SINEMA YA SITTI MTEMVU YA ENDELEA………


Mshindi wa Miss Tanzania 2014 Sitti Mtemvu, kwa hiari yake mwenyewe bila kulazimishwa na mtu ameamua kulivua rasmi taji hilo la urembo.

Akiongea na EATV mratibu wa shindano hilo Hashimu Lundenga amesema kuwa Sitti Mtemvu ameamua kwa maamuzi yake binafsi na sio wao kama kamati ya Miss Tanzania.

“Sababu kubwa ya Sitti kulivua taji hilo ni baada ya kuchoshwwa na maneno mengi yaliyozushwa juu yake, maana pia aliitwa na RITA kwaajili ya uchunguzi zaidi hivyo ameona mambo yanazidi kuzushwa mengi hivyo ameamua kulivua taji hilo”. Amesema Hashimu Lundenga.VICTOR SIMON/mjengwablog