Kutoka Gazeti la Mwananchi LEO:Wakati vyama vya upinzani vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), vikitafakari jina la mgombea urais, Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila tayari anaye mtu anayefaa; anamtaka Dk Willbrod Slaa.


Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbrod Slaa
—–
Wakati vyama vya upinzani vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), vikitafakari jina la mgombea urais, Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila tayari anaye mtu anayefaa; anamtaka Dk Willbrod Slaa.
Kwa maoni yake, si kwamba viongozi au wanachama wa vyama vingine vinavyounda Ukawa hawana sifa za kuwania nafasi hiyo ya juu katika siasa nchini, bali Dk Slaa ana sifa ya ziada; ana mvuto.
Katika mahojiano maalumu na gazeti hili, Kafulila, ambaye alikuwa mwanachama wa Chadema kabla ya kuondoka na kujiunga na NCCR-Mageuzi mwaka 2010, alisema Dk Slaa ana nafasi kubwa kuliko viongozi wa vyama vingine vya siasa vinavyounda umoja huo ambavyo ni Chadema, NCCR, NLD na CUF kwa sababu katibu huyo mkuu wa Chadema anakubalika zaidi katika jamii kulinganisha na wengine.
read more

Kutoka Gazeti la Mwananchi LEO: Siku moja baada ya Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), Nimrod Mkono kusema amelishwa sumu akiwa London, Uingereza, Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee amemtaka kusema ukweli na si kulihadaa Taifa kwa uongo.


Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee.
  Siku moja baada ya Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), Nimrod Mkono kusema amelishwa sumu akiwa London, Uingereza, Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee amemtaka kusema ukweli na si kulihadaa Taifa kwa uongo.
Mkono akizungumza na waandishi wa habari juzi kuelezea mwenendo wa afya yake, alisema lengo la kulishwa sumu ilikuwa ni kutaka kuharibu figo zake ndani ya saa 72 kitendo kilichoshindikana.
Mdee aliyekuwa na Mkono katika ziara hiyo alisema: “Hakuna ukweli wowote kwamba alilishwa sumu, nilikuwa naye kule na mazingira aliyoanza kuumwa hadi kupona kwake ni utata… awaeleze Watanzania anaumwa nini na si kusema alilishwa sumu.
“Nilikaa kimya baada ya kuripotiwa na gazeti moja (The Citizen) kwamba Mkono kalishwa sumu, sasa amezungumza tena nikaona si busara kukaa kimya wakati alilidanganya Taifa. Mkono waeleze ukweli watu mbona unawadanganya.”
read more

Serikali Tanzania ichunguze kashfa ya pembe za ndovu


Serikali ya Tanzania imetakiwa ifanye uchunguzi wa kimataifa kubaini watu waliohusika na ripoti iliyoitia doa serikali kuhusu madai ya kusafirishwa pembe za ndovu kwenye ndege ya Rais wa China, Xi Jinping.
Kauli hiyo imetolewa Bungeni na Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA), Joseph Mbilinyi wakati akichangia mapendekezo ya utekelezaji wa mpango wa taifa kwa mwaka wa fedha 2015/2016.
Mbunge huyo wa chama kikuu cha upinzani cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA amesema kuwa, serikali isije na kauli nyepesi kama ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, kuwa taarifa hizo ni za uzushi na badala yake ifanye uchunguzi.
Akizungumza hivi karibuni katika mahojiano maalumu na idhaa hii ya Radio Tehran, Profesa Ibrahim Haruna Lipumba Mwenyekiti Taifa wa Chama cha Upinzani cha Wananchi CUF alielezea kusikitishwa kwake na mitandao ya ufisadi na ujangili iliyokita mizizi serikali na kubainishwa kwamba, umefika wakati sasa kwa Watanzania kuleta mabadiliko ya uongozi ili kuokoa utajiri na rasilimali za nchi zinazoporwa huku serikali ya chama tawala CCM ikionekana kushindwa kukabiliana na wimbi hilo la uporaji.