LOWASSA: KIONGOZI AWE NA NGOZI KAMA YA TEMBO


Edward Lowassa

Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa

NA NORA DAMIAN, DAR ES SALAAM

WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowasa amesema viongozi wenye maono na wasioogopa kusemwa ndio wanaotakiwa katika dunia ya sasa.

Lowasa aliyasema hayo jana alipokuwa akizindua helkopta ya Kanisa la Ufufuo na Uzima na vitabu tisa vilivyoandikwa na Askofu wa kanisa hilo, Josephat Gwajima.

“Hapa duniani kuna viongozi wa aina mbili, kuna viongozi ambao kazi yao ni kusimamia mahesabu na viongozi wenye maono.

“Na katika dunia hii ukitaka kushinda unatakiwa uwe na maono, mahusiano na mashirikiano mazuri na wenzako. Ukiogopa kusemwa hapa duniani hutaishi, unatakiwa kuwa na ngozi kama ya tembo,” alisema.

Kuhusu mgogoro wa ardhi unaolikabili kanisa hilo, Lowasa alisema atahangaika ili kuhakikisha kanisa hilo linafanikiwa kupata ardhi na kujenga kanisa kubwa.

Awali Askofu Gwajima alisema, amenunua helkopta hiyo kwa malengo mawili ambayo ni kusaidia watu wakati wa majanga mbalimbali pamoja na kueneza injili.(Martha  Magessa)

Read more…