WATANZANIA TUMPE SUPPORT MISS TANZANIA HAPPINESS WATIMANYWA KWENYE SHINDANO LA MISS WORLD 2014


    Happiness Watimanywa (20) aliyekuwa Redds Miss Tanzania 2013 sasa yuko jijini London Uingereza kwa ajili ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss World 2014.
Happiness ambaye kwa sasa anashikilia taji la Miss World Tanzania 2014 amesema ana kila sababu ya kurudisha taji nyumbani ikiwa watanzania watamuunga mkono kwa kusambaza video zake katika mitandao mbalimbali ya kijamii.
“Hebu angalia uzuri wa taifa letu, amani, upendo na vivutio mbalimbali vya utalii. Hebu niangalie na mimi mwenyewe… tuna kila sababu ya kurudisha taji nyumbani.” alisema Happiness Watimanywa
Shime shime watanzania, tumuunge mkono wa nyumbani kwa ku-retweet, ku-like na ku-share post zake mbalimbali kwa kutumia Hashtag #Happiness4MissWorld

Soma Taarifa ya VIP Engineering and Marketing Ltd: Umiliki wa fedha za escrow hauna utata, tatizo ni Mawakili


read more

Kutoka Gazeti la Mwananchi LEO: Siku moja baada ya Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), Nimrod Mkono kusema amelishwa sumu akiwa London, Uingereza, Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee amemtaka kusema ukweli na si kulihadaa Taifa kwa uongo.


Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee.
  Siku moja baada ya Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), Nimrod Mkono kusema amelishwa sumu akiwa London, Uingereza, Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee amemtaka kusema ukweli na si kulihadaa Taifa kwa uongo.
Mkono akizungumza na waandishi wa habari juzi kuelezea mwenendo wa afya yake, alisema lengo la kulishwa sumu ilikuwa ni kutaka kuharibu figo zake ndani ya saa 72 kitendo kilichoshindikana.
Mdee aliyekuwa na Mkono katika ziara hiyo alisema: “Hakuna ukweli wowote kwamba alilishwa sumu, nilikuwa naye kule na mazingira aliyoanza kuumwa hadi kupona kwake ni utata… awaeleze Watanzania anaumwa nini na si kusema alilishwa sumu.
“Nilikaa kimya baada ya kuripotiwa na gazeti moja (The Citizen) kwamba Mkono kalishwa sumu, sasa amezungumza tena nikaona si busara kukaa kimya wakati alilidanganya Taifa. Mkono waeleze ukweli watu mbona unawadanganya.”
read more

PINDA AHUDHURIA SHEREHE ZA KUMWEKA WAKFU ASKOFU WA ANGLICAN DODOMA


 

unnamedWaziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Maaskofu wa kanisa la Anglican nchini bada ya kuwasili kwnye Kanisa lao Kuu mjini  Dodoma kuhudhuria ibada ya kumweka wakfu Askofu wa Dayosisi ya Central Tanganyika,Dkt. Dickson Chilongani Novemba 23, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

unnamed1Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi zawadi ya picha Askofu  wa Dayosisi ya Central Tanganyika,Dkt. Dickson Chilongani katika ibada ya kumweka wakfu  Askofu huyo iliyofanyika kwenye kanisa kuu la Anglican mjini Dodoma Novemba 23, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

unnamed4Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na washiriki wa ibada ya kumweka wakfu, Askofu wa Da yosisi ya Central Tanganyika,Dkt. Dickson Chilongani   kwenye  kanisa Kuu la Anglican mjini Dodoma  Novemba 23, 2014.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

unnamed Baadhi ya washiriki wa  Ibada ya  kumweka wakfu Askofu wa Dayosisi ya Central Tanganyika,Dkt. Dickson Chilongani  wakimsikiliza Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati alipozungumza kwenye ibada hiyo iliyofanyika kwenye kanisa Kuu la Anglican mjini Dodoma  Novemba 23, 2014.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

TARATIBU ZA TIBA YA RAIS MH. JAKAYA MRISHO KIKWETE ZAKAMILIKA


D92A4106

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoka katika hospitali ya Johns
Hopkins iliyopo Baltimore Maryland baada ya kutolewa nyuzi katika
mshono baada ya kufanyiwa upasuaji wiki iliyopita.Rais Kikwete
anatarajiwa kurudi tena hospitalini hapo Jumatatu kwa ukaguzi wa
maendeleo ya kidonda na ushauri .Kulia kwake ni Daktari wa Rais
Profesa .Mohamed Janabi

………………………………………………………………….

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI LEO

Taratibu za matibabu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, zimekamilika leo, Jumatatu, Novemba 24, 2014.

Taratibu hizo za matibabu za Mheshimiwa Rais Kikwete zimekamilika kiasi cha saa 12 asubuhi ya leo wakati madaktari bingwa katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko mjini Baltimore, Jimbo la Maryland, Marekani, walipomfanyia hatua ya mwisho ya tiba.

Hata hivyo, Rais Kikwete ataendelea kupumzika na kuangaliwa kwenye Hoteli Maalum inayohusiana na Hospitali ya Johns Hopkins kwa siku mbili hadi tatu kabla ya kuanza safari ya kurejea nyumbani.

Kama kila kitu kitakwenda kama ilivyopangwa na madaktari, Rais Kikwete anatarajiwa kurejea nyumbani Jumamosi, Novemba 29, 2014.

Rais Kikwete aliondoka nchini Alhamisi ya Novemba 6, 2014, kwenda kufanyiwa uchunguzi wa afya yake lakini madaktari katika Hospitali ya Johns Hopkins waliamua kumfanyia upasuaji wa tezi dume Jumamosi ya Novemba 8, 2014.

Rais Kikwete anaendelea kuwashukuru Watanzania kwa sala na maombi yao ya kumtakia heri ya kupona haraka na kurejesha afya njema katika kipindi chote cha ugonjwa wake.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
24 Novemba,2014

MKUSANYIKO WA U12 DAR ES SALAAM


 

Watoto wenye umri chini ya miaka 12 wa Mkoa wa Dar es Salaam wanakusanyika kesho Jumamosi (Novemba 22 mwaka huu) asubuhi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume kwa ajili ya kusaka kombaini ya mkoa.

 Mkusanyiko wa kusaka kombaini hiyo kwa ajili ya timu itakayoshiriki mashindano ya Taifa yatakayofanyika mwishoni mwa mwezi ujao uko chini ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA).

 Wachezaji hao wataanza kujaribiwa saa 1 hadi saa 5 asubuhi. Mashindano ya Taifa yatafanyika jijini Mwanza kuanzia Desemba 28 mwaka huu.

 IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

No judiciary interference in IPTL saga


 

Bunge told The Judiciary has not written any formal letter to Parliament aimed at discouraging the tabling of Controller and Auditor General’s (CAG) report on IPTL saga in the House. bunge tanzania Bunge Tanzania Parliamentary Chairman Idd Zungu told Members of Parliament during the morning session on Friday that rumours that the Judiciary had interfered with the working of Parliament, by writing to ask the House not to debate the details of the report were false. “The rumours that have gone here during the last few days that the Judiciary had written to Parliament are not true. Please desist from repeating that rumour. The two organs, Parliament and Judiciary have a good working relationship,” he said. He moved to remove the rumour that was growing to have some legitimacy even as there had not been official communication confirming receipt of the letter. Some MPs had viewed it as manipulation by the Executive to undermine the supremacy of the House in discussing the CAG and the Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB) reports. The Tegeta escrow scandal revolves around a questionable withdrawal, from the central bank of whopping 306bn/- in taxpayer’s money that was shared among few individuals working with government and others in the private sector. Read more »