta. Hana uvumilivu. Ana hulka ya kujiskia kwamba mawazo yake hayapingwi.
-Ni mzushi asiyeogopa kusema na kupindisha mantiki ya jambo ili tu kushinda hoja. Iweje mtu aliyenibembeleza nigombee uraisi kupitia chama chake mwaka juzi leo aseme sifai kuongoza hata kata kwasababu tu nimetamka ukweli juu ya udhaifu wa chama chake cha siasa?
Niliyoyasema pale Karagwe majuzi katika uchambuzi wangu wa vyama vya siasa nchini ni kwamba CHADEMA wamekuwa hodari wa kukosoa na kuishambulia CCM na serikali zake lakini wanasau kuwa ili wawe mbadala kwa kuiongoza nchi hawana budi kurutubisha safu yao ya uongozi nawe na watu wakutosha kuweza kushika madaraka ya ngazi mbalimbali za uongozi wa Taifa. Kuukataa ukweli kwamba safu ya uongozi wa CHADEMA ni nyembamba ni kujidanganya tu.Kupita mikoani kutangaza kwamba matatizo yote ya wananchi yanatokana na CCM ni kazi rahisi na ina mvuto wake kisiasa lakini mwanasiasa makini hana budi kwenda mbele zaidi ya hapo. Hana budi kutuambia wapiga kura mipango ya chama chake inayoeleweka na inayotekelezeka na iliyo makini kukabiliana na changamoto mbalimbali za maendeleo ya nchi. Ahadi za alinacha za tiba bure, elimu bure bila kuonyesha vyanzo halisi vya mapato ni porojo tu. Kusema kwamba raslimali za nchi kama vile gesi asilia, madini, makaa ya mawe, utalii zinatosha kuondoa umaskini ni nadharia tupu ambayo uhalisia wake hauna budi kubainishwa kwa mikakati dhahiri na thabiti ya kiutawala (uendeshaji) inayoweza kuchuma utajiri huo kwa ufanisi, kwa uendelevu na kwa faida ya wengi 1. Kuhusu mwenyekiti Mh Mbowe – MB

Katika hotuba yangu sikukejeli uzoefu wa Mhe Mbowe, wala sijasema Mhe Mbowe ni mcheza disko. Niliuchambua wasifu wa viongozi wa CHADEMA na kutamka uzoefu  wa Mhe Mbowe katika vitega uchumi vya burudani hii siyo kudharau bali ni kutamka ukweli tu.Huwezi kuuelezea wasifu wa Mhe Mbowe bila kuelezea mchango wake mkubwa katika tasnia ya burudani.Mmoja wa maraisi maarufu wa marekani (USA)alikuwa ni mcheza sinema Ronald Reagan.Na hapa Tanzania tulikuwa na mzee R. Kawawa ambaye alianzia katika tasnia ya uigizaji, kwa hiyo Mhe Mbowe au Dr.W. Slaa anaweza akawa Rais wetu kwa maana ya kupigiwa kura za uchaguzi wa demokrasia.Kumudu au kutoyamudu madaraka hayo ni suala tofauti. Tathmini yangu ilihusu safu nzima ya uongozi wa CHADEMA kwa ujumla wao.Ni safu nyembamba mno.
2. Kujiunga na CHADEMA

Kama alivyosema Dr. Slaa Chadema walifanya jitihada ya kunishawishi niingie CHADEMA 2010 na niwe mgombea wao wa Urais. Jambo hili nililitafakari na kutafuta ushauri kwa watu wangu wa karibu na nikabaini kwamba:-
-CHADEMA wana migawanyiko yao ya uongozi tena ni ya hatari kwasababu ni ya kikanda za nchi – yaani nani anatoka wapi.
-Kutokana na yaliomo katika ilani yao ya uchaguzi 2010 – 2015 nilibaini mambo ya kiitikadi ambayo siyakubali kama vile sera ya majimbo. Sera ya majimbo inawezekana katika nchi ambazo ni tajiri na pia isiyo na tofauti kubwa ya hali ya maisha baina ya kanda mbalimbali za nchi kama vile Marekani (USA). Kuleta majimbo Tanzania ambako kuna tofauti kubwa za kimaendeleo baina ya Kaskazini, Mashariki, kati, Kusini na Magharibi ni kusababisha nchi ichanike vipande vipande. Huduma bure za elimu kuanzia chekechea hadi chuo kikuu na huduma bure za afya kwa wote ni ndoto na ni ghilba kwa wananchi. Isitoshe siamini kwamba kazi ya Serikali yoyote Duniani ni kuwalea Wananchi kwa umaskini huku ukiwaahidi huduma za bure badala ya kuwaendeleza wajitume na waongeze kipato ili wamudu gharama za maisha. Kwa hiyo nisingeweza kuwa mgombea Uraisi ndani ya chama ambacho itikadi zake za msingi sikubaliani nazo.

Baada ya hapo nisingeweza eti baada ya uchaguzi Mkuu niombe kugombea Uspika kupitia chama cha CHADEMA.
3. Kuhusu CCJ
Kama ilivyo kawaida kwa vyama vya siasa kutafuta wagombea bora, CCJ ni miongoni mwa vyama vilivyonifuata mimi na baadhi ya wanasiasa wakati wa maandilizi ya uchaguzi mkuu. jambo hili si la siri wala la ajabu na Nimelizungumza hili mara nyingi. Isitokee katika mfumo wa vyama vingi vya siasa mtu kutoka chama kumoja cha siasa na kujiunga na chama kingine haiwezi kusemwa kuwa ni uhaini. Na kama Ningeridhika na mambo yao ningejiunga na CCJ mwaka 2010 lakini sikufanya hivyo. Pia ni uzushi usio na msingi kunihusisha na uanzishaji wa chama hicho. Waanzilishi wa chama hicho cha siasa wanajulikana na wapo hai, ni haki ya kikatiba ya kila Mtanzania kuanzisha au kujiunga Binafsi na chama chochote cha siasa.
4. Madai mengine
Eti nilitamka kwamba ningehamia chadema na Wabunge wa CCM 55 ni porojo za Dr. Slaa kama ulivyo usemi ningeihama CCM siku chache kabla ya kuvunjwa Bunge la 9.
Inashangaza kwa Dr Slaa kukejeli uendeshaji wa bunge la 9 ambalo ndilo lililowapa fursa watu kama yeye kujulikana na kujipatia umaarufu.
Haya madai ya mimi nikiwa Spika kukwamisha uchunguzi wa Meremeta na Richmond ni kutokana na hisia tu za chuki. Taratibu za Kibunge hazimwezeshi Spika kuwa Dikteta anayeamua nini kijadiliwe na nini kisijadiliwe. Yote yapo katika kanunu za Bunge. Maamuzi ya Bunge si lazima yawe ni ya Spika.
Kuhusu ofisi ya Mbunge jimboni Urambo mahasimu wangu ndani ya CCM na nje yake wameng’ang’ania kwa makusudi maalum kuiita ofisi ile kuwa ni ya Spika. Michoro yake na gharama zake hata ukijumuisha samani haifikii tarakimu za ajabu wanazotaja mahasimu wangu kujenga hoja istoshe ofisi hiyo haina maslahi yeyote binafsi kwangu Aidha viongozi wengine waliofikia hadhi za juu mathlani ya uwaziri mkuu nao wamejengewa majimboni ofisi zinazolingana na hiyo 
Porojo nyingine binafsi kama vile kumuhusisha mke wangu kumpigia simu Dr Slaa kumsihi anisaidie kisiasa ni upuuzi wa aina yake unaodhihirisha umahiri wa Dr.Slaa katika siasa za kiwango cha chini.
5. HITIMISHO
Mimi nikiwa mwanasiasa mzoefu na mkongwe nimetoa ushauri na nitaendelea kutoa ushauri kwa makundi mbalimbali nchini.Kuniambia naingilia mambo ya CHADEMA ni kichekesho.Wakiwa wao ni chama cha siasa kinachoendesha harakati za kuwania kuchukua madaraka ya kuongoza nchi ambayo mimi ni raia wasitazamie kuwa sisi wapiga kura tutaacha kuwachambua.Wanalo tatizo kubwa la safu nyembamba mno ya uongozi, Kulingana na majukumu ya kuendesha nchi. Kujilinganisha na safu ya uongozi ya Baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere  ni mzaha wako wapi akina R.M Kawawa, Pauli Bomani, George Kahama, Amir Jamal, Solomoni Eliufoo, Tewa Saidi, Tewa Abdallah, Fundikira wa CHADEMA? Kutembea nchi nzima kuhamasisha chuki dhidi ya serikali iliopo madarakani ni jambo jepesi lakini Watanzania walio  makini wanahitaji maelezo ya mipango mbadala ya uchumi kuinua hali za maisha yao na kuiona safu ya uongozi itakayowezesha kwa dhati kubuni na kusimamia mikakati endelevu ya kuondoa umaskini kujenga uchumi imara na kuimarisha umoja wa watanzania

MWANDISHI DAUD MWANGOSI AUAWA JIONI HII


 

 

 

 ( Pichani Daud Mwangosi akiwa kazini muda mfupi kabla kufikwa na mauti yake.)
 
Hii hapa ni taarifa kutoka kwa Francis Godwin,

Mwandishi wa habari wa Chanel Ten mkoa wa Iringa na Mwenyekiti wa chaa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa Daud Mwangosi ameuwawa katika vurugu za Polisui i na wafuasi wa Chadema katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa leo

Mwanahabari huyo Daud Mwangosi aliuwawa majira ya saa 10 jioni katika ofisi za Chadema Nyololo huku askari mmoja akijeruhiwa vibaya kwa risasi .

Kabla ya kuuwawa kwa mwanahabari huyo mabomu yaliweza kupigwa eneo hilo kuwatawanya wafuasi hao wa Chadema ambao walikuwa wakigoma kutawanyika eneo hilo na kuamua kukaa chini kuwa haapo tayari kuondoka katika ofisi yao.

Chanzo cha mwanahabari Mwangosi kuuwawa klitokana na kukamatwa kwa mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe mkoa wa Iringa Godfrey Mushi na hivyo mwanahabari huyo kkutaka kuhoji polisi sababu ya kukamatwa kwa mwanahabari huyo ndipo askari hao walipoanza kumshambulia kwa kichapo na baadae mlio kama wa bomu ulisikika eneo hilo na mwandishi huyo na askari mmoja waliaguka chini .

Ndani ya dakika tano ilisikika sauti kutoka kwa askari huyo kuwa afande nimekufa ndipo walipomchukua na kumpeleka Hospitali ya wilaya ya Mufindi huku mwili wa mwanahabari huyo ukipelekwa chumba cha kuhifadhia maiti .

Katika vurugu hizo zilizodumu kwa takribani dakika 30 kwa askari na wafuasi wa Chadema kurushiana mawe kwa mabomu zaidi ya magari matano ya Chadema na ya wananchi yameharibiwa huku watu kadhaa wamejeruhiwa na mwanahabari mmoja Godfrey Mushi akijeruhiwa vibaya.

Hii ni taarifa ya Jeshi la polisi kabla ya tukio kwa vyombo vya habari

JESHI la polisi mkoa wa Iringa limesema limezuia mikutano ya vyama vya siasa kwa vyama vyote na sio kwa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) pekee hivyo laonya vyama vyote kutii sheria bila shuruti.

Hata hivyo jeshi hilo la Polisi limesema kuwa halifanyi kazi kwa matakwa ya chama chochote cha siasa na kuwa si kweli kama wanavyodai viongozi wa Chadema kuwa jeshi la polisi linatumiwa na chama cha mapinduzi (CCM) kuzuia mikutano hiyo.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Michael Kamuanda ametoa kauli hiyo leo ofisini kwake alipozungumza na waandisha wa habari kuhusu zuio la mkutano wa Chadema uliopangwa kuanza leo katika wilaya ya Mufindi.

” Nawatangazia wanasiasa na vyama vyote vya siasa pamoja na wananchi wa mkoa wa Iringa kuwa hakutakuwa na mikutano ya kisiasa kutokana na shughuli za sensa zinazoendelea ….hivyo basi nawaomba wananchi wote kutoshiriki mikutano yoyote ya kisiasa itakayoitishwa na wanasiasa “alisisitiza

Kuwa mikutano hiyo imezuiliwa kwa kipindi hiki cha sensa kilichoongezwa hadi hapo tamko litakapotolewa tena na msajili wa vyama vya siasa John Tendwa kama alivyokwisha kutoa tamko la kuzuia shughuli hizo za vyama vya siasa kwa kipindi hiki cha sensa.

“Wananchi wote wa mkoa wa Iringa mnaombwa kutii sheria bila shuruti hii ni amri ….nawaombeni sana wananchi kutodanganywa na wanasiasa kwa kuvunja sheria “aliongeza kamanda huyo wa polisi.

Hata hivyo alisema kuwa kimsingi zoezi la sensa lilipaswa kuhitimishwa Septemba mosi mwaka huu ila kutokana na serikali kuongeza muda wa zoezi hilo bado jeshi hilo la polisi linazingatia maagizo ya Msajili wa vyama vya siasa kama alivyoyatoa kwa jeshi hilo.

Kamanda Kamuanda alisema kuwa jeshi hilo la polisi wala msajili wa vyama vya siasa hajazuia vyama vya siasa kuendelea na vikao vyao vya ndani kwa kipindi hiki na kuwa hata Chadema wakiwa mkoani Iringa wameendelea kufanya vikao vyao vya ndani katika kata mbali mbali za mkoa wa Iringa na hakuna mtu aliyewazuia kuendelea kufanya hivyo.
Majibu ya Dkt Slaa
Wakati jeshi la polisi likipinga shughuli hizo za vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara katibu mkuu wa Chadema Taifa Dkt Willbroad Slaa ameibuka na kusema kuwa chama chake kitaendelea na mikutano kama kilivyojipangia na kuwa wapo tayari kwa lolote litakalojitokeza .

Dkt Slaa alisema kuwa walivumilia mara ya kwanza walipozuiwa mikutano hiyo mkoani Iringa na kuvuta subira hadi jumamosi zoezi hilo lilipomalizika sasa anashangazwa kuona jeshi hilo likiendelea kuzuia mikutano hiyo tena.

“Tumemsikiliza kamishina wa sensa Hajati Amina Mrisho Said kuwa hadi sasa watu asilimia 95 wameandikishwa huku akiwata wale ambao bado kuwapigia simu wenyeviti wa mitaaa na vijiji ili wakaandikishwe na makarani wa sensa ….sasa jeshi la polisi linataka kutuambia kuwa hao watu asilimia 5 waliobaki wapo Iringa peke yake hadi wakazuia mikutano yetu? tunasema hatutakubali tutaendelea na mikutano yetu kama kawaida hatupotayari kabisa kusubiri hadi tarehe nane” alisema Dkt Slaa.

Pia alisema kuwa kama ni uzalendo sasa umefika kikomo na kuwa wataendelea na ratiba zao za mikutano kama ilivyopangwa na watapambana kwa lolote . Chanzo: Francisgodwinblog ( Iringa)

Rais Jakaya Kikwete Ashiriki Mazishi ya Kiongozi wa Ethiopia Marehemu Meles Zenawi


 

 Mmoja wa Askari Nchini Ethipia akilia kwa uchungu

 Jeneza la aliyekuwa Waziri mkuu wa Ethiopia Marehemu Meles Zenawi likiletwa katika viwanja vya Addis kwaajili ya maombolezo ya kitaifa kabla ya mazishi yake yaliyofanyika leo. Askari wa kike akilia kwa uchungu
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Rais Jackob Zuma wa Afrika ya kusini wakati wa mazishi ya aliyekuwa Waziri mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi jijini Addis Ababa leo mchana.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais Yoweri Kaguta Museveni wakati wa mazishi ya kiongozi wa Ethiopia marehemu Meles Zenawi yaliyofanyika leo jijini Addis Ababa.Picha na Freddy Maro-IKULU