WAFANYAKAZI MUHIMBILI WAONGEZA MAPATO HADI KUFIKIA SH 4.8 BILIONI


mase1

Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza katika hafla ya kuwatunukia vyeti wafanyakazi bora 54. Hafla hiyo imefanyika  katika hospitali hiyo.

mase2

Wafanyakazi wa hospitali hiyo wakiwamo madaktari na wauguzi wakimsikiliza Profesa Museru

mase3

Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Muhimbili, Mziwanda Chimwege akisoma risala kwa mgeni rasmi, Profesa Museru katika hafla ya kuwakabidhi vyeti wafanyakazi bora.

mase4

Wafanyakazi wa hospitali hiyo wakimsikiliza Mwenyekiti wa TUGHE, Mziwanda Chimwege.

mase5

William Chimwege wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Hospitali hiyo, akipokea cheti  kutoka kwa Mkurugenzi wa Uuguzi, Agness Mtawa baada ya kuchaguliwa kuwa mfanyakazi bora.

mase6

Mkurugenzi wa hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru akimkabidhi cheti mfanyakazi wa Idara ya Ajira na Mafunzo, Farisha Jumanne baada ya kuchaguliwa kuwa mfanyakazi bora.

mase7

Wafanyakazi wa Muhimbili wakiserebuka baada ya wafanyakazi bora kutunukiwa vyeti. Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)

Na John Stephen, MNH

Dar es Salaam. Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imefanikiwa kuongeza mapato kutoka Sh 2.3 bilioni yaliyokuwa yakikusanywa Desemba mwaka jana hadi kufikia Sh 4.8 bilioni Mei mwaka huu.

Hayo yamesemwa LEO na Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru wakati hafla ya kutunuku vyeti kwa wafanyakazi bora wa hospitali hiyo.

Hospitali hiyo imefanikiwa kuongeza mapato kutokana na juhudi za wafanyakazi ambao wanafanya kazi kwa ari kubwa ili kutoa huduma bora kwa wagonjwa. Pia, wafanyakazi wamehamasika kutokana na mkurugenzi huyo kuwajali wafanyakazi na kusikiliza kero na kuzitatua kwa wakati kwa mfano hivi karibuni alilipa malimbikizo ya wafanyakazi.

Profesa Museru amesema mapato hayo yameongezeka kutokana na juhudi za wafanyakazi ambao wamekuwa wakifanya kazi kwa bidii na hivyo kusababisha mapato hayo kufikia Sh 4.8 bilioni.

“Mafanikio haya yametokana na juhudi za wafanyakazi. Mwaka jana niliwaomba wafanyakazi wafanye kazi kwa bidii, na wao walikubali. Imani yangu ni kwamba posho kwa wafanyakazi wangu zitaanza kulipwa baada ya bodi kupitisha ombi la kuwaongezea. Nafikiri tukiwaeleza vizuri bodi watatuelewa na hivyo wafanyakazi watapata kile tulichowaahidi,” amesema Profesa Museru.

Mkurugenzi huyo amesema kwamba hospitali imepata mafanikio makubwa yakiwamo kuongeza huduma za afya kwa mfano kuanzishwa kwa huduma ya kusafisha figo, kuongeza wodi kwa wagonjwa wanaohitaji uangali maalumu, huduma za matumbo na kuboreshwa kwa mazingira ya kutolea huduma.

Amesema hospitali hiyo inajitahidi kuongeza mapato zaidi ili iweze kulipia huduma za umeme, huduma za simu, ankra za maji pamoja na kudi za majengo.

“Sisi hatufanyi biashara bali tunatoa huduma kwa wagonjwa, tunapaswa kuongeza mapato ili kulipia huduma kutoka kwa washirika wetu akiwamo Tanesco, kulipia maji na huduma za simu,” amesema Kaimu Mkurugenzi huyo.

Akizungumzia changamoto, Profesa Museru amesema sehemu zinazotumika kutoa huduma zinatakiwa kukarabatiwa. Amesema miundombinu inapaswa kukarabatiwa kwa kuwa imekuwa ikichakaa kutokana na kuongezeka kwa wagonjwa hospitali hapo.

“ Majengo ya hospitali hayajakarabatiwa karibu miaka 20, hivyo tunapaswa kukarabati sasa,” amesema.

Pia Profesa  Museru amewapongeza wafanyakazi bora ambao wametunukiwa vyeti baada ya kuibuka kuwa wafanyakazi bora. Chanzo:mjengwablog

Advertisements

SEKTA YA KILIMO YAZIDI KUAJIRI WANAWAKE NA VIJANA NCHINI by John Bukuku on July 25, 2016


 

????????????????????????????????????

Na Beatrice Lyimo-MAELEZO

Dar es Salaam
SERIKALI imesema sekta ya kilimo inaendelea kuwa sekta muhimu katika uchumi wa Tanzania kwa asilimia 25% ya pato la taifa na kuajiri asilimia 75% ya watanzania  wakiwemo wanawake na vijana.
Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano katika Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Richard Kasuga wakati wa uzinduzi wa mchezo wa redio uitwao KUMEKUCHA unaotarajia kuonyesha mchango wa wanawake na vijana katika kutokomeza tatizo la uhaba wa chakula nchini.
Kasuga  amesema kuwa igizo hilo la mchezo wa redio, litaakisi umuhimu wa ushirikishwaji wa wanawake na vijana katika kukuza sekta ya kilimo na kutoa ujumbe kwa vijana kuona umuhimu wa kilimo hasa kilimo cha biashara.
“Sheria na tamaduni zilizopo zinakwaza juhudi za mwanamke kupata fursa za kiuchumi kwa sababu hawana haki ya kumiliki ardhi au vifaa vya kilimo, vyanzo endelevu vya maji, ukosefu wa mikopo ambayo wanahitaji ili kufanikisha juhudi zao”alisema Kasuga.
Kwa upande wake mwakilishi kutoka shirika la msaada la Marekani (USAID) Randy Chester alisema kuwa mchezo wa KUMEKUCHA umeandaliwa na taasisi ya Africa Lead kwa kushirikiana na Media for Development International (MFDI) na kufadhiliwa na USAID kwa lengo la kupunguza uhaba wa vyakula vyenye virutubisho hapa Tanzania.
Mchezo wa KUMEKUCHA ni mchezo wa redio wa kila wiki ambao unaangazia maisha, vikwazo na fursa za wakulima Tanzania na utaanza kurushwa hewani kuanzia Julai 25, 2016 kupitia Redio Free Afrika, Redio Abood FM, Redio Ebony FM na Redio Bomba FM

RAIS DK.SHEIN AWAAPISHA VIONGOZI ALIOWATEUWA LEO,


 

z1Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Bw.Said Bakar Jecha kuwa Kamishna wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma,katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo.

z2Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Bibi Septuu Mohamed Nassor kuwa Kamishna wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma,katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo,

z3Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Dk.Juma Yakout Juma kuwa Naibu Katibu Msaidizi wa Baraza la Mapinduzi (Sera,Ufuatiliaji na Tathmini) katika  hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar.

z4Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Ndg.Tahir Mohamed Khamis Abdulla kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira  katika  hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar

z5Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Issa Haji Ussi (Gavu) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Katiba Sheria,utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe,Haroun Ali Suleiman wakiwa ni miongoni mwa Viongozi waliohudhuria katika kuapishwa Viongozi mbali mbali leo Ikulu Mjini Zanzibar.

[Picha na Ikulu.] 25/07/2016.

WHO YATOA MAFUNZO KWA WATAALAM WA AFYA KUTOKA NCHI 14 ZA AFRIKA JIJINI DAR ES SALAAM


 

W1Mtaalam na Mkufunzi wa masuala ya Afya kutoka Makao Makuu ya Shirika la Afya Duniani (WHO) Geneva,Switzarland Olau Poppe akitoa mafunzo kwa Timu ya wataalam wa Afya kutoka nchi zipatazo 14 za Bara la Afrika kuhusu mfumo wa taarifa unaotumika kutambua sababu za kifo cha mgonjwa kuwajengea uwezo watalaam hao uelewa wa ujazaji wa taarifa sahihi juu ya sababu ya kifo cha mgonjwa kwenye cheti cha kifo (Death Certificate) ili wakatoe mafunzo kwa wataalam wengine kwenye nchi zao. Mafunzo hayo ya Siku mbili yanafanyika jijini Dar es salaam.

W2Mtaalam na Mkufunzi wa masuala ya Afya kutoka Makao Makuu ya Shirika la Afya Duniani (WHO) Geneva, Olau Poppe akifuatilia majadiliano ya washiriki wa mafunzo ya siku 2 ya wataalam wa Afya kutoka nchi zipatazo 14 za Bara la Afrika kuhusu mfumo unaotumika kutambua  sababu ya kifo cha mgonjwa utakaowasaidia watalaam hao kujaza taarifa sahihi kwenye cheti cha kifo.

W3Mtakwimu kutoka Makao Makuu ya Shirika la Afya Duniani (WHO) Geneva,Switzarland Doris MA FAT (Kulia) akigawa machapisho yenye mwongozo kuhusu namna ya kujaza taarifa mbalimbali zinazosababisha vifo wakati wa mafunzo ya siku 2 ya wataalam wa Afya kutoka nchi zipatazo 14 za Bara la Afrika leo jijini Dar es salaam.

W4 W5 W6Baadhi ya Washiriki wa mafunzo kwa Timu ya wataalam wa Afya kutoka Tanzania, Zambia na Cameroon wakifuatilia miongozo mbalimbali iliyokuwa inatolewa na watalaam kutoka Makao Makuu ya Shirika la Afya Duniani (WHO) wakati wa Mafunzo kuhusu mfumo wa taarifa unaotumika kutambua sababu za kifo cha mgonjwa kuwawezesha watalaam hao kujaza taarifa sahihi juu ya sababu ya kifo cha mgonjwa leo jijini Dar es salaam.

PICHA/Aron Msigwa -MAELEZO

DK. JOHN POMBE MAGUFULI ACHAGULIWA MWENYEKITI MPYA WA CCM, AMCHAGUA TENA KINANA KUWA KATIBU MKUU


1Mwenyekiti Mpya wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli na Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Dk. Jakaya Kikwete wakiwapungia mikono wajumbe wa mkutano mkuu maalum wa CCM baada ya wajumbe hao Kumthibitisha kuwa Mwenyekiti wa awamu ya Tano Kwa kumpigia kura zote za ndiyo wajumbe waliopiga kura ni 395 kura zilizoharibika ni 0 na Mwenyekiti Dk. John Pombe Magufuli ameshinda kwa kwa kupigiwa kura zote 395, Lakini pia mwenyekiti  huyo ameamua kuendelea na Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana na Sekretarieti nzima iliyokuwa chini ya Mwenyekiti Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DODOMA)

2Mwenyekiti Mpya wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akipongezwa na Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Dk. Jakaya Kikwete mara baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa CCM.

3Mwenyekiti Mpya wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akikabidhiwa ripoti ya uchaguzi uliopita na  Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Dk. Jakaya Kikwete.

6Mwenyekiti Mpya wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisikiliza machache kutoka kwa  Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Dk. Jakaya Kikwete kabla ya kukabidhiwa ripoti hiyo.

7Mwenyekiti Mpya wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akipokea ilani ya uchaguzi kutoka kwa  Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Dk. Jakaya Kikwete.

8 9

Viongozi wastaafu wakiwa katika mkutano huo kutoka kushoto ni Mzee John Samwel Malecela, Mzee Amani Abeid Karum, Mzee Salim Ahmed Salim, Mzee Mohamed Gharib Bilal na Mzee Pius Msekwa.

10Viongozi hao wakiwa katika meza kuu wakati wa mkutano huo.

11

Mwenyekiti wa Chama cha TLP Ndugu Agustino Mrema akiwasliana na wake wa viongozi wastaafu.

12Baadhi ya wajumbe wakishangilia mara baada ya mkutano huo kumthibitisha Rais Dk. John Pombe Magufuli kuwa Mwenyekiti wa CCM.

13 14 15Mwanachama wa CHADEMA Mgana Msindai akiwapungia mkono wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM baada ya kurejea CCM alipotangaza rasmi kwenye mkutano mkuu huo.

16Mgana Msindai akielekea jukwaani ili kutangaza nia yake ya kurejea CCM leo kwenye mkutano mkuu wa CCM mjini Dodoma.

17Mzee John Momose Cheyo Mwenyekiti wa UDP aktoa salam zake kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM.

18Freddy Mpendazoe aliyekuwa mwanachama wa chama cha CHADEMA akitangaza nia yake ya kurejea CCM kwenye mkutano mkuu wa Chama hicho uliofanyika mjini Dodoma leo.leo.

19Mzee Yusuf Makamba akisalimiana na Mwanaye Januari Makamba Mzee Makamba alikuwa ni kivutio kwa wajumbe wa mkutano mkuu kutokana na hotuba yake aliyoituma leo.

20Mzee Yusuf Makamba akisalimiana na baadhi ya wake wajumbe wa mkutano huo.

21Mwenyekiti Mpya wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akijadi;iana jambo na  Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Dk. Jakaya Kikwete mara baada ya kuahirishwa kwa mkutano mkuu wa CCM uliofanyika mjini Dodoma leo .Chanzo:fullshangweblog

WANACHAMA WA CUF KUPIGA HODI KWA IGP MANGU


Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrul (wa nne kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, wakati akitoa msimamo wa chama hicho kuhusu mikakati ya Jeshi la Polisi dhidi ya vyama vya siasa hasa cha Cuf. Wengine ni maofisa mbalimbali wa chama hicho.

Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Tanzania Bara, Shaweji Mketo, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam , wakati wa kutoa msimamo wa chama hicho kuhusu mikakati ya Jeshi la Polisi dhidi ya vyama vya siasa hasa cha Cuf. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Ulinzi Taifa, Mustafa Wandu na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrul.

Na Dotto Mwaibale 

MKURUGENZI wa Uchaguzi wa Chama cha Wananchi (CUF) Shaweji Mketo amesema iwapo Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu ataendelea kukifuatilia chama hicho wanachama wa chama hicho watekwenda ofisini kwake kumsalimia.

Mketo ameyasema hayo Makao Makuu ya Chama hicho Buguruni jana Dar es Salaam leo wakati Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrul alipo kuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu msimamo wa chama hicho kuhusu mikakati ya Jeshi la Polisi dhidi ya vyama vya siasa hasa cha Cuf.

“Tunasema sisi Cuf hatumuogopi IGP na kama ataendelea kutufuatafuata haita pita wiki mbili tutamfuata kwenda kumsalimia ofisi kwake” alisema Mketo. Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrul

alisema chama hicho kimesikitishwa na kauli ya IGP aliyoitoa hivi karibuni wakati akihojiwa Tido Mhando wa Kituo cha Televisheni cha Azzam kuwa jeshi hilo wakati wowote litamkamata Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad kwa kuwachochea wafuasi wake ili waichukie serikali iliyopo madarakani.

Alisema baada ya kuitafakari kauli hiyo ya IGP wamebaini kwamba hivi sasa IGP Mangu ameamua kuwathibitishia watanzania kuwa jeshi la polisi ni idara maalumu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mazrul alisema kwa muda mrefu IGP Mangu amekuwa akilitumia jeshi la polisi kushiriki katika matukio mbalimbali ya kuhujumu demokrasia na kukiuka haki za binadamu kwa lengo la kukinusuru Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutokana na anguko kubwa la kukataliwa na wananchi kama ilivyothibitika kabnla na baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka jana.

Alisema jeshi la polisi limekuwa na utaratibu wa kukamata raia, kuwapiga kuwabambikia kesi, kuwashikilia na kuwatesa katika vituo vya polisi bila ya kuwafikisha mahakamani.

Mazrul alisema hadi sasa zaidi ya wananchi 400 wameathiriwa kutokana na hujuma za jeshi la polisi kwa kuwabambikia kesi.

TANZANIA NA CHINA ZATILIANA SAINI HATI YA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO UJENZI WA RELI YA KATI KWA KIWANGO CHA KIMATAIFA


FED1

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile (aliyeipa mgongo kamera), akizungumza jambo kabla ya kutia saini Hati ya makubaliano ya ushirikiano wa ujenzi wa miradi mbalimbali ukiwemo ujenzi wa Reli ya Kati katika kiwango cha Kimataifa (Standard gauge) na Benki ya Exim ya China, Jijini Dar es salaam.

FED2

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile (Kulia) akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt. Leonard Chamuriho (katikati) kabla ya kutia saini Hati ya makubaliano ya ushirikiano wa ujenzi wa miradi mbalimbali ukiwemo ujenzi wa Reli ya Kati katika kiwango cha Kimataifa (Standard gauge) na Benki ya Exim ya China, Jijini Dar es salaam Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James.

FED3

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile (Kushoto) akitoa maelezo kwa mmoja wa maafisa wa Benki ya Exim-China,  kabla ya kutia saini Hati ya makubaliano ya ushirikiano wa ujenzi wa miradi mbalimbali ukiwemo ujenzi wa Reli ya Kati katika kiwango cha Kimataifa (Standard gauge), na Benki ya Exim ya China, Jijini Dar es salaam.

FED4

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile na Naibu Meneja Mkuu (Mikopo Nafuu) wa Benki ya Exim ya China, Zhu Ying, wakitia saini Hati ya Makubaliano ya  Ushirikiano wa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwemo ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Kimataifa (Standard gauge), Jijini Dar es salaam.

FED5

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile akipeana mkono na Naibu Meneja Mkuu (Mikopo Nafuu) wa Benki ya Exim ya China, Zhu Ying, mara baada ya kutia saini Hati ya Makubaliano ya  Ushirikiano wa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwemo ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha Kimataifa (Standard gauge), Jijini Dar es salaam.

FED6

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip I. Mpango (Mb) (kushoto), akizungumza na Rais wa Benki ya Exim-China, Liu Liange, katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere jijini Dar es salaam kabla ya Rais huyo aliyekuwepo nchini kwa ziara ya kikazi kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli. Kulia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa.

FED7

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip I. Mpango (Mb) (kulia), akipeana mkono na  Rais wa Benki ya Exim-China, Liu Liange, katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere jijini Dar es salaam kabla ya Rais huyo aliyekuwepo nchini kwa ziara ya kikazi kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, kuondoka nchini.

FED8

Rais wa Benki ya Exim kutoka China, Liu Liange (kulia) akiwa katika Uwanja wa ndege wa  Kimataifa  wa JK Nyerere, muda mfupi kabla ya kuondoka nchini kurejea China baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi nchini ambapo Benki yake imeahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania kutekeleza Miradi Kadhaa ya Maendeleo ukiwemo ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha kimataifa (Standard gauge)

FED9

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip I. Mpango (Mb) (kulia), akiagana na  Rais wa Benki ya Exim-China, Liu Liange, katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere jijini Dar es salaam kabla ya Rais huyo aliyekuwepo nchini kwa ziara ya kikazi kwa mawaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli. Chanzo:mjengwablog