MWANASPOT: SIMBA WACHARUKA, WATAKA YANGA IWALIPE SH 50 MILLIONI


MAIMARTHA JESSE: SAFARI HII NATOA GARI KWA MWANAMKE KIGOLITZ 2013


ImageMkurugenzi wa Manywele Entertainment ya jijini Dar es Salaam Maimartha Jesse , leo asubuhi kaniambia kwamba ameamua kutoa zawadi ya gari lenye thamani ya shilingi Milioni tisa kwa mshindi wa shindano la Kigoli TZ 2013 .Shindano hilo la aina yake kwa wanawake wa Tanzania limepangwa kuzinduliwa tarehe 31 mwezi huu katika ukumbi wa Sun Siro huku bendi ya Extra Bongo  ikifanya bududani mbele ya wapenzi wa muziki. Hii blogu ni mdhamini mmojawapo wa shindano hilo.

Gari la polisi lanaswa na bangi


 

 

 

kamandamwema 4e060

Gari aina ya Toyota Landcruiser linalotumiwa na Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), Mkoa wa Arusha, lilikamatwa juzi mjini Moshi likiwa limesheheni magunia 18 ya bangi.

Habari za awali zilieleza kuwa gari hilo lilikamatwa juzi saa 4:00 usiku katika Mji mdogo wa Himo, Moshi Vijijini likisafirisha bangi hiyo kwenda Tarakea, Rombo.

 

 

Polisi wawili akiwamo dereva wa gari hilo wanashikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Himo na gari lipo Makao Makuu ya FFU, Moshi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz alithibitisha kukamatwa kwa askari hao: “Mchakato wa kuwafikisha mahakama ya kijeshi unaandaliwa. Bangi hiyo ilikuwa inapelekwa kwa mfanyabiashara mmoja huko Rombo na ndiye aliyewakodi.”

Hata hivyo, Kamanda Boaz alisema atatoa taarifa zaidi leo kwani uchunguzi bado unaendelea.

Bangi ilivyonaswa

Habari zimeeleza kuwa polisi waliokuwa doria waliliona gari hilo likitengenezwa na waliamua kuwauliza wenzao kulikoni? Wakajibiwa kuwa kuna kitu walikuwa wakirekebisha na lilikuwa ni tatizo dogo tu.

“Walipoulizwa kwani mnaelekea wapi wakasema wanapeleka mzigo wa bosi huko Tarakea mpakani na kwa taratibu zetu za kijeshi huwezi kuuliza ni bosi gani,” kilidokeza chanzo kimoja ndani ya polisi.

Hata hivyo, polisi hao wa doria walirudi katika gari yao ili waendelee na doria lakini baadhi ya polisi wakamweleza ofisa aliyekuwapo katika gari hilo kwamba wanashuku gari lile limebeba bangi.

“Lilikuwa na harufu kali ya bangi na hilo ndilo lililowafanya wale polisi kurudi tena kwa wenzao na kuwaambia wanataka waone wamebeba nini ndipo wakakutana na magunia 18 ya bangi,” kilieleza chanzo chetu.

Inadaiwa kuwa baada ya kukuta bangi hiyo, polisi hao waliwasiliana na Mkuu wa Upelelezi (RCO), Mkoa wa Kilimanjaro, Ramadhan Ng’anzi ambaye naye alimjulisha Kamanda Boaz.

Ilielezwa kuwa Kamanda Boaz aliagiza kuwekwa mahabusu kwa polisi hao katika Kituo cha Himo na gari hilo lipelekwe FFU, Moshi.

 

MANYWELE ENTERTAINMENT INAKULETEA SHINDANO LA KIGOLI 2013


Image

WARAKA KUHUSU MUSWADA WA BARAZA LA VIJANA LA TAIFA WA MWAKA 2013


 

Mbunge wa Jimbo la Ubungo (Chadema), John Mnyika.

 

Vijana wenzangu na wote wenye dhamira ya kuwezesha maendeleo ya vijana nchini, salaam!

Mtakumbuka kwamba mwezi Januari 2013 nilitoa taarifa kwa umma ya kueleza kuwa niliwasilisha kwa Katibu wa Bunge Muswada Binafsi wa Sheria ya Baraza la Vijana la Taifa na kuomba hatua za ziada toka ofisi ya Bunge kwa kuzingatia Kanuni ya 21 na Kanuni ya 81 ya Kanuni za Kudumu za Bunge.
Toka wakati huo muswada huo mpaka sasa Mei 2013 haujachapwa katika gazeti la Serikali na nimepokea barua toka kwa ofisi ya Bunge kwamba wamepokea ushauri toka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwa muswada huo hauwezi kuchapishwa katika gazeti la Serikali kwa kuwa umekiuka masharti ya ibara ya 99 ya Katiba ya Nchi.
Sababu ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kutoa ushauri huo ni kuwa muswada unalenga pamoja na mambo mengine kupitia kifungu cha 31 kipengele cha kwanza kuanzisha Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kwa madhumuni ya kugharamia shughuli za baraza la vijana la taifa, mipango ya baraza na kutekeleza miradi ya vijana kwa ajili ya maendeleo ya vijana.
Kwa maoni yangu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ametoa ushauri huo bila kuzingatia kwamba kifungu cha 31 kipengele cha pili kinataja vyanzo mbalimbali vya fedha za mfuko ikiwemo kutaja kuwa fedha za mfuko zitatokana na fedha zilizotengwa na Serikali na Bunge kwa ajili ya Baraza kwa mujibu wa Ibara ya 135 kifungu cha pili cha katiba ya Nchi.
Ibara ya 135 (2) ya Katiba ya Nchi inatamka kuwa “fedha ambazo hazitawekwa kwenye Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali ni zile zote ambazo zimetajwa na sheria ya kwamba zitumike kwa shughuli maalum au ziwekwe kwenye mfuko mwingine kwa ajili ya matumizi maalum”.
Hivyo, ni maoni yangu kuwa ibara hiyo ya Katiba ya Nchi inaweza kutumika kuwezesha kuanzishwa kwa Baraza la Vijana na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana bila kufungwa na Ibara ya 99 ya Katiba kifungu cha kwanza ambacho kimeweka masharti kuwa “Bunge halitashughulikia jambo lolote kati ya mambo yanayohusika na ibara hii isipokuwa kama Rais amependekeza kwamba jambo hilo lishughulikiwe na Bunge na pendekezo hilo la Rais liwe limewasilishwa kwenye Bunge na Rais.”
Kifungu cha pili kinataja mambo yanayohusika na ibara hiyo ya 99 ni pamoja na muswada wa sheria kwa ajili ya “kuagiza kwamba malipo au matumizi ya fedha yafanywe kutokana na Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali au mfuko mwingine wowote au kubadilisha kiwango hicho kwa namna nyingine yoyote isipokuwa kupunguza”.
Toka Sera ya zamani ya maendeleo ya vijana ya mwaka 1996 itamke kwamba Serikali itawezesha kuanzishwa kwa Baraza la Vijana na suala hilo kurudiwa katika Sera mpya ya mwaka 2007; miaka takribani 17 imepita marais wote wa awamu husika na mawaziri wenye dhamana hawajawasilisha bungeni muswada huo hali ambayo imenifanya niandae muswada binafsi kuwezesha baraza kuundwa.
Muswada wa Sheria ya Baraza la Vijana la Taifa 2013 niliouwasilisha kwa maoni yangu hauna lengo la kuagiza malipo au matumizi ya fedha yafanywe kutokana na Mfuko mkuu wa Hazina ya Serikali au Mfuko mwingine wowote kwa mujibu wa ibara ya 99 bali unalenga kuanzisha Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kwa kuzingatia masharti ya Ibara ya 135.
Hata hivyo, kwa kuwa muswada huu unahusu mustakabali wa vijana na ni suala la kitaifa kupitia waraka huu naomba kupata maoni yenu kuhusu suala hili, mapendekezo ya marekebisho yanayohitajika kufanyika na hatua zinazopaswa kuchukuliwa.
Maoni, mapendekezo na hatua hizo zitumwe kupitia mbungeubungo@gmail.com au kwa Afisa wa Ofisi ya Mbunge Ubungo Gaston Garubimbi (0715825025) kabla ya tarehe 24 Mei 2013.
Nakala ya rasimu ya muswada wa Baraza la Vijana la Taifa wa mwaka 2013 inapatikana katika mtandao wa http://mnyika.blogspot.com kwa ajili ya rejea.
Aidha, nawaalika kushiriki mikutano ya kupokea maoni kupitia mtandao huo tarehe 20 mpaka 23 Mei 2013 saa 9 alasiri mpaka 10 Jioni ambayo nitashiriki na kutoa maelezo ya zaidi kwa kadiri itakavyohitajika.
Natarajia kupokea maoni ya vijana na wananchi wengine bila kujali tofauti mbalimbali kwa kuwa madai ya kutaka kuundwe Baraza la Vijana la Taifa yamekuwa yakitolewa na vijana, asasi na taasisi kwa muda mrefu.
Vyama vya siasa kwa kuzingatia matakwa hayo viliahidi kutekeleza azma hiyo kwa mfano Ilani ya CHADEMA ya mwaka 2010-2015 kipengele 6.4.1 (viii) ilitamka “Kwa kuwa vijana ndio kundi kubwa hapa nchini, na kwa kuwa uhai wa muda mrefu wa taifa letu upo mikononi mwa vijana, Serikali ya CHADEMA itawezesha vijana kuunda Baraza la Vijana (BAVITA) ambalo limekwamishwa na Serikali ya CCM kwa muda mrefu”.
Kwa upande mwingine, Ilani ya CCM ya mwaka 2010-2015 iliahidi katika kipengele 80 (k) “Kuhamasisha ushiriki wa vijana katika ngazi mbalimbali za maamuzi ikiwa ni pamoja na kukamilisha uanzishaji wa Baraza la Vijana”.
Mwaka 2011 niliihoji Serikali bungeni ni lini itakamilisha uanzishwaji wa baraza hilo na ikaahidi kwamba kazi hiyo itakamilishwa katika mwaka wa fedha 2011/2012 hata hivyo sasa ni Mei 2013 Serikali haijakamilisha.
Hivyo vijana, wabunge na wananchi kwa ujumla ni muhimu kuboresha muswada huo na uwasilishwe bungeni kuwezesha baraza la vijana na mfuko wa maendeleo vijana kuanzishwa; maslahi ya umma kwanza.
Wenu katika uwakilishi wa wananchi,
John Mnyika (Mb) 
19 Mei 2013 
Dodoma

Muswada wa Baraza la Vijana 2013-Rasimu ya Kwanza; pakua hapa (download here):
https://docs.google.com/file/d/0B8xvLNf5FlohSHJPX2trR3p6YzQ/edit?us…

FLORA BAHATI LYMO NI MWANAMKE ANAYEDAI KUBAKWA NA MBUNGE WA CHADEMA


BINTI mrembo aitwaye Flora Bahati Lyimo anamtuhumu mbunge mmoja wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaloongozwa na Spika Anne Makinda kuwa amembaka
 

Katika uchunguzi wake, hivi karibuni ,Uwazi lilielezwa kuwa kuna habari ya kashfa nzito inayomtafuna mbunge huyo anayetokea Kanda ya Kaskazini lakini haikufafanua kwamba inahusu nini.
Baada ya kutulia na kupekua kwenye vyanzo vyake, Uwazi lilibaini kuwa kashfa inayomlenga mheshimiwa huyo ni ya ubakaji na tayari imefikishwa mahakamani huko London nchini Uingereza.

 

 

 

 

 

Habari hiyo ilielezwa ‘kijuujuu’ hivyo uwazi likamtafuta Flora ambaye ni Mtanzania anayetokea mkoani Kilimanjaro ambaye anaishi katika Jiji la London kikazi.
Alipopatikana Flora alibanwa kisawasawa ndipo akaibua mazito huku akieleza tukio zima lilivyofanyika kwa data na vielelezo vya kila aina ikiwemo barua ya Mahakama ya Crown ya London.
 

 

 

 

“Ni kweli mheshimiwa … (anamtaja jina) alinibaka Agosti, mwaka jana. Yeye na makada wenzake wa chama chake walikuja hapa London kwa ziara ya kichama na kwa kuwa mimi sina chama nilikwenda kuhudhuria mkutano wao kwa kuwa nina mtandao wangu (blog) hivyo nilitaka kupata habari za kuingiza kwa sababu ni za watu wa nyumbani (Tanzania).

 

 

 


Akiendelea kuweka wazi kisa hicho, Flora anasema: “Nikiwa kwenye mkutano….(jina la mbunge) alinifuata akaniuliza nimeandika watu wangapi waliohudhuria mkutano huo, nikamjibu 50 akaniambia niongeze idadi hiyo ili ionekane mkutano ulikuwa na watu (Watanzania waishio Uingereza) wengi.
 

 

“Hapo ndipo alipoanza kunizoea. Alitaka kunipa kadi ya chama chake  nikakataa, ndipo akadai kwamba mimi nilitumwa kwenye mkutano huo na balozi na rais kwa ajili ya ushushushu.


“Mkutano ulimalizika, sasa nilipokuwa naondoka kurudi nyumbani kwangu, mbunge huyo na wenzake nao walitoka. 

 

 

 

 

 

Tukiwa njiani wenzake walikwenda kujisaidia haja ndogo, yeye akaniomba akajisaide nyumbani kwangu, nilimkubalia. 

 

 

 

 

 

Alipofika ndani, bila kujua kila kitu kinaonekana kwenye kamera alinibadilikia kama vile adui vitani, ona sasa wema wangu ukawa umeniponza.


Alinirukia, akaniburuza hadi kitandani kwangu. Nilipokuwa mkali na kwa namna nilivyokuwa nimechanganyikiwa sishikiki ndipo akanivamia maungoni, akanichania nguo zangu akitaka nimwachie atimize lengo lake la kuniingilia kimwili kwa nguvu.
 

 

 

 

“Nilijitahidi ili asifanikiwe, nikamwambia amekwisha kwani lazima nimwanike ndipo akanipiga nusu aniue akisisitiza kuwa kama nitauanika uovu wake huo au kuchukua hatua zozote ataniua.
 

 

 

 

“Inaniuma sana, kunibaka anibake halafu atishie kuniua, unyama gani huu?”
Flora anaendelea kusema:
“Katika purukushani hiyo, nilipopata mwanya kidogo tu, nikapiga namba ya polisi 999 kuomba msaada. Alipoona hivyo alitoka na kutokomea kusikojulikana. Polisi walipofika hawakufanikiwa kumkamata.”

Flora alisema polisi walimchukua na kila kitu cha ushahidi zikiwemo nguo zake hadi kituoni, wakamhoji kwa kumrekodi sauti, wakampa namba ya jalada la kesi inayosomeka; 4621279/2012-UBAKAJI/KUTISHIA KUUA ambapo hadi leo mbunge huyo anasakwa na Polisi wa London, akikanyaga tu Uingereza lazima akamatwe akajibu tuhuma za ubakaji na kutishia kuua.
 

 

 

 

Flora akaongeza: “Ukweli ni kwamba hakufanikiwa kukamatwa kwa sababu alikuwa na passport za kidiplomasia ambazo nyingine hakutumia jina lake halisi.

 

 

 

“Kesho yake nilisikia alikimbilia Ujerumani, nikawaambia polisi lakini walikumbana na tatizo lile kwani majina niliyowapa siyo aliyotumia kuingia Ulaya.
 

 

“Januari mwaka huu nilipotaka kurudi nyumbani Kilimanjaro, mahakama ya hapa (Uingereza) ilinipa barua ambayo nilipofika niliipeleka Kituo Kikuu cha Polisi Moshi nikafunguliwa faili Namba Mos/RB/17127/12 kwa ajili ya ulinzi chini ya R.C.O Ramadhan Ng’anza.

 

 

“Niliwaeleza kuwa mtu anayetaka kuniua ni mbunge huyo. Kweli waliahidi kunisaidia, nilipoondoka kurudi London niliwasiliana na polisi Kilimanjaro lakini niliona kama kuna kitu au mbunge huyo yupo juu ya sheria kwani walikana kunifahamu.
“Sitachoka kutafuta haki na kutetea wanawake wanaobakwa kila siku wanaona aibu kusema, naamini aibu haipo kwa mbakwaji bali kwa mbakaji, yule …. (anataka jina) ni mbakaji.
 

“Nimesharipoti mashirika mengi ya haki za binadamu ya Uingereza. Kuna siku nilishinda mahakamani, kule ni yeye tu anasubiriwa atiwe mbaroni akasimame kizimbani ndipo dunia itajua ninachokisema.”


Flora allisema kama kweli mbunge huyo ni mwanaume aende tena jijini London kama hatasimamishwa kizimbani na kuozea jela.”
 

Chanzo: Gazeti la uwazi

Rais Kikwete katika Sherehe za Kuapishwa Askofu Mkuu wa Anglikana Tanzania akutana na Skofu wa Cantebury


 

 

8E9U5797Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania aliyemaliza muda wake Dkt.Valentino Mokiwa(katikati) akimtambulisha kwa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete  Askofu Mkuu wa Canterbury Justin Portal Welby muda mfupi kabla ya kuanza kwa ibada ya kumtawaza askofu Mkuu Mpya wa Kanisa hilo hapa nchini Askofu Jacob Erasto Chimeledya iliyofanyika katika Kanisa kuu la Roho Mtakatifu Dodoma. 8E9U5921Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana nchini aliyemaliza muda wake Dr.Valentino Mokiwa akimtawaza aksofu Mpya wa Kanisa hilo Askofu Dkt. Jacob Erasto Chimeledya wakati wa ibada iliyofanyika katika kanisa Kuu la Roho Mtakatifu mjini Dodoma leo. 8E9U6203Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Askofu Mkuu Mpya wa Kanisa la Anglikana nchini Askofu Dkt.Jacob Erasto Chimeledya wakati wa ibada ya kumtawaza kuwa askofu Mkuu iliyofanyika katika kanisa Kuu la roho Mtakatifu,mjijni Dodoma Leo(picha na Freddy Maro).

Follow

Get every new post delivered to your Inbox.

Join 4,718 other followers

%d bloggers like this: