Wabunge wataka uwazi mali za viongozi


 

 

 

Na Mwandishi wetu
KAMATI za Bunge zinazosimamia fedha za umma zimeazimia kuwa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma haiweki uwazi wa kutangaza umiliki wa mali za viongozi.
 
Hali hiyo inasababisha viongozi kutoweka wazi mali wanazozimiliki na ni rahisi mtu kuzushiwa umiliki usio wa kweli.
 
Katika maazimio yao 22 yaliyofikiwa siku ya mwisho wa mafunzo, juzi, kamati hizo za Hesabu za Serikali (PAC), Serika za Mitaa (LAAC) na ile ya Bajeti zimependekeza kuwa ni vema sekretarieti ikafanya utafiti wa umiliki wa mali kwa viongozi wa umma na kuweka taarifa hizo katika tovuti yake.
 
Lengo la kufanya hivyo ni kuwawezesha wananchi kuziona mali zinazomilikiwa na viongozi wao na pale ambapo kiongozi hatakuwa ametoa taarifa ya umiliki huo basi taarifa hiyo itolewe kwa tume.
 
Katika maazimio mengine kamati zimekubaliana kuwa kutokana na kutokuwepo na taarifa sahihi kuhusu deni la taifa, kuna umuhimu wa kuwakutanisha wadau wakuu wanaohusika hususan Benki Kuu (BoT), Hazina, Kamati za Bunge na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Fedha za Serikali (CAG).
 
Hatua hiyo itawawezesha kujua kwa usahihi zaidi ukubwa wa deni hilo. Vilevile imeamuliwa kuwa serikali ishauriwe kuunda chombo huru kitakachosimamia deni la taifa.

“Kamati za Bunge zinazoshughulikia usimamizi wa fedha na rasilimali za taifa zishughulikie zaidi maafisa masuuli hatarishi (risk based) ili kuleta thamani ya fedha katika utendaji wao. Kamati zishirikiane na CAG katika kuamua ni afisa masuuli yupi aitwe kukutana na Kamati,” walisema.
 

 

Advertisements

Waziri wa Uchukuzi,Mh.Dkt. Harison Mwakyembe amewafukuza kazi mtandao mzima uliohusika kusaidia kusafirisha madawa ya kulevya yaliyokamatwa huko Afrika Kusini hivi karibuni.


 Waziri wa Uchukuzi,Mh.Dkt. Harison Mwakyembe akionyesha picha ya Msanii Agness Gelard maarufu kwa jina la Masogange mbele ya waandishi wa habari,masogange alikamatwa na madawa ya kulevya huko nchini Afrika Kusini hivi karibuni.
 Waziri wa Uchukuzi,Mh.Dkt. Harison Mwakyembe akiongea na waandishi wa habari  jana ofisini kwake jijini Dares salaam juu ya hatua zilizochukuliwa na Wizara ya Uchukuzi juu ya sakata la madawa ya kulevya yaliyokamatwa huko Afrika Kusini hivi karibuni.Dkt. Mwakyembe amewafukuza kazi mtandao mzima uliohusika kusaidia kusafirisha madawa hayo, pia Waziri Mwakyembe ameliagiza jeshi la Polisi kuwakamata wafanyakazi hao na kuwaunganisha na wenzao kujibu mashitaka ya jinai.
waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Uchukuzi akiwa anafafanua hatua zilizochukuliwa na Serikali kuushughulikia mtandao mzima uliosaidia kupitisha madawa ya kulevya.
Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe jana ameanika majina ya watu saba waliohusika kupitisha mabegi tisa yaliyokuwa na kilo 180 za dawa za kulevya zenye thamani ya Sh8 bilioni, Julai 5 mwaka huu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), wakiwamo maofisa usalama wanne wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) na polisi mmoja.
 

Alisema mizigo ikishaondoka mikononi mwa abiria hukaguliwa tena kwa kutumia mbwa wa Idara ya Usalama wa Taifa, lakini siku ya tukio hilo mbwa hao walichelewa na walitumika baada ya mizigo kuingizwa kwenye masanduku ya chuma.
“Kwa abiria watatu kuwa na mabegi makubwa tisa yanayofanana si kitu cha kawaida kukwepa jicho la maofisa wa ushuru wa forodha na vyombo vya usalama, sijui walikuwa wapi siku hiyo?” alihoji Mwakyembe.Kwa Habari Zaidi Bofya na Endelea…>>>>>>>>

CCM YAWAVUA UDIWANI MADIWANI 8 WA MANISPAA YA BUKOBA-KAGERA


 

 

 

Nape

 

Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kagera jana tarehe 13/08/2013 katika kikao chake cha siku moja kilichofanyika mjini Bukoba imetangaza uamuzi wake wa kuwafutia dhamana ya CCM hivyo kuwavua Udiwani Madiwani wanane wa Manispaa ya Bukoba waliotokana na CCM.

 

Kwa mujibu wa utaratibu wa kutoa adhabu kwa viongozi wa CCM walio kwenye vyombo vya dola hasa Wabunge na Madiwani uamuzi wa Halmashauri Kuu ya Mkoa sio wa mwisho.  Uamuzi huo unapaswa kupata Baraka za Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ndipo utekelezwe.

 

Hivyo basi, mpaka sasa Madiwani hao wanane waliosimamishwa wanapaswa kuendelea na kazi zao kama kawaida wakisubiri kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa kitakachoketi tarehe 23 Agosti, 2013 mjini Dodoma ambacho pamoja na mambo mengine kitapitia uamuzi huo wa Halmashauri Kuu ya Mkoa wa Kagera.

 

Pamoja na hilo, tumepokea barua za Madiwani hao za kukata rufaa kupinga uamuzi huo wa Halmashauri Kuu ya Mkoa kwa msingi wa madai ya kukiukwa kwa utaratibu katika kufikia uamuzi huo.Tunawasihi wananchi wa Bukoba na Kata husika, wanachama na viongozi wote kuwa watulivu katika kipindi hiki ambapo suala hili linashughulikiwa na vikao vya Kitaifa.

 

Imetolewa na:-

 

Nape M. Nnauye,

 

KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA

 

ITIKADI NA UENEZI

 

14/08/2013

CUF yalaani waliomwagia tindikali wageni Zanzibar


 

 

 

 

Chama cha Wananchi, CUF, Zanzibar nchini Tanzania kimeelezea kushtushwa na tukio la kumwagiwa tindikali kwa raia wawili wa Uingereza katika maeneo ya Mji Mkongwe Zanzibar. 

 

 

 

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Salim Biman, Mkurugenzi wa Haki za Binadamu, Habari, Uenezi, Mawasiliano na Umma imesema CUF inalaani kwa nguvu zote tukio hilo la kikatili la kuwamwagia tindi wageni hao ,na kinawataka polisi Zanzibar kufanya uchunguzi wa kina na waharaka pamoja na kuhakikisha kuwa wale wote waliohusika na tukio hilo la kikatili wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria. 

 

 

 

Taarifa ya Chama cha CUF imesema kama ninavyonukuu, “hii ni dalili mbaya kwa Zanzibar kwani matukio haya ya tindikali yamekuwa yanaonekana kama ni masuala ya kawaida jambo ambalo linatishia uchumi wa Visiwa vyetu.

Taarifa Maalum Kwa Umma Kutoka Kwa Mbunge wa Jimbo la Mji Mkongwe Zanzibar Ismail Jussa:Taswira ya Zanzibar kama kisiwa cha amani inachafuliwa


Mbunge wa Mjini Mkongwe-CUF Ismail Jussa

Taswira ya Zanzibar kama kisiwa cha amani imechafuliwa tena jana usiku pale watu wasiojulikana walipofanya kitendo cha kinyama na kishenzi cha kuwamwagia tindikali (acid) wananchi wawili wa Uingereza katika maeneo ya Shangani, jimbo la Mji Mkongwe. 

Taarifa za awali nilizozipata ni kwamba vijana hao wawili wapo Zanzibar wakiwa ni sehemu ya vijana wanaojitolea (volunteers) katika shughuli za sanaa (Arts).

Nikiwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi wa jimbo la Mji Mkongwe, mwananchi wa Zanzibar ninayeipenda nchi yangu na pia nikiwa kama binadamu ninayethamini utu wa kila mtu nalaani vikali na kwa nguvu zote uovu na uhalifu huo ambao umekiuka misingi ya ubinadamu na utu. 

Polisi na mamlaka nyengine za nchi zinapaswa kufanya uchunguzi wa kina na wa haraka wa kuwajua ni nani waliohusika na tukio hili na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria. Hili la kuchukua hatua za haraka na za dharura na kuongeza kasi ya uchunguzi ni la muhimu sana maana sasa matukio ya hujuma kwa kutumia tindikali (acid) yamekuwa ni jambo la kawaida na yanaendelea kuongezeka. 


Tukio hili la jana linakwenda moja kwa moja na kupiga moyo wa uchumi wa Zanzibar kwa maana ya sekta ya utalii. Tusipochukua hatua za haraka na za dharura na kuonekana tunajali, uchumi wa Zanzibar unaweza kuathirika kwa kiasi kikubwa na kuyumbisha utoaji wa huduma kwa wananchi, huduma ambazo zinategemea mapato yanayotokana na utalii. 

Nilipata nafasi ya kufika haraka pale walipokuwepo waathirika wa tukio hilo mara baada ya kupata taarifa na pia kuwasindikiza hadi Uwanja wa Ndege wa Zanzibar nikiwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii naMichezo, viongozi wa Jumuiya ya Wawekezaji katika Sekta ya Utalii (ZATI) na  Balozi wa Heshima wa Uingereza aliyepo Zanzibar. 

Nawapa pole wasichana hao wawili na nawaombea wapone kwa haraka. Fikra, hisia na dua zetu ziko pamoja nao. Sifa ya Zanzibar kwa karne nyingi imekuwa ni kisiwa cha amani ambacho watu wake ni wastaarabu, wakarimu na wanaopenda wageni. Mjengeko wa jamii ya yetu ya Kizanzibari wenyewe umetokana na mchanganyiko wa watu kutoka sehemu mbali mbali duniani ambao walihamia Zanzibar na kupafanya ndiyo maskani yao. Kitendo kama hichi kilichotokea jana kinakwenda kinyume na misingi ya historia yetu hiyo.

Ni mapema kusema ni nani aliyepo nyuma ya kitendo hichi lakini jambo moja la wazi ni kuwa yeyote anayehusika amekusudia kuiumiza Zanzibar na Wazanzibari. Kuuhujumu utalii ni kuuhujumu uchumi wa Zanzibar na kuyahujumu maisha ya Wazanzibari. Wakati mamlaka zinazohusika zikiendelea na uchunguzi wa tukio hili, kuwasaka waliohusika na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria, natoa wito kwa Serikali kuchukua hatua zifuatazo: 

  1. Kuongeza doria za polisi ndani ya Mji Mkongwe ambao bado unabakia kuwa ndiyo mji mkuu wa Zanzibar na pia kituo kikuu cha harakati zote za kiuchumi ikiwemo biashara na utalii. Kuwepo kwa Polisi Jamii chini ya dhana ya Ulinzi Shirikishi kusiwe ndiyo mbadala wa Jeshi la Polisi kutekeleza wajibu wake hasa kufanya doria za kawaida. 


   1. Kuuwekea Mji Mkongwe kamera za mitaani za kufuatilia nyenendo za watu (surveillance cameras) hasa ikizingatiwa kuwa Mji Mkongwe ndiko kwenye harakati nyingi zinazopelekea mkusanyiko wa watu wengi wakiwemo watalii na wageni wengine wanaotembelea Zanzibar. 


    1. Mji Mkongwe kurejeshewa huduma ya taa za njiani na za mitaa (street lights) ili kuongeza usalama wa watu wakiwemo wageni wanaotembelea eneo hili ambako kuna idadi kubwa ya hoteli za kitalii. 


     1. Jeshi la Polisi Zanzibar limekuwa likilalamika kwa kuwa na bajeti ndogo isiyokidhi mahitaji ya kutekeleza wajibu wao ipasavyo ikiwa ni pamoja na kutokuwa na usafiri wa uhakika, mafuta na vifaa vya kazi. Mamlaka zinazohusika zinapaswa kukaa pamoja na kutatua matatizo haya. 


     1. Serikali, Jeshi la Polisi, na mamlaka nyengine zinazohusika pia wanapaswa kuwa na vikao vya mashauriano vya mara kwa mara na Jumuiya ya Wawekezaji katika Sekta ya Utalii (ZATI) na Jumuiya ya Watoa Huduma za Usafirishaji na Utembezaji Watalii (ZATO) ili kushughulikia matatizo mbali mbali yanayojitokeza hususan yale yanayohusu masuala ya usalama wa wageni wanaotembelea Zanzibar.


     Mwisho, natoa wito kwa wananchi na wakaazi wote wa Mji Mkongwe na Zanzibar kwa ujumla kuwa makini na kufuatilia nyenendo zinazotia mashaka au zinazoashiria mwelekeo wa kufanya vitendo vya uhalifu ndani ya Mji wetu na ndani ya Zanzibar au hata nje ya Zanzibar na pale wanapobaini mwelekeo kama huo kutoa taarifa haraka kwa mamlaka zinazohusika. ISMAIL JUSSA MJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI JIMBO LA MJI MKONGWE a na Jumuiya ya Wawekezaji katika Sekta ya Utalii (ZATI) na Jumuiya ya Watoa Huduma za Usafirishaji na Utembezaji Watalii (ZATO) ili kushughulikia matatizo mbali mbali yanayojitokeza hususan yale yanayohusu masuala ya usalama wa wageni wanaotembelea Zanzibar.


     Mwisho, natoa wito kwa wananchi na wakaazi wote wa Mji Mkongwe na Zanzibar kwa ujumla kuwa makini na kufuatilia nyenendo zinazotia mashaka au zinazoashiria mwelekeo wa kufanya vitendo vya uhalifu ndani ya Mji wetu na ndani ya Zanzibar au hata nje ya Zanzibar na pale wanapobaini mwelekeo kama huo kutoa taarifa haraka kwa mamlaka zinazohusika.


     ISMAIL JUSSA 

     MJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI 
     JIMBO LA MJI MKONGWE

     Tendwa afunguka baada ya kustaafu


      

      

     tendwa c3c74

     Siku moja baada ya kutangazwa rasmi kwamba aliyekuwa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa amestaafu kwa mujibu wa sheria, amejitokeza na kueleza yaliyo moyoni mwake.Katika mahojiano maalumu na Mwananchi jijini Harare jana, Tendwa alisema amepokea kwa mikono miwili kustaafu kutoka katika nafasi hiyo nyeti katika siasa za Tanzania, huku akisema anajiona mwenye bahati kufanya kazi na marais wawili katika nafasi yake.

     Tendwa amefanya kazi chini ya uongozi wa Rais Mstaafu Benjamin Mkapa na baadaye Rais Jakaya Kikwete. Nafasi ya Tendwa, imechukuliwa na Jaji Francis Mutungi ambaye alikuwa jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma.

     Akizungumzia kuhusu viongozi wa vyama vya upinzani kupokea kwa nderemo kustaafu kwake, Tendwa alisema wala hashangai kuyasikia hayo kwani inaonyesha kwamba kazi yake alikuwa akiifanya vyema na mujibu wa sheria.

     “Unajua unapokuwa msajili na ukaona wadau wote wanakushangilia hapo ujue kuna tatizo kubwa, nimekuwa ninafanya kazi yangu vizuri sana kwa kuzingatia misingi ya sheria ambayo imewekwa kwa mujibu wa sheria na kanuni,”alisema Tendwa.

     LM

      

      

     Alisema kwamba, “Unajua kuvilea vyama ni kazi kubwa sana ndugu yangu, maana kuna wakati hata Chama Cha Mapinduzi (CCM) walikuwa wanasema ninaegemea na kuvipendelea sana vyama vya upinzani. Leo nimestaafu nasikia vyama vya upinzani vinasema kwamba nilikuwa nawapendelea CCM, hiyo inaonyesha kwamba nilikuwa ninafanya kazi yangu sawa sawa.”

     Kitu gani ambacho Tendwa hatakisahau?

     Alisema kwamba katika miaka yake 13 ambayo amekuwa msajili hatomsahau waziri mmoja wa CCM.

     Hata hivyo, Mwananchi lilimbana kumtaja waziri huyo, lakini agoma kwa madai kwamba hapendi kuendeleza malumbano naye baada ya kustafu kwake utumishi wa umma.

     Tendwa alisema katika utumishi wake, waziri huyo alikuwa akimpatia wakati mgumu sana kwa kumpakazia kwamba yeye ni mpinzani.

     “Katika miaka yangu 13 ofisini sitaweza kumsahau huyo waziri maana alikuwa ananipakazia kwamba mimi ni mfuasi wa vyama vya upinzani. Ninamshukuru Mungu kwamba baadaye alikuja kuniomba msamaha, lakini ilikuwa imenisumbua sana katika kazi zangu,” alisema huku akionyesha masikitiko

     Kwa nini vyama vinashuka?

     Kuhusu kushuka na kupanda kwa vyama vya siasa hasa vile vya upinzani nchini baada ya uchaguzi kumalizika, Tendwa alisema katika kipindi chake cha uongozi aligundua kuwa migogoro ndani ya vyama hivyo ndio chanzo kikubwa cha kupoteza mvuto kwa wananchi.

     “Tatizo la vyama vingi vya upinzani Tanzania vinadhani kuwapata wabunge basi ndio vinakuwa vimechukua Serikali, vinasahau kujizatiti na kujipambanua mbele ya macho ya wapigakura kuwa vinasimamia kitu gani, badala yake nimekuwa vikiishia kwenye migogoro isiyo ya lazima,” alisema Tendwa.

     Tendwa alielezea jinsi ambavyo NCCR-Mageuzi ilivyokuwa na nguvu sana katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995, lakini baada ya kuingia kwenye migogoro chama hicho kikapoteza mvuto.

     “Badala ya kujiingiza kwenye migogoro vinatakiwa kujipanga kisayansi, lazima wajue kwamba siasa ni sanyasi,” alisema.

     Alisema hata CUF kilianza kupoteza mvuto kwa jamii baada ya kupata wabunge na kuanza kuibuka migogoro ya ndani.

     Jambo la kujivunia

     Tendwa alisema anajivunia kitengeneza muundo wa ofisi ambayo inazingatia maadili.

     Alisema wakati anakabidhiwa ofisi alikuwa peke yake ndiye mwanasheria mwenye kiwango cha shahada ya chuo kikuu, lakini hivi sasa msajili mteule atakuta zaidi ya wanasheria 16 katika ofisi zote tano za kanda pamoja na makao makuu.

     Pia alisema aliweza kuleta nidhamu ya matumizi ya fedha pamoja na kuleta weledi katika kujenga misingi imara ya ofisi hiyo ambayo imekabidhiwa jukumu kuvisimamia na kuvilea vyama vya siasa nchini.

     Ushauri kwa mrithi wake

     Tendwa alisema hawezi kumfundisha kazi Jaji Mutungi kwani anaamini atafanya kazi yake kwa mujibu wa sheria na taratibu kama ambavyo miongozo inavyotaka.

     “Mutungi atafanya kazi kwa mujibu wa sheria, siku zote atafuata sheria na kutafsiri sheria maana yeye ni Jaji. Ninawaomba wadau wampatie ushirikiano maana sasa anakuja kufanya kazi na wanasiasa,” alisema Tendwa.

     Alisema endapo Jaji Mutungi ataanza kubezwa na wanasiasa anatakiwa kujua ndani ya moyo wake kwamba anafanya kazi yake sawasawa.

     “Ila kama ataona wanasiasa wanamsifia basi atakuwa kuna sehemu ambazo hatekelezi vyema majukumu yake. Kufanya kazi na wanasiasa kunahitaji busara na sio kufuata vitabu vya sheria vinasemaje,” alimshauri Jaji Mutungi.

     Alisema baada ya kustaafu ana mpango wa kufanya kazi za ushauri katika siasa za kimataifa na sio siasa za maji taka.

     “Nahitaji muda kidogo kufikiri nitafanya nini ila napenda sana kuwa ‘international consultant’ kwenye masuala ya siasa, lakini pia ikumbukwe kwamba mimi ni mwanasheria ambaye nimekuwa katika masuala ya uwakili kwa takriban miaka 23. Muda utaongea nifanye nini, ngoja kwanza nikabidhi ofisi,” alisema Tendwa.

     Chanzo:Mwananchi

     Gazeti la Mwananchi: John Tendwa nje


      

      

      

     Rais Jakaya Kikwete amemteua Jaji Francis Mutungi kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa kujaza nafasi iliyoachwa na John Tendwa ambaye amestaafu kwa mujibu wa sheria.
      
     Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue ilisema kuwa uteuzi huo ulianza Agosti 2, 2013.
      
     Kabla ya uteuzi huo, Mutungi ambaye ameshika nyadhifa mbalimbali katika idara ya Mahakama, alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma.
      
     Alikotoka
      
     Historia ya Jaji Mutungi katika utumishi wake mahakamani ilianza mwaka 1989 alipoanza kazi akiwa hakimu, baadaye akateuliwa kuwa Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
      
     Baadaye aliteuliwa na kushika nafasi za Msajili Mahakama ya Ardhi; Hakimu Mfawidhi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Msajili Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Msajili Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Msajili Mahakama ya Rufani na hatimaye Jaji katika Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma.
      
     Kuhusu Tendwa
      
     Tendwa ameachia nafasi hiyo akiwa katika msuguano wa kisiasa na baadhi ya vyama vya siasa, kikiwamo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambacho hivi karibuni kilitangaza kutokumtambua wala kushirikiana naye.