Je ulijua kama Kondo la Nyuma au ‘Placenta’ huliwa?


Je ulijua kama Kondo la Nyuma au ‘Placenta’ huliwa? Saturday, 08 November 2014 Published in Jamii Read: 13 times Be the first to comment! Hugeuka kuwa uchafu pindi mamaanapojifungua , sasa kwa nini baadhi ya wanawake wanaamua kula Kondo la nyuma au Placenta ikiwa mbichi ? Kondo la Nyuma huwa ni sehemu ya mwili wa mama anapokuwa mjamzito, sehemu hiyo humsaidia mtoto kupata chakula na hewa kutoka kwa mama akiwa tumboni. Pindi mama anapojifungua kazi ya Kondo la Nyuma huisha papo hapo na hivyo hutupwa , lakini sio kila mtu ana mtazamo huu. Baadhi ya wanawake wanaamini kuwa madini yanayopitia kwa mkondo wa Nyuma hadi kwa mtoto ili kumuwezesha mtoto kukuwa huwa bado yanaweza kutumika na kwamba sio vizuri kuitupa. Njia za kula Kondo la Nyuma Husagwa na kuwa majimaji kama Sharbati vileInaweza kukaushwa na kutengezwa kama tembeKupikwa kwa kukaangwa kama vile nyama Wanasema kuwa mama bado anaweza kupata madini muhimu wakati anapoendelea kupata nafuu baada ya kujifungua na pia anapoanza kuonyonyesha kwa kula Kondo la nyuma.BBC