Mbunge ‘Sugu’ afikishwa Mahakamani na Kushinda Kesi ya Kumuita Waziri Mkuu ‘Mpumbavu’


 

images c94ff

Leo asubuhi Joseph Mbilinyi (Sugu) alipelekwa mahakamani kwa shitaka la kutumia lugha ya matusi dhidi ya Waziri Mkuu, shtaka hili lilifunguliwa kwenye mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Dodoma na mwendesha mashitaka wa serikali.

Baada ya kufunguliwa shtaka hilo, Lissu ambaye alikuwa wakili wa Sugu aliitaka mahakama ifutilie mbali shtaka hilo kwani halina msingi wowote wa kisheria, na baada ya mabishano ya kisheria baina ya Lissu na wanasheria wa serikali kushindwa kuthibitisha kuwa neno Mpumbavu ni lugha ya matusi, hakimu ameamua kufuta shtaka hilo na ametangaza kuwa Sugu yuko huru na hana kesi ya kujibu.Chanzo:mjengwablog

Rais Jakaya Kikwete Akutana Kwa Mazungumzo na Kiongozi wa Shirika la UNDP (UNDP Administrator) Bi. Helen Clark ikulu jijini Dar es Salaam


 

 Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha na kufanya mazungumzo na Kiongozi wa Shirika la UNDP (UNDP Administrator) Bi. Helen Clark ikulu jijini Dar es Salaam jana asubuhi.
 Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akifanya mazungumzo na Kiongozi wa Shirika la UNDP (UNDP Administrator) Bi. Helen Clark ikulu jijini Dar es Salaam janaasubuhi.
 Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha na kufanya mazungumzo na Kiongozi wa Shirika la UNDP (UNDP Administrator) Bi. Helen Clark ikulu jijini Dar es Salaam jana asubuhi.Picha na Freddy Maro-IKULU

BARNABA NA MAREHEMU MAMA YAKE ENZI ZA UHAI WAKE


Barnabas Elias ‘Barnaba Boy’ akiwa na mama yake mzazi enzi za uhai wake.

Mwanamuziki Barnabas Elias ‘Barnaba Boy’ alfajili ya jana (Jumamosi) aliondokewa na mama yake mzazi aliyekuwa anasumbuliwa na presha. Kupitia ukurasa wake wa Twitter muda mfupi uliopita Barnaba ameweka picha yake akiwa na marehemu mama yake enzi za uhai wake na kuandika ujumbe huu wa majonzi: Amka. Mama hata dk.1 uliniita nikakwambia naja kesho kumbe ulikuwa uniage. Mama angu amka. Uwii nani ale matunda yangu. Ujumbe mwingine alioandika staa huyo kutoka kundi la THT ni huu: Lala mahali pema peponi na Mungu akuweke kwenye amani ya milele. Naumia mama amka. Hata Dk. 1 uwiii. Umefanya niimbe leo. Haupo, uwii mama yangu!

Mtandao huu unamtakia roho ya ujasiri Barnaba katika kipindi hiki kigumu na Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu. AMEN.Chanzo:www.globalpublishers.info

 

Neno La Leo; ” Hell Is The Other People!”- Jehanam Ni Wale Wengine!


 

 

 

 

 

 

 

 

 

Neno La Leo; ” Hell Is The Other People!”- Jehanam Ni Wale Wengine!

 

 

 

Ndugu zangu,

Mwanafalsafa Jean- Paul Sartre anasema; “ Hell is the other people” – Kwamba jehanam ni wale wengine. Anataka pia tukubaliane, kuwa pepo yaweza kuwa ni wale wengine.

Na hakika, tofauti ya mwanadamu na mnyama iko kwenye kufikiri. Mnyama anaongozwa na hisia, lakini mwanadamu anapaswa aongozwe na kufikiri. Ndio maana ng’ombe anaweza kumpanda mama yake. Ni hisia tu zitakazoongoza tendo lake.

Hivyo, mwanadamu kwenye mambo ya msingi hapaswi kabisa kuongozwa na hisia ikiwamo ushabiki. Anapaswa kufikiri. Na zaidi kufikiri kwa bidii.

Vinginevyo, ni ukweli, kuwa kijamii, mwanadamu anaweza kuwa kiumbe anayeishi kwenye mahusiano ya kirafiki na kiadui na wenzake. Na katika hilo la uadui, wanadamu, kama ilivyo kwa wanyama, wanaweza kushindania na hata kugombania vingi; iwe fedha, mashamba, wanawake na hata kivuli cha mti.

Ndio, unaweza kabisa kuwakuta wanadamu wawili wanagombania kivuli cha mti, kwamba nani mwenye haki ya kukaa kivulini. Na wanaweza kugombana mpaka akatokea mwendawazimu atakayekuja kuukata na huo mti wenyewe. Na wanadamu hao watabaki wakitazamana juani.

Mara nyingi, migogoro husababishwa na kugombania kisichotosha. Hivyo, lililo la msingi ni kutambua, kuwa wanadamu tunategemeana. Kwamba panapo kushindania jambo, mwanadamu, tofauti na mnyama, anapaswa kufikiri sana. Atangulize kwanza hekima na busara.

Na kwenye mgogoro wowote ule, mwanadamu ayape mazungumzo nafasi ya pekee katika kufikia muafaka, na si vurugu au mapigano. Kwenye mgogoro, na kwenye kuitafuta amani, panakosekana mazungumzo, basi,  ina maana ya uwepo wa mazingira ya kuvunjika kwa amani.

 

 

 

Na wanadamu sisi tumekuwa wepesi sana wa kunyosheana vidole na hata kuhukumiana pasipo kudadisi ili kuujua ukweli.

 

 

 

Na hapa nawaletea leo kisa cha wanandoa waliokaa miaka mingi bila kupata mtoto. Wakaamua wamfuge paka nyumbani. Naye paka huyo wakampenda sana kama mtoto wa kumzaa. Paka naye aliwapenda sana bwana na bibi nyumbani.

 

 

 

Ikatokea mke yule akapata mimba na hata kuzaa salama mtoto. Ikawa kama miujiza. Furaha nyumbani ikaongezeka.

 

 

 

Siku moja bwana na bibi walimwacha mtoto wao amelala kitandani. Nao wakaenda zao kuwasabahi jamaa na marafiki.

 

 

 

Walipokaribia nyumba yao wakati wakirudi nyumbani wakshtuka sana. Walimwona paka wao nje ya mlango akiwa na kipande cha nyama mdomoni. Sura yake ilitapakaa damu pia.

 

 

 

Wote wawili wakachukua miche ya kutwangia nafaka.  Kwa hasira wakamtwanga paka yule kichwani. Alikufa papo hapo.

 

 

 

Walipoingia chumbani wakamkuta mtoto wao amelala salama kitandani. Kando kuna nyoka mkubwa aina ya chatu. Nyoka  amekufa baada ya kujeruhiwa kwenye mapambano na paka.

 

 

 

Hell is the other people!- Jehanam ni wale wengine, lakini, pepo yaweza pia kuwa ni wale wengine. 

 

 

 

Ni Neno La Leo.

 

 

 

Maggid,

 

Iringa

 

Mwanasiasa mkongwe nchini Christopher Mtikila ameshinda kesi aliyofungua Mahakama ya Haki za Binadamu ya Afrika (AfCHPR) mjini Arusha akidai Tanzania inakiuka demokrasia inapozuia wagombea binafsi.


 

 

 

Mwanasiasa mkongwe nchini Christopher Mtikila

 

— 

 

Mwanasiasa mkongwe nchini Christopher Mtikila ameshinda kesi aliyofungua Mahakama ya Haki za Binadamu ya Afrika (AfCHPR) mjini Arusha akidai Tanzania inakiuka demokrasia inapozuia wagombea binafsi.

 

 

 

Katika hukumu iliyosomwa jana jioni, mahakama imesisitiza kuwa kwa kulazimisha viongozi watoke vyama vya siasa, Tanzania inawanyima wananchi wake fursa huru ya kushiriki kwenye uongozi.

Mchungaji Mtikila, ambaye ana historia ndefu ya kukwaruzana na serikali ya Chama Cha Mapinduzi, alifungua shauri mahakama ya Afrika mwaka 2011 baada ya jitihada zake za kupindua mabadiliko ya kikatiba yaliyofuta ugombea binafsi kugonga mwamba kwenye mahakama za kitaifa.Chanzo:hakingowiblog

SOMA RATIBA YA MAZISHI YA MSANII LANGA KILEO ALIYEFARIKI JANA


 

 

 

 

 

 


Ratiba ya mazishi ya ndugu yetu Langa Kileo itakuwa kama ifuatavyo, msiba upo nyumbani kwa wazazi wa Langa maeneo ya Mikocheni nyuma ya Hospitali ya AAR zamani kulikuwa na ofisi za Benchmark Production.

 Mwili wa marehemu utaagwa siku ya Jumatatu majira ya saa 7 mchana na baada ya hapo mwili utaelekea makaburi ya Kinondoni kwa mazishi majira ya saa kumi alasiri.Pia unaweza kubonyeza…http://www.kingkif.blogspot.com

From The Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation:President Jakaya Kikwete Congratulates Queen Elizabeth II on her 87th birthday.


 

 

 

 President Jakaya Kikwete

 

 

 

H.E Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania has sent a congratulatory message to Her Majesty Queen Elizabeth II on the occasion of her 87th Birthday.The message reads as follows: – 

 

 

 

“Your Majesty Queen Elizabeth II,
  Buckingham Palace,
  LONDON,  United Kingdom.

 

  On behalf of the people and the Government of the United Republic of Tanzania I have the pleasure to  congratulate Your Majesty mostly sincerely on the occasion of your 87thBirthday.

As you celebrate this important day please allow me to express my appreciation of the excellent bilateral relations that cordially exist between our two countries and peoples.

The occasion of your birthday offers us another opportunity to reaffirm our commitment to continue working closely in further strengthening the ties of friendship, cooperation and partnership

Please accept, Your Majesty, my very best wishes for your continued personal good health and peace and prosperity for the people of the United Kingdom”.

ALLY CHOKI:NIKIFA ASHA BARAKA ASIJE KWENYE MSIBA WANGU, NA KAMA ATAKUFA YEYE BASI SITAENDA


 


Asha Baraka amesema kama ni roho mbaya Chocky ndio anaoongoza kwa roho mbaya.

 

 

 

MKURUGENZI wa Extra Bongo Ally Chocky ametoa kauli nzito kuhusu waajiri wake wa zamani, Asha Baraka na Baraka Msilwa.

Katika maongezi yake  Chocky alisema katika watu asiowapenda duniani ni Asha Baraka (Mkurugenzi wa ASET) na Baraka Msilwa (Mwenyekiti wa ASET). Asha Baraka na Baraka Msilwa ni mtu na kaka yake.

Kiongozi huyo wa Extra Bongo akaenda mbali zaidi kwa kusema: “Nikifa leo hii Asha Baraka na Baraka Msilwa wasije kwenye mazishi yangu, na kama watanitangulia wao na mimi sitakwenda kwenye mazishi yao.“Nina uhakika leo hii nikipata matatizo au nikifa Asha na Msilwa watafurahi, sasa kuna haja gani ya watu kama hao kuja kwenye mazishi yangu.

“ASET ni kama simba wako tayari kukutafuna hadi macho, nimetafakari kwa muda mrefu sana nimevumilia mengi sana lakini nimeshindwa na sasa natamka rasmi, Nikifa wasinizike.”

Chocky ameorodhesha sababu nyingi sana za kufikia hatua hiyo lakini miongoni mwa sababu zake ni hizi tatu:

Kwanza kitendo cha Aset kumpeleka mahakamani kumdai gari, pili Aset kukataa kurudisha pesa za Miraji Shakashia na tatu ni ASET kutothamini michango ya wasanii walioizalishia pesa nyingi.

Chocky ansema kitendo cha Aset kumpeleka mahakamani kumdai gari ambalo walimpa mwenyewe kilimkera sana.

“Mtu anapokupeleka mahakamani maana yake ni kwamba yupo tayari hata ufungwe, ukifungwa maana yake ni kila kitu kwenye maisha yako kinaharibika.

“Gari walinipa wenyewe na maandishi yapo kwamba nikimaliza mkataba wangu gari litakuwa la kwangu.

Lakini badala yake wakanigeuzia kibao na kwenda kunidai mahakamani kwamba nimeiba gari.

Kuhusu Shakashia, Chocky amesema mwanamuziki huyo alichukua shilingi milioni tano za Extra Bongo ili ajiunge nayo na akasaini mkataba wake.

“Lakini badala yake Shakashia akaingia mitini na pesa zetu, Aset wakasema watazirudisha wao na sasa wanakuja na hadithi mpya.

“Wanasema hawawezi kurudisha hizo pesa eti kwa vile wananidai, wanasahau kuwa mkataba wa Shakashia ni kati yeke na Extra Bongo na sio Ally Chocky.

“Hata kama kipo wanachonidai hiyo ni kati ya Chocky na Aset na haiingii akilini kuliingiza suala la Shakashia ndani yake.

“Huu ni utapeli na inatoa picha kuwa Aset walimtumia Shakashia kufanya utapeli huu, lakini wajue kuwa mwisho wa siku atakayeathirika ni Shakashia mwenyewe,” alisema Chocky.

Kuhusu kutothamini wasanii waliozalishia pesa nyingi kampuni, Chocky anasema wasanii walipota ASET na kuizalishia pesa hawana chochote walichopewa kulingana na thamani ya kile walichokizalisha. “Sio pesa tu bali hata heshima pia hakuna,” alifafanua Chocky.

Chocky akazama zaidi na kuwataja wakongwe kama Shem Karenga na Kasongo Mpinda ambao waliwahi kufanya kazi katika familia ya kina Asha Baraka kupitia bendi za MK Group na MK Beats.

“Wako wapi Kasongo Mpinda na Shem Karenga, Kasongo aliwatengenezea pesa nyingi kupitia MK Group “Ngoma za Magorofani” huku Shem Karenga  akiwatengenezea utajiri katika MK Beats “Tukunyema”.

“Lakini hebu tujiulize wako wapi hawa wazee na wana kipi cha kujivunia?” alihoji Chocky.
 

 Haikuishia hapo, tuliamua kumpigia Asha Baraka ambaye naye alikuwa na yake ya kujibu kuhusu  mapigo ya Chocky.

Asha Baraka amesema hayo ni mambo ya kike na kwamba kuzikana si tija.

Asha Baraka akasema: “Hata mimi sina mpango wa kwenda kwenye mazishi yake na yeye pia asije kwenye mazishi yangu.

“Hivi kuzikana ni nini? Wazazi wangu walifariki na Chocky hakuja kuzika, kilipungua nini? Halafu mi nikifa sitaona na yeye akifa sitaona kwahiyo hiyo siyo ishu, wamanyema wenzangu watatosha kunizika hata wasanii wote wasipokuja achilia mbali huyo Chocky.

“Nilimzikia wazazi wake na hakuliona hilo kwahiyo hata tusipozikana hakipungui kitu.

“Chokcy tunamdai gari na pesa shilingi milioni 13, kwenda mahakamani ni sehemu ya kudai haki na yeye kama anaona amedhulumiwa kuhusu pesa za Shakashia basi aende mahakamani.”

Asha Baraka alimtaka Chocky aelewe kuwa baadhi ya wasanii wa Twanga ni virusi na watammalizia pesa zake bure.

“Wako wasanii wamelelewa vizuri, wamefanyiwa mengi na Twanga na wanaelewa utu kwahiyo akijipendekeza kwao atapoteza pesa zake bure.

“Hao ni virusi wetu, wanatuletea taarifa zote za kila mtu anapotaka kuwachukua.
Asha Baraka amesema kama ni roho mbaya Chocky ndio anaoongoza kwa roho mbaya.

“Alikaa yeye na kamati yake yenye wakiwemo mpaka wafanyakazi wa umma na kuzoa wanamuziki wa Twanga”

Anawataja wasanii wa Twanga waliowahi kuchukuliwa na Extra Bongo ni pamoja na Ferguson, Rogart Hegga, Hosea, Otilya, Nyamwela, Danger Boy, Aisha Madinda, Maria Soloma, Subrina pamoja na Kanuti ambaye baadae alirudisha pesa zao na kubakia Twanga.

Asha Baraka anawataja wasanii wengine wenye damu ya Aset ambao wako Extra Bongo ni Ephraim Joshua, Martin Kibosho, Athanas, Banza Stone na yeye mwenyewe Chocky.

“Kwa mfumo huo utaona wazi kuwa Extra Bongo inapumua kwa nguvu ya Aset lakini sisi hatujasema kitu, kama ni kutoa kauli ya kutozikana basi sisi ndio tulipaswa kuwa wa kwanza,” alifafanua Asha.

“Tunajua pia kuwa Chocky alihusika kushawishi usajili wa Chaz Baba Mashujaa Band akiamini kuwa kwa kuondoka Chaz Twanga itakufa,” aliongeza

Asha Baraka amemtaka Chocky aonyeshe mfano wa namna ya kulea wasanii kwa kuwapa maisha mazuri wanamuziki waandamizi kama Banza na Rogart.

“Asiangalie mambo ya Aset, ajitazame yeye anaishi vipi na Banza anaishi vipi, badala ya kutoa milioni tano kumnunua Shakashia, angemnunulia japo Corola Banza au Rogart.

“Chocky aitishe mkutano wa waandishi wa habari halafu mimi na yeye twende na mikataba ya wasanii inayoonyesha mishahara na marupurupu tuone nani analea vizuri wasanii.

“Mimi nilifanya kazi Bima na sijajengewa nyumba wala kununuliwa gari, silalamiki kwa kuwa haikuwa sehemu ya makubaliano yetu.

“Kama Chocky anadhani muziki unalipa kiasi cha kumnunulia kila mtu gari na nyumba basi atuonyeshe mfano kupitia Extra Bongo.

“Kila baya linalomfika basi mchawi ni Aset, mbona mimi naumwa mguu na sijawahi kusema ni Chocky?

“Chocky akapime afya yake apate ukweli, tunajua rekodi ya sehemu alizopita, sasa asije akadondoka akasema ni Aset …akapime kwanza” alimaliza Asha Baraka.Chanzo:saluti5.com

CHADEMA YAMNASA WAZIRI MULUGO KWA RUSHWA KATA MBALAMAZIWA WILAYA MUFINDI IRINGA.


 

 

 

 
 
 
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Phillip Mulugo.


CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemfikisha Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Phillip Mulugo, mbele ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa tuhuma za kutoa rushwa ya ahadi ya mifuko ya saruji na fedha taslimu 40,000 kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi.
Chama hicho pia kimemfungulia faili la tuhuma za ubakaji mgombea udiwani wa Chama cha Mapinduzi katika uchaguzi mdogo wa kata ya Mbalamaziwa, Zuberi Nyomolela, kwa kosa kuishi kinyumba na binti mwanafunzi.
Hayo yamesemwa jana katika kijiji cha Mbalamaziwa na mwanasheria wa CHADEMA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Sinkara Lucas, kwenye mkut ano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Mbalamaziwa, uliohudhuriwa na mwenyekiti wa chama hicho taifa, Freeman Mbowe.
“Ndugu zangu wakati wa kampeni hasa za nyumba kwa nyumba tulikuwa tunakutana na maneno maneno hivi yanazungumzwa kuhusu mgombea wa CCM, maneno mazito sana, sasa kama kawaida ya CHADEMA kama mnavyojua huwa hatukurupuki, tunafanyia kwanza vitu utafiti kabla hatujatoka hadharani kutuhumu; tunakuwa na ushahidi wa kutosha.
“Wananchi wa Mbalamaziwa ninyi ni mashahidi; majuzi alipita hapa Phillip Mulugo akatoa rushwa ya ahadi ya mifuko 20 ya saruji na fedha taslimu 40,000 eti kwa vijana wakanunue mipira lakini wamchague Zuberi…amefanya yote hayo hadharani hapa jukwaani, kinyume cha sheria za uchaguzi na sheria za nchi. Sasa tunao ushahidi na tumeupeleka TAKUKURU na hivi sasa wanalifanyia kazi faili hilo. Wakati wowote atakamatwa.
“Atakamatwa na faili linashughulikiwa. Wananchi wenzangu hiyo ndiyo CCM inayolea rushwa na ufisadi na huyo Zuberi naye itakula kwake…hajapata udiwani anafanya hivyo sasa akipata itakuwaje…?” alisema Lucas.
Akihutubia mkutano huo wa kampeni kumnadi mgombea wa udiwani kwa tiketi ya CHADEMA, Ezekia Ambangile Mlyuka, Mwenyekiti wa Taifa, Mbowe alisema vitendo vyovyote vya makosa ya jinai havistahili kuvumiliwa hivyo chama chake hakitakubali kuona vinafanyika, ikiwemo rushwa kwenye uchaguzi.
Mkutano huo uliohudhuriwa pia na wabunge Peter Msigwa, David Silinde, Mbowe mbali ya kuwapa pole kwa kufiwa na diwani aliyekuwepo, aliwaambia wananchi kuwa wasirudie makosa kwa kuichagua CCM, akisema kuwa imekuwa sababu na chanzo cha umaskini wa Watanzania.
Akitolea mifano namna kata hiyo ilivyo nyuma katika maendeleo kwa kukosa huduma za msingi za kijamii kama kukosa kituo cha afya, na zahanati kwa zaidi ya miaka 50 ya uhuru. Mbowe alisema ni wakati mwafaka wa kuanza kubadilisha uongozi.
Akijibu tuhuma hizo, Mulogo alikiri kutoa rushwa hiyo ya ahadi kwa sababu hakujua kama mkutano wa kampeni ulishafunguliwa.
“Mimi nilikuwa napita kwenda Mbeya, sikujua kama mkutano wa kampeni ulishafunguliwa ila niliwakuta watu wakiwa wamekusanyika na nikakumbuka kwamba niko katika kata ya mheshimiwa Menrad ambaye alishawahi kuniomba msaada wa mifuko ya saruji kwa ajili ya shule moja hivi katika kata yake. 
Niliahidi hivyo na nikasema nitatoa mifuko hiyo,” alisema Mulugo. Alipobanwa kwamba haoni kufanya hivyo ni kuvunja sheria, Mulugo alisisitiza kwamba hakujua kama mkutano wa kampeni ulishaanza.
Kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi, viongozi wa serikali hawaruhusiwi kutoa msaada wala ahadi wakati wa mikutano ya kampeni kwani kufanya hivyo ni rushwa. CHANZO TANZANIA DAIMA.