SITTA APOKEA MESEJI ZA MATUSI


sssita_88efd.jpg

Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, Samuel Sitta amesema anapokea meseji za simu zaidi ya 50 kwa siku za kumtukana na kusisitiza ataendelea kupambana kuhakikisha Katiba inayopendekezwa inapatikana.

Sitta alitoa kauli hiyo bungeni mjini Dodoma jana wakati akielezea kutoridhishwa kwake na kile alichodai ni namna hukumu ya kesi iliyofunguliwa na Saed Kubenea inavyopotoshwa na wanaomchukia.

“Kuna baadhi ya vyombo vya habari wananichukia mimi binafsi. Wasichanganye chuki hizo na mchakato wa Bunge Maalumu,” alisema Sitta na kuongeza;

“Mimi napokea matusi kila siku. Meseji zisizopungua 50 viongozi wa Chadema wameweka namba zangu katika tovuti nitukanwe kila siku hilo mimi niko tayari na mnaniona niko safi tu wala sihangaiki nalo.”

“Lakini sasa Bunge Maalumu ni chombo cha kikatiba, kiko tofauti na mwenyekiti wake. Huwezi kuliadhibu Bunge Maalumu kwa sababu hupendi sura ya mwenyekiti wake,” alisema.(P.T)

Read more…

BUNGE MAALUM LA KATIBA LAPENDEKEZA MAKAMU WA TATU WA RAIS


bungepic_0d073.jpg

Na Mwandishi wetu_MAELEZO_Dodoma

Bunge Maalum la Katiba limependekeza muundo wa uongozi wa Serikali utakuwa na Makamu watatu wa Rais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania.

Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi wa Bunge Maalum la Katiba,Mhe. Andrew Chenge wakati akiwasilisha Rasimu ya Katiba inayopendekezwa wakati wa kikao cha arobaini na mbili cha Bunge hilo.

Amesema kuwa katika mapendekezo hayo mgombea mwenza ndio atabaki kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais, na kwa upande wa Rais wa Zanzibar atakuwa Makamu wa Pili na Waziri Mkuu atakuwa Makamu wa tatu wa Rais.(P.T)

Read more…

MKATABA WA MOSOTI, SIMBA UMEVUNJWA – FIFA


SIMBA6

Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Mrisho Ngassa (17), akimpiga chenga aliyekuwa beki wa  Simba, Mkenya, Donald Mtosi wakati mchezo wao wa Nani Mtani Jembe mwezi Desemba  mwaka jana

Na Bertha Lumala, Dar es Salaam

Wakati uongozi wa Simba ukidai kuwa bado una mkataba na beki Mkenya Donald Mosoti, Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limeitaka klabu hiyo kumlipa fidia beki kwa kuwa mkataba wake umevunjwa.

Katibu Mkuu wa Simba, Stephen Ally alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini jana akisema kuwa Mosoti bado ni mchezaji wao halali kwa vile mkataba kati yao na mchezaji huyo badi haujavunjwa.

Donaldi Mosoti akiwa kazini enzi zake Simba sc

Klabu hiyo kongwe nchini, iliamua kumwacha beki huyo dakika za mwisho za usajili msimu huu ili kumsajili Emmanuel Okwi aliyevunja mkataba wake na Yanga huku mwanasheria wa Mosoti, Felix Majani akidai kuwa uamuzi huo ulifanywa bila kumshirikisha mteja wake.(P.T)

Read more…

LIVERPOOL YABANWA 2-2, YATOKEA KWENYE PENALTI 14-13 ANFIELD


Mario Balotelli akipambana jana Anfield

KLABU ya Liverpool imeifunga Middlesbrough kwa penalti 14-13 katika Raundi ya Tatu ya Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One Cup kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 120 Uwanja wa Anfield.

Kinda Jordan Rossiter alianza kuwafungia Wekundu hao baada ya kupewa nafasi ya kwanza kuchezea kikosi cha kwanza, kabla ya Adam Reach kuwasawazishia wageni akimalizia pasi ya Grant Leadbitter.

Mchezo huo ulihamia kwenye muda wa nyongeza kufuatia timu kumaliza zikiwa zimefungana 1-1 baada ya dakika 90.(P.T)

Read more…

Kikwete addresses UN General Assembly on Tuesday


President Jakaya Kikwete on Monday started a series of meetings that will take a week at the UN General Assembly and other bilateral sessions here in New York.

President Jakaya Kikwete
The president, who arrived in New York from Washington DC at the weekend together with First Lady Salma Kikwete, will attend various meetings including those involving security.
On Tuesday, the president will attend the opening plenary of the 2014 Climate Summit for Heads of State and Government. Tomorrow, he will address the UN General Assembly.
The First Lady, on her part, will also attend a meeting for all the First Ladies focusing on maternal and new born health with special emphasis on adolescent girls. Meanwhile, Tanzanians living in New York were among the 300,000 people who took part in the international day of action on climate change in the city here throughout Sunday.
The demonstration, which started on 86 Central Park West, down to 59 Central Park South, to the Avenue of America exceeded organizers’ hopes for the largest protest on the issue in history.
One of the Tanzanians in the procession, Mr Abdul Salim, said their participation was part of their contribution to the global cause to address climate change across different countries.

Wajumbe wa Z’bar watishwa


Na Daniel Mjema, Mwananchi

Dodoma. Hali imeanza kuwa tete Bunge la Katiba kutokana na ujumbe unaosambazwa kwa kasi katika mitandao ya kijamii, ili kuwagombanisha na kuwafitinisha wajumbe wa kundi la 201 kutoka Zanzibar.

Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha-Rose Migiro.PICHA|MAKTABA

Ujumbe huo ambao gazeti hili limeuona, ulianza kusambazwa juzi, ukiwataka wajumbe wa kundi la 201 kutoka Zanzibar, kuondoka bungeni ili theluthi mbili ya Katiba inayopendekezwa isipatikane.

Upigaji wa kura kulingana na masharti ya Ibara ya 37 ya kanuni za Bunge Maalumu la Katiba, unatarajiwa kuanza Septemba 29 na kukamilika Oktoba 2 mwaka huu.
Hata hivyo, taarifa nyingine zimedai ujumbe huo unatumwa na baadhi ya wanaCCM kama mbinu ya kuwakatisha tamaa kundi la 201 wanaoonekana kuwa na msimamo thabiti ili hatimaye warudi upande wa CCM kwa kuona wamenyanyapaliwa.
Ujumbe huo unaaminika unaweza kuwa ni sehemu ya propaganda kutoka kwa baadhi ya wanaCCM kutoka Maskani ya Kisonge Zanzibar ili wajumbe hao waanze kusalitiana na wale wenye msimamo wajenge chuki na kusalimu amri.
“Tunawaambia wazi wajumbe hao wa kundi la 201 watoke katika Bunge la Katiba mara moja kabla ya upigaji wa kura vinginevyo hatutawaelewa,” unasomeka ujumbe huo wa WhatsApp na kuongeza;
“Hatuhitaji wapige kura ya siri wala ya wazi. Tunachohitaji ni theluthi mbili ya Zanzibar isipatikane kabla hata ya huo upigaji wa kura”, unasomeka ujumbe huo ambao umeweka picha za baadhi ya wajumbe baadhi ya wanaCCM kama mbinu ya kuwakatisha tamaa kundi la 201 wanaoonekana kuwa na msimamo thabiti ili hatimaye warudi upande wa CCM kwa kuona wamenyanyapaliwa.

Ban ataka kukomeshwa mashambulizi ya Daesh Syria


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametaka kusitishwa mara moja mchafuko yanayofanywa na kundi la kigaidi la Daesh huko Syria.
Msemaji wa Ban Ki moon ameeleza kuwa, Ban anafuatilia kwa karibu hujuma zinazoendelea kufanywa na kundi hilo la kigaidi katika mji wa Ayn al Arab kaskazini mwa Syria.
Taarifa ya msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa imeongeza kuwa, machafuko yanayojiri katika mji wa Ayn al Arab huko kaskazini mwa Syria yamewapelekea maelfu ya raia kuyahama makazi yao.
Numan Kurtulmus, Naibu Waziri Mkuu wa Uturuki amesema kuwa, Wakurdi wa Syria wasiopungua elfu sitini wamevuka mpaka na kuingia Uturuki tangu Ijumaa iliyopita wakiwahofia mashambulizi ya kundi la kitakfiri la Daesh.
Daesh wameviteka vijiji zaidi ya 20 huko kaskazini mwa Syria karibu na eneo la Wakurdi la Ayn al Arab ambalo hujulikana pia kwa jina la Kobane.

Balozi Sefue afunguka Katiba Mpya


Na Elias Msuya, Mwananchi

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue amesema hakuna uwezekano wa kubadili muundo wa muungano kutoka Serikali mbili kwenda Serikali tatu katika mchakato wa Katiba.

Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue.

Kauli ya Balozi Sefue imekuja ikiwa ni siku chache tangu Rais Jakaya Kikwete kukutana na viongozi wa Kituo cha Demokrasia (TCD) na kutoa uamuzi wa kuahirisha mchakato wa Katiba hadi baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Suala la muundo wa muungano lilichukua mjadala mkali ndani ya Bunge Maalumu la Katiba huku wajumbe wanaounda kundi la Ukawa wakiunga mkono mapendekezo ya Rasimu ya Katiba ya muundo wa Serikali tatu na wajumbe wa CCM wakisisitiza muundo wa Serikali mbili.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili, Balozi Sefue alisema mchakato wa Katiba unahitaji maridhiano, lakini suala la muundo wa muungano halina maridhiano katika jamii hivyo litachelewesha upatikanaji wa Katiba:
“Katika historia ya nchi yoyote, wakati unafika wananchi wakawa na maridhiano fulani, wakaamua kuyaingiza ndani ya Katiba. Tatizo linajitokeza pale watu au makundi fulani yanapong’ang’ania kuingiza ndani ya Katiba mambo ambayo ni dhahiri hayana maridhiano ndani ya jamii. Mfano ni suala la muundo wa Muungano,” alisema na kuongeza:
“Uzoefu wa Bunge Maalumu hadi sasa ni kuwa hakuna uwezekano wa kupata maridhiano ya kubadili muundo wa Muungano kutoka Serikali mbili kwenda tatu. Hutapata maridhiano hayo ndani ya Bunge Maalumu na hutapata maridhiano ukienda kwa wananchi,” alisema.

Uhuru Kenyatta atakiwa mahakamani ICC 8,Octoba


Raisi wa Kenya Uhuru Kenyatta atakiwa ICC tarehe 8 Octoba
Raisi wa Kenya Uhuru Kenyatta atakiwa ICC
tarehe 8 OctobaREUTERS/Noor Khamis
Na Martha Saranga Amini
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imemtaka raisi wa Kenya Uhuru Kenyatta kufika mahakamani tarehe 8 mwezi Oktoba licha ya majaji wanaotarajiwa kusikiliza kesi dhidi yake kuiahirisha.
majaji katika mahakama hiyo wanataka kumhoji juu ya madai kwamba serikali yake imeficha hati iliyoombwa na waendesha mashitaka wanaosikiliza kesi yake ya uhalifu dhidi ya ubinadamu.
Kesi hii imekuwa ikicheleweshwa mara kadhaa sasa.hata hivyo raisi kenyata amekanusha kuandaa mauaji ya kikabila baada ya uchaguzi mwaka 2007.
Takribani watu elfu moja mia mbili waliuawa na laki sita kuyakimbia makazi yao.
Wiki mbili zilizopita, waendesha mashitaka waliomba kesi dhidi yake kuahirishwa kwa muda usiojulikana, kwa vile hawakuwa na ushahidi wa kutosha kwa sababu ya serikali ya Kenya kuweka vizuizi.