Rais Dk.AShein akutana na Balozi wa Urusi


Daktari.
Dr. Mayige ameendelea kwa kusema yakuwa wameona ni vyema kwa kituo hicho kuwa hapa Dar es
Salaam kwasababu Dar es Salaam kuna ongezeko kubwa la watu wenye matatizo ya shinikizo la damu,
magonjwa ya Moyo na Kisukari na hii imesababisha kuwa na ongezeko kubwa la hitaji la huduma za
kudhibiti na kuzuia magonjwa hayo. Magonjwa haya yanahitaji kituo maalum ili kuweza kutoa huduma
na elimu kwa watu wote wenye matatizo hayo.
Inasemekana kuwa kuna zaidi ya milioni 347 ya watu duniani kote wanaishi na ugonjwa wa Kisukari.
Mwaka wa 2004, watu milioni 3.4 walikuwa na ugonjwa wa Kisukari. Zaidi ya asilimia 80 ya vifo
vinavyotokana na Kisukari hutokea katika nchi maskini. Shirika la Afya Duniani (WHO) wanasema
kwamba ifikapo mwaka wa 2030, ugonjwa wa Kisukari utakuwa ni sababu ya saba (7) ya vifo duniani.
Katika bara la Afrika, ugonjwa wa Kisukari ni tatizo kubwa na linalokuwa siku baada ya siku. Inafikiriwa
ya kuwa mmomonyoko wa lishe ya kitamaduni na kutokuwa na mazoezi ya mwili ni chanzo kikubwa cha
ongezeko la tatizo hili au ugonjwa huu wa Kisukari.
Kwamujibu wa tafiti zilizotolewa mwaka wa 2000, ongezeko la ugonjwa wa Kisukari linazidi kukuwa
kutoka asilimia moja (1%) katika miaka ya 1980 mpaka kufikia asilimi sita (6%). Inakadiriwa kuwa katika
nchi za Afrika pamoja na Tanzania, ongezeko hili litakuwa zaidi ifikapo mwaka wa 2030. Ongezo la
ugonjwa huu wa Kisukari linamaanisha kuwa asilimia wa watu wenye umri kuanzia umri wa miaka ya 20
mpaka 79 wana Kisukari aina ya kwanza au aina ya pili ya Kisukari. Watu wengi Tanzania wapo katika
hatari kubwa ya kupata ugonjwa wa Kisukari na Shinikizo la Damu kwasababu ya mpangilio mbovu wa
lishe/chakula na kutofanya mazoezi.
Kisukari ni nini?
Kisukari ni ugonjwa unaotokana na kuwa na kiasi kikubwa cha sukari katika damu, na hii inasababishwa
na kongosho kuzalisha kiwango kidogo cha kichocheo cha insulin, au insulin haipeleki sukari
inayohitajika katika seli/chembehai. Sababu zote hizo zinaweza kusababisha Kisukari. Mgonjwa wa
Kisukari hupata matatizo ya kujisaidia haja ndogo marakwamara, hupata kiu kisichoisha na kikali, na pia
mgonjwa huhisi njaa kali marakwamara

 

IMG_3301 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimia na Balozi wa Shirikisho la Urusi Nchini Tanzania Alexander A.Rannik,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.] IMG_3306Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Balozi wa Shirikisho la Urusi Nchini Tanzania Alexander A.Rannik,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.] IMG_3327Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na  Balozi wa Shirikisho la Urusi Nchini Tanzania Alexander A.Rannik,baada ya mazungumzo yao alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

Hebu Cheki Taswira Rasmi Kutoka IKULU Wakati Rais Jakaya Kikwete Alipolihutubia Bunge Mjini Dodoma


 

Rais Jakaya Kikwete akilihutubia Bunge Jana Mjini Dodoma.
 Baadhi ya wabunge wakimsikiliza kwa makini Rais Kikwete Bungeni jana
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisaini Kitabu cha Wageni katika ofisi ya Spika Jana muda mfupi kabla ya kulihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kushoto ni Spika Mhe.Anna Makinda na kulia ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda.Picha na Freddy Maro-IKULU