ZIARA YA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA BAJETI KATIKA VISIMA VYA GESI ASILIA, MADIMBA

Picha Na 1
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evodi Mmanda (mbele) akizungumza na  wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, kabla ya kuanza kwa ziara katika miradi mbalimbali ya gesi asilia iliyopo mkoani humo.
Picha Na 2
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Hawa Ghasia (kulia) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kushoto mbele) wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na  Meneja wa Kiwanda cha Kuchakata Gesi Asilia cha Madimba kilichopo Mtwara, Leonce Mroso (hayupo pichani) kwenye  eneo la kiwanda hicho katika ziara hiyo. Katikati nyuma ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Jaji Mstaafu, Josephat Mackanja.
Picha Na 3
Sehemu ya mitambo ya Kiwanda cha Kuchakata Gesi cha Mnazi Bay kilichopo mkoani Mtwara
Picha Na 4
Mtaalam kutoka Kiwanda cha Kuchakata Gesi Asilia cha Mnazi Bay kilichopo mkoani Mtwara, Laurent Jars (katikati) akielezea shughuli za uchakataji wa gesi zinavyofanywa na kiwanda hicho kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti.
  Picha Na 5
Mtaalam kutoka Kiwanda cha Kuchakata Gesi Asilia cha Mnazi Bay kilichopo mkoani Mtwara, Nyomwa Kilemo (katikati) akifafanua jambo kwa  wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kwenye ziara hiyo.
Picha Na 6
Mtaalam kutoka Kiwanda cha Kuchakata Gesi Asilia cha Mnazi Bay kilichopo mkoani Mtwara, Laurent Jars (kulia) akifafanua jambo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kushoto) kwenye ziara hiyo.
Picha Na 7
Mtaalam kutoka Kiwanda cha Kuchakata Gesi Asilia cha Mnazi Bay kilichopo mkoani Mtwara, Laurent Jars (kushoto) akielezea usafirishaji wa gesi asilia kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Hawa Ghasia (kulia) katika ziara hiyo.
Picha Na 8
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Hawa Ghasia (katikati) akionesha wajumbe wa kamati hiyo  sehemu ya eneo la Pwani lililomegwa na maji karibu na Kiwanda cha Kuchakata Gesi Asilia cha Mnazi Bay kilichopo mkoani Mtwara kwenye ziara hiyo.
Picha Na 9
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Hawa Ghasia (kulia mbele) akielezea manufaa ya gesi asilia kwenye uchumi wa mkoa wa Mtwara kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kwenye ziara hiyo.
Picha Na 10
Sehemu ya mitambo ya Kiwanda cha Kuchakata Gesi Asilia cha Madimba  kilichopo mkoani Mtwara.
Picha Na 11
Meneja wa Kiwanda cha Kuchakata Gesi Asilia cha Madimba kilichopo Mtwara, Leonce Mroso (kulia) akielezea matumizi ya  gesi asilia kwenye uzalishaji wa umeme kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kwenye eneo la kiwanda hicho.
Picha Na 12
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Hawa Ghasia (wa tatu kulia mbele) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo ( wa pili kulia mbele) wakiongoza wajumbe wa kamati hiyo kwenye ziara katika eneo la Kiwanda cha Kuchakata Gesi Asilia cha Madimba kilichopo mkoani Mtwara.
……………………..
Wataalam Madimba watakiwa kuwa wazalendo
Na Greyson Mwase, Mtwara
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Hawa Ghasia amewataka  vijana wanaofanya kazi katika Kiwanda cha Kuchakata Gesi Asilia cha Madimba kilichopo mkoani Mtwara kuwa wazalendo na kufanya kazi kwa weledi, hivyo kuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi kupitia sekta ya gesi.
Ghasia aliyasema hayo kwenye ziara ya kamati hiyo kwenye miradi mbalimbali ya  gesi mkoani Mtwara yenye lengo la kujionea mafanikio na changamoto zake.
Alisema Serikali imekuwa ikisomesha vijana katika  masuala ya gesi na mafuta, ndani na nje ya nchi lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa vijana wanakuwa sehemu  ya umiliki wa  uchumi wa gesi asilia.
Aidha, katika hatua nyingine, alishauri  Shirika la Maendeleo ya Petroli  Tanzania (TPDC) kuendelea na mikakati ya kuwa programu za mafunzo ya mara kwa mara kwa wataalam hao kwa kuwa teknolojia inabadilika kila wakati.
“ Vijana wanaofanya kazi nzuri katika kiwanda hiki ni vyema wakahudhuria mafunzo ya mara kwa mara ili kuendana na teknolojia inayobadilika mara kwa mara.
Pia alishauri maslahi kwa ajili ya vijana wanaofanya kazi katika kiwanda hicho yakaendelea kuboreshwa zaidi ili kuwapa motisha wa kazi zaidi.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s