JAJI LUBUVA AITAKA TUME YA HAKI ZA BINADAMU KUJIFUNZA KWA TUME YA UCHUNGUZI KUIMARISHA UTAWALA BORA

1

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva (kulia) akiungana kuimba wimbo wa Taifa na Mgeni Rasmi wa Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Kuanzishwa kwa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi (TKU) Mhe. Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki (kushoto) na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bahame Nyanduga, kwenye ufunguzi wa maadhimisho hayo liliyofanyika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

2

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva (kulia) akieleza uzoefu wake kuhusu shughuli za Tume ya Kudumu ya Uchunguzi (TKU) kwenye kongamano hilo.

3

Baadhi ya viongozi wa Serikali waliohudhuria Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Kuanzishwa kwa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi (TKU) kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam wakiongozwa na Rais Mstafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi (wa pili kulia) wakifuatalia taarifa ya Jaji Mst. Lubuva.Wengine ni Mawaziri Wakuu Wastaafu Fredrick Sumaye (kulia), Jaji Mstaafu Joseph Warioba (wa tatu), na Mwanasheria Mkuu Mstaafu Jaji Mack Bomani na Mwenyekiti Mstaafu wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Jaji Kiongozi Mstaafu Amiri Manento.

4

Baadhi ya Wageni Waalikwa wakiwemo kutoa Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania na Wawakilishi wa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi za nchi za Afrika, wakifuatilia taarifa ya Jaji Mst. Lubuva.

5

Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Alhaj Ali Hassan Mwinyi akipokea tuzo ya Heshima ya Utawala Bora kutoka kwa Mgeni Rasmi wa Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Kuanzishwa kwa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi (TKU) Mhe. Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

6

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva (katikati) akiwa amepokea Cheti cha Utambuzi wa Utumishi wake kwenye Tume ya Kudumu ya Uchunguzi (TKU) kutambua mchango wake.Kushoto ni Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Bahame Tom Nyanduga na kulia ni Katibu Mtendaji wa Tume hiyo Mary Massay.

7

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva (wa tatu kulia) akiungana na kwenye picha ya pamoja na na Mgeni Rasmi wa Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Kuanzishwa kwa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi (TKU) Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Viongozi wengine wa Serikali Wastaafu waliohudhuria maadhimisho hayo kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam..

8

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva, akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi.

9

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva akimueleza jambo Mgeni Rasmi wa Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Kuanzishwa kwa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi (TKU) Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki baada ya ufunguzi wa maadhimisho hayo.

10

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva, akibadilisha mawazo na Wanasheria Wakuu wa Serikali Wastaafu wenzanke Jaji Mst. Mark Bomani 1965-1976 na Jaji Mst. Joseph Sinde Warioba 1976 -1985.Jaji Mst. Warioba alitumikia nafasi hiyo kuanzia mwaka 1985 hadi 1993.

11

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva akizungumza na kituo cha Televisheni cha ITV baada ya ufunguzi wa Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Kuanzishwa kwa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi (TKU) Picha na Hussein Makame-NEC

Hussein Makame, NEC

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva ameitaka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kujifunza uzoefu wa tendaji wa  Tume ya Kudumu ya Uchunguzi (TKU) ili kuimarisha utawala bora nchini.

Jaji Mst. Lubuva ametoa wito huo wakati akeleza uzoefu wake juu ya utendaji kazi wa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi (TKU) wakati wa Maadhimisho ya Miaka 50 ya Tume hiyo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

Alisema pamoja na TKU kukabiliwa na changamoto nyingi katika inatekeleza majukumu yake wakati huo lakini ilifanya kazi zake kwa ufanisi kutokana na malalamiko ya wananchi yaliyoshughulikiwa kwa wakati huo.

“Katika hali na mazingira ya Tume ya wakati huo, bila kusita nashawishika kusema kuwa Tume ya Kudumu ilianzishwa wakati ambapo si watu wengi kwa bahati mbaya Afrka ambao walijali haki za binadamu na utawala bora” alisema Jaji Mst. Lubuva.

Aliongeza kuwa itakuwa si kusifia kusema kuwa TKU ilifanya kazi nzuri katika kipindi chake cha miaka 32 kwani ulikuwa wakati ambapo Tanzania ndio ilikuwa imejikomboa kutoka utawala wa Kikoloni na ilijitahidi kuendesha shughuli za maendeleo kwa wananchi.

Hata hivyo alisisitiza kuwa walithubutu kwa mwalimu kuleta wazo la kuanzisha TKU ili kunusuru wananchi kutakona na madhila ya matumizi mabaya ya madaraka ya viongozi na watendaji kwa wakati huo.

“Kwa upande mwingine Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ina kibarua kizito katika kutekeleza majukumu yake katika mazingira ya sasa ambapo tume hii si rahisi kuelezea kwa wananchi kwa nini isifanikiwe zaidi ya TKU”

Alisema THBUB tofauti na TKU ina bahati ya kujifunza kutokana na uzoefu wa tume hiyo ya kudumu katika mazingira ya sasa kulinganisha maendeleo na uelewa wawananchi kiujumla kuhusu haki zao za kimsingi kisiasa na kiutawala.

“Hivyo tunaposherehekea miaka 50 ya Tume ya Uchunguzi ni halali kusema kwamba ilikidhi haja na matakwa ya wananchi kwa wakati huo kuweka misingi imara ambayo THBUB itaitumia katika juhudi za kusonga mbele”alisema Jaji Mst. Lubuva.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejiment ya Utuishi wa Umma Mhe. Angellah Kairuki alisema lengo kubwa la Serikali kuanzisha TKU ilikuwa ni kumlinda mwananchi na lilifanikiwa kwa kushughulikia malalamiko 39,000 kwa kipindi cha miaka 35.

“Aidha malalamiko yaliyopokelewa katika kipindi cha miaka 15 (2001-2016) ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ni 32,000 na hivyo kufanya idadi ya malalamiko ya miaka 50 kufikia 71,000” alisema Mhe. Waziri Kairuki na kuongeza kuwa:

“Idadi hiyo inaonesha jinsi vyombo hivi vilivyo na manufaa kwa wananchi wanyonge.Baadhi ya malalamiko yaliyopokelewa ni kuhusu vitendo vya unyanyasaji, masuala ya utumishi, kuchelewa kutekeleza wajibu, , kukataliwa kuomba rufaa, kutrofuata taratibu za kisheria, mirathi, matumizi mabaya ya mali ya umma na migogoro ya ardhi”

Naye Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bahame Nyanduga alisema Maadhimisho ya Miaka 50 ya TKU yamekwenda sanjari na kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kwa kuanzisha Tume hiyo ikiwa ni taasisi ya kusimamia uwajibikaji wa watumishi wa umma kwa wananchi.

“Pili ni kujikumbusha huko tulikotoka na kujifunza kutokana na kazi za TKU, changamoto na na mafanikio iliyoyapata na mwelekeo unaotakiwa katika kuhakikisha dhana ya uwajibikaji na utawala bora zinaendelezwa nchini Tanzania” alisema Nyanduga.

Katika maadhimisho hayo Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi walipata Tuzo na Cheti cha kutambua mchango wao kuweka misingi ya uwajibika na utawala Bora. (P.T)

Leave a comment