MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA WIKI YA MAZINGIRA DUNIANI KWA KUPANDA MITI KATIKA KAMBI YA KIKOSI CHA JESHI LA KUJENGA TAIFA RUVU


001 (2) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohameed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Mazingira Duniani, wakati alipofika kwenye Kambi ya JKT Ruvu kwa ajili ya kupanda miti ikiwa ni sehemu ya uzinduzi huo, ambapo jumla ya miti 8,000, imeandaliwa kupandwa katika eneo hilo. Picha na OMR
2 (6) Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantum Mahiza, akipanda mti katika eneo la Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa, JKT Ruvu, ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa Wiki ya mazingira Duniani. jumla ya miti 8,000 inatarajia kupandwa katika eneo hilo. Picha na OMR
01 (5)Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiumwagia maji mti alioupanda katika eneo la Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa, JKT Ruvu, ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa Wiki ya mazingira Duniani. jumla ya miti 8,000 inatarajia kupandwa katika eneo hilo. Picha na OMR
3 (5) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Jiwe la msingi baada ya kupanda mti katika eneo la Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa, JKT Ruvu, ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa Wiki ya mazingira Duniani. jumla ya miti 8,000 inatarajia kupandwa katika eneo hilo. Picha na OMR
4 (4) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Jeshi wa kambi ya JKT Ruvu baada ya kupanda miti. Picha na OMR
5 (1) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi walio katika mpango maalum wa kampeni ya upandaji miti hiyo, baada ya kupanda miti. Picha na OMR
22W

Maalim Seif awaasa wagombea uongozi CUF: Msikubali kununuliwa


 

 
Na Haji Nassor, PEMBA
 
KATIBU mkuu wa Chama cha wananchi CUF Zanzibar Mhe: maalim Seif Sharif Hamad, amewataka wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya ya Mkoani wa chama hicho, wasikubali kununuliwa na wagombea nafasi mbali mbali, na badala yake wawachague viongozi kwa kuwaona wanafaa.
 
KATIBU mkuu wa CUF Mhe: maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya ya Mkoani Pemba wa chama hicho, ambao uliambatana na uchaguzi mkuu wa wilaya, uliofanyika Jimbo la Mtambile jana (picha na Haji Nassor, Pemba)
 
Alisema ni kweli wapo baadhi ya wagombea wa nafasi zinazogombewa wamekuwa wakimwaga pesa kwa wajumbe hao, na endapo watazichukua na kisha kuwapa kura kutokana na fedha hizo, waelewa kuwa chama kitaanza kudhoofika.
 
Maalim Seif ametoa kauli hiyo jana Mtambile wilaya ya Mkoani Pemba, wakati alipokua akifungua mkutano mkuu wa wilaya, ulioambatana na uchaguzi wa kuwachagua viongozi mbali mbali akiwemo Katibu, Mwenyekiti na wajumbe wa mkutano kuu taifa CUF taifa.
 
Alisema ni vyema wajumbe hao kuwa makini na kujitenga mbali na wagombea wenye nia ya kusambaaza fedha, kwao kwa ajili ya kuwapigia kura wakijua kuwa viongozi wa aina hiyo hawana nia thabiti na chama.
 
Alieleza kuwa ni vyema kuwachagua viongozi ambao ni wapiganaji wa kweli na ambao wataweza mapambano na vyama vyengine katika uchaguzi mkuu ujao, ili kuendelea kushika hatamu wa nafasi mbali mbali ikiwa ni pamoja udiwani, uwakilishi na ubunge.
 
‘’Mimi niwanasihi sana ndugu wajumbe wa mkutano huu, ambao ndio wapiga kura wa kuwachagua viongozi, lakini muelewa kuwa mkiwachagua viongozi legeleg ndio mnakidhoofisha chama, na mkiwa makini ndio kusema CUF inaweza kushinda hata ngazi ya raisi’’,alifafanua.
 
 

MADUDU KATIKA ELIMU YAENDELEA


 

WABUNGE wamesema hali ya elimu nchini ni mbaya na kumshauri Rais Jakaya Kikwete, kuunda Tume ya Kudumu ya Elimu ili kuangalia ubora na kudhibiti sekta hiyo muhimu.

Katika michango yao kwenye mjadala wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, uliotarajiwa kuhitimishwa jana jioni, wabunge wamesema suala la elimu halina siasa, na nchi isipochukua hatua sasa, itakuwa hatari kwa vizazi vijavyo.

Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia (NCCR-Mageuzi), alieleza matatizo kadhaa katika mitihani ya Darasa la Saba pamoja na ule wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) na kudai kuwa “kuna madudu makubwa.”(Martha Magessa)

Mbatia aliyekuwa ameshika nakala za mitihani hiyo na baadaye kuiwasilisha kwa Naibu Spika, Job Ndugai, alidai baadhi ya mitihani hiyo ni migumu na imewashinda maprofesa wa vyuo vikuu.

Profesa, dau “Mimi niliwapatia mitihani hii maprofesa wa vyuo vikuu, imewashinda. Niliwapa huu wa Hisabati, akanirudishia akisema mtihani wenyewe haufanyiki. “Sasa kama yupo mtu humu atamudu kuufanya na kupata alama mia moja, nampa milioni kumi,” alisema Mbatia, huku Naibu Spika akieleza kuwa Waziri Profesa Sospeter Muhongo yuko tayari kuufanya. “Profesa Muhongo ni profesa wa miamba, kama ataweza huu hapa aje achukue,” alitamba Mbatia.

Mbatia alisema elimu ya Tanzania ni dhaifu na nchi imeshindwa katika elimu na kuwa suala hilo si la chama cha siasa.

Akitoa majawabu ya hoja zake, Mbatia alimshauri Rais kuunda Tume ya Kudumu ya Elimu, ambayo pamoja na mambo mengine, alisema itaangalia ubora na kudhibiti elimu nchini.

Msomi huyo alitaka pia Tume hiyo ifanye kazi ya kuandaa mitaala, kuhariri vitabu akisema Tanzania haina wahariri wa vitabu kama ilivyo kwa vyombo vya habari vyenye wahariri wa aina mbalimbali.

Alizitaja kazi nyingine kuwa ni kufanya utafiti wa kisayansi, kuamua lugha ya kufundishia na kuangalia kwa ujumla tatizo la kushuka kwa elimu.

Alisema elimu siyo bidhaa ya kuuzwa sokoni, bali iwe huduma na kukerwa na kodi nyingi katika elimu na gharama za ada kwa shule binafsi.

“Ni lazima tuukubali ukweli na kukabiliana nao. Elimu yetu imeshuka. Watoto wa walalahoi watapata tabu, kama hatukuisimamia hili, tutapata tabu katika miaka 20 au mia ijayo hasa wakati huu wa sayansi na teknolojia,” alisema Mbatia.

Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba (CCM), aliyesema kuwa elimu iko katika chumba cha wagonjwa wenye uangalizi maalumu (ICU). Kama Mbatia, Serukamba alishauri kuanzishwa kwa Tume ya kujichunguza kuhusu kuporomoka kwa elimu nchini, akisema “tukubali waseme, tujisahihishe.”

Alisema suala hilo si la mtu mmoja, na kuacha siasa na kuongeza kuwa kama kuna jambo “tunacheza nalo, basi ni elimu, tunaua kizazi kijacho.”

Alisema si vyema kutatua tatizo la elimu kwa kuangalia leo tu, bali uwepo mkakati wa dhati wa muda mrefu, na kutolea mfano Marekani ilivyopitia mfumo wake wa elimu mwaka 1981.

Ada kubwa Kwa upande wake, Mbunge wa Bukoba Vijijini, Jason Rweikiza (CCM), ambaye anamiliki shule kadhaa nchini, alisema kuna tatizo la shule binafsi kulundikiwa kodi nyingi, na ndio manaa zinatoza ada kubwa.

“Kuna sijui kodi ya mapato, PAYE, majengo, SDL, yaani ni michango, michango, kodi. Kwa staili hii, ada inapanda, baadaye shule inakufa,” alisema Rweikiza.

Aidha, kama walivyopendekeza wabunge wengine waliochangia jana, mbunge huyo alitaka ukaguzi utiliwe mkazo, akitoa mfano kuwa shule zake hazijakaguliwa tangu mwaka 2005.

Mbunge wa Ngara, Deogratius Ntukamazina (CCM), alisema kwa sasa hakuna Wizara ya Elimu baada ya kuondolewa kwa shule za msingi na sekondari.

Badala yake, akashauri wizara hiyo ibaki kuwa kitovu cha mawazo bora ya elimu kama ilivyo Tume ya Mipango kuhusu masuala ya mipango.

Said Arfi wa Mpanda Mjini (Chadema), licha ya kuzungumzia ukaguzi, alisema bajeti ya elimu imezidi kutegemea wahisani ambao hawatekelezi ahadi zao.

Nyambari Nyangwine wa Tarime (CCM), ambaye ni mtunzi wa vitabu, alipendekeza kuanzishwa kwa Shirika la Uchapaji, kwani vitabu ni moja ya maeneo yanayochangia mporomoko wa elimu nchini.

Mbunge wa Viti Maalumu, Magdalena Sakaya (CUF) alisema mazingira mabovu, ukaguzi kuachwa, shule kukosa maabara na kushuka kwa morali ya walimu, kumechangia kushuka kwa elimu nchini.

Muundo Mbunge wa Kilolo, Profesa Peter Msolla (CCM), alitaka masuala ya shule za msingi na sekondari yabaki katika wizara hiyo na irejeshwe wizara ya kusimamia elimu ya juu, huku akisisitiza kuwa upangaji madaraja ni angamizo katika elimu nchini.

Naibu Spika Ndugai naye alipendekeza masuala ya elimu yaondolewe Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na kurejeshwa kwa wizara hiyo ili yasimamiwe vyema.

Kambi Rasmi ya Upinzani ilisema kuwa malengo na mikakati yote iliyoainishwa ni mizuri, lakini “tunadhani mikakati hiyo imekuwepo muda mrefu, kilichokosekana ni utekelezaji na ufuatiliaji wake.”

Msemaji wake, Susan Lyimo alishauri mikataba ya utendaji kazi katika kila ngazi ya elimu iwekwe wazi ili atakayeshindwa kutekeleza wajibu wake ijulikane atawajibika vipi.

CHANZO:HABARILEO

DKT. SHEIN AONGOZA UFUNGAJI WA MAFUNZO YA MAAFISA KMKM


IMG_9890 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mkuu KMKM alipowasili katika kambi ya KMKM Kama katika ufungaji wa Mafunzo Maalum ya Maafisa (Special Duty) mkupuo wa saba(7) leo,(katikti) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Haji Omar Kheri.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
IMG_9908 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akipokea salamu ya hesha ya gwaride la Maafisa wakati ufungaji wa Mafunzo Maalum ya Maafisa (Special Duty) mkupuo wa saba(7) katika kambi ya KMKM Kama  Wilaya ya Magharibi Unguja leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
IMG_9925Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akikagua gwaride la Maalum wakati wa ufungaji wa Mafunzo Maalum ya Maafisa (Special Duty) mkupuo wa saba(7) katika kambi ya KMKM Kama  Wilaya ya Magharibi Unguja leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]IMG_9979Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein alipokuwa akiwatunuku  Kamisheni Maafisa Wanafunzi waliohitimu mafunzo ya awali katika kambi ya KmKm kama leo,alipoyafunga mafunzo hayo katika mkupuo wa saba (7) wilaya ya Magharibi Unguja.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]IMG_9878Makamanda wa KmKm waliohudhuria katika sherehe za ufungaji wa Mafunzo Maalum ya Maafisa (Special Duty) mkupuo wa saba(7) katika kambi ya KMKM Kama  Wilaya ya Magharibi Unguja leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.] 

IMG_9880Baadhi ya wananchi walioalikwa katika hafla ya sherehe za ufungaji wa Mafunzo Maalum ya Maafisa (Special Duty) mkupuo wa saba(7) katika kambi ya KMKM Kama  Wilaya ya Magharibi Unguja leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.] 

KUHUSU MAADHIMISHO YA SIKU YA FAMILIA DUNIANI ITAKAYOADHIMISHWA TAREHE 15/5/2014


1 (8) 2 (8)Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia waanguzi   na wananchi kwenye sherehe za waauguzi duniani ambazo kitaifa zimefanyika Mjini Arusha katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid leo Tarehe.12.05.2014(picha na Freddy Maro).

Wauguzi Washerekea siku yao Mjini Arusha

1 (7) Baadhi ya wauguzi waliohudhuria sherehe za siku ya wauguzi duniani wakifuatilia kwa makini Hotuba ya mgeni rasmi,rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete mjini Arusha leo(picha na freddy maro)2 (7)Baadhi ya Wauguzi wakila kiapo cha uaminifu na kutunza siri za wagonjwa wakati wa maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani yaliyofanyika katika uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha leo.

Rais Kikwete awahutubia wauguzi Arusha


1 (8) 2 (8)Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia waanguzi   na wananchi kwenye sherehe za waauguzi duniani ambazo kitaifa zimefanyika Mjini Arusha katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid leo Tarehe.12.05.2014(picha na Freddy Maro).

Wauguzi Washerekea siku yao Mjini Arusha

1 (7) Baadhi ya wauguzi waliohudhuria sherehe za siku ya wauguzi duniani wakifuatilia kwa makini Hotuba ya mgeni rasmi,rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete mjini Arusha leo(picha na freddy maro)2 (7)Baadhi ya Wauguzi wakila kiapo cha uaminifu na kutunza siri za wagonjwa wakati wa maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani yaliyofanyika katika uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha leo.

Picha Maalum Kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa:Tazama Matukio Mbalimbali ya Ziara ya Kikazi ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe nchini Uturuki


 
 
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe akisalimiana na Naibu Meya wa jiji la Ankara ambaye naye alikuja Uwanja wa Ndege kumlaki
Waziri Membe kushoto akibadilishana mawazo na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania katika Chumba cha Wageni Maalum kwenye Uwanja wa Ndege wa Ankara
 Naibu Meya wa jiji la Ankara aliyeketi kushoto akibadilishana mawazo na Mhe. Membe kabala ya kuondoka kutoka katika kiwanja hicho
 Waziri Membe akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Italia ambaye pia anawakilisha Uturuki aliyekaa kushoto pamoja na Bw. Salvator Mbilinyi, Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Italia aliyechutama wakibadilishana machache katika Chumba cha Wageni Maalum ndani ya Uwanja wa Ndege wa Ankara.
 Waziri Membe akiendelea kuwahutubia waandishi wa habari hawapo pichani
 Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Mhe. Bernard K. Membe akihutubia Mkutano wa Waandishi wa Habari huku akimshika mkono Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Mhe. Almet Dovutoglu
 
 
Waziri Membe kulia akishikana mkono na Waziri Mkuu wa Uturuki mara baada ya viongozi hao kumaliza mazungumzo.
 Waziri Mkuu wa Uturuki, Mhe. Recep Tayyip Erdogan (kulia) akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania, Mhe. Bernard K. Membe (Mb). mazungumzo hayo yalifanyika katika Ofisi ya Waziri Mkuu mjini Ankara, Uturuki tarehe 08 Mei, 2014.